Profesa Tibaijuka: Trump kusitisha misaada ARVs zitaadimika Afrika. African Union iitishe kikao maalum kuweka mkakati

Safi sana, asitishe, kwaninimpaka leo hii tutegemee wazungu?

Hakuna cha kuitisha mkutano wala nini, tumieni fursa ya kufungua viwanda vyenu vya dawa na muwachae uasherati, uzinzi na ushoga.
 
Kiama gan wakati asilimia kubwa ya hela ya misaada inaishia mifukoni mwa viongozi. Nashangaa kuendelea kutupa misaada huku wakijua hela zao zinaliwa. Na mataifa mengine makubwa yafuate mfano wa Trump.
Kwani unafikiri hilo hawalijui toka tangu na tangu, data zote zote zoooote wanazo Mobutu Se alipewa vibunda vya kutosha na ..... halafu huyo huyo ..... akaja akamchomoa madarakani
 
Kwanini tutegemee USA in the first place ?!!!


Ufike wakati kama Afrika tuanze kujitegemea nchi kama India watu wakishagundua hizo Dawa watu wanaingia maabara na kutengeneza copies ya dawa kama hizo kwa kutumia brand name nyingine haya mambo ya kutegemea misaada wala in real sense sio misaada sababu wanachokunyonya ni kikubwa zaidi. Alisema Sankara; 'He who feeds you, controls you'
 
Kwahiyo Huyu Mama kaamua kuwatisha Watanzania.
Huyu Mama ana Roho Mbaya sana...ni shetani kabisa.
 
kwaiyo watu waache kula arv badala yake wakale mbogamboga au sio?
Hapana, acha kula mboga mboga, kula ARVs asubuhi kama kitafunwa, kula mchana kama mboga, na kula usiku kama dinner.., kula kama chakula tu..

Ila ,
-kama unataka kufubaza virusi, kula ARVs,

- Kama unataka kupandisha kinga, kula mlo kamili

- kama unataka vyote, kula vyote..

- Kama unataka kufa kwa failure ya ini na figo, kula ARVs
 
Mimi nilliiona hili na nikawaonya watu,baada ya watu kusema kuwa sasa ngoma ni kama mafua tu, nikasema kwasababu sisi Waafrika ndio tunaongoza kuwa na wagonjwa wengi iko siku atatokea Racist mmoja huko....
He isn't the only...
Ni mpuuzi tu mmoja..

Na anaweza akafa muda wowote pia..
 
Rais mpya wa marekani ametangaza kusitisha misaada ( foreign aid ) iliyokuwa ikitolewa na nchi yake kwa nchi zinazoendelea kupitia mashirika yake na program za USAID, PEPFAR, ubia na WHO na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali.
Hili jumba bovu linakwenda kuwaangukia watu wanaofanya kazi katika miradi inayosimamiwa na mashirika haya. Kwa hapa Tanzania hawa ni baadhi ya watu waliokuwa wanatengeneza kipato kizuri na cha kuheshimika( decent income ) . Since COVID 19 nilijifunza umuhimu wa kuwa na escape plan unapofanya kazi na NGO’s , pamoja na kipato kizuri kilichopo huku, game huwa linabadilika ndani ya sekunde .
 
Inatubidi tuamke kwakweli. Watoa misaada wametugwaya.
Tumezidi ombaomba
Halafu wangekata misaada zamani kwa sababu nchi masikini kuna majizi sana yenye madaraka makubwa na hao ndio wanavuruga kwa wizi wao
Na sisi hatutaamka kama wanatupa misaada kila leo
Ni kama mtu anakaa kwa baba yake miaka yote analipiwa kila kitu yeye kazi yake kubwa ni kalala tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…