Professional Players:

Professional Players:

Mario Kejob

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2020
Posts
441
Reaction score
536
Kama tuliona wachezaji wazawa hawafai kwa namna fulani, now it's a high time to bring in professional referees kwani hawa wazawa wamekuwa ni kizungumkuti.
Mechi ya derby ya Simba na Yanga ijayo, tafadhalini sana tuleteeni marefa wa kimataifa maana hawa marefa wetu wa Gambosh hawajui kuzitafsiri sheria 17 za FIFA. Gharama ya kuwaleta italipwa kwa kuweka ongezeko la shilingi 500 kwa kila tiketi. Ikumbukwe kwamba ligi yetu inafuatiliwa na ukanda mzima wa Afrika Mashariki na kati hivyo ni aibu kuyaonyesha madudu yetu huko.
 
Hakuna Refa ambaye hatakosea labda wanunue teknolojia ya VAR.
 
Kwa bahati mbaya ni kwamba marefa wote waliopo duniani ni wanadamu, hakuna hata refarii ambao ni malaika. Hivyo makosa ya kimaamuzi hayawezi kuepukika na ndio maana ligi za ulaya wameweka VAR pamoja ya kwao wao ni wazungu wenye upeo na akili na maarifa zaidi lakini wameshindwa kutafsiri sheria 17 za soka kwa weledi zaidi. Hao wenzetu wenyewe kuna VAR lakini bado wanakosea pia.
 
Refa hana beji hata moja kama mimi tu
 
Kuna makosa ya kibinadamu na kukusudia marefa wa bongo wanafanya mambo kwa kukusudia hii ni mara ya pili naunga mkono iongezwe miatano kwenye tiketi walete marefa wa nje tumechoka na upotolo wao
 
Hilo wazo sidhani kama utopolo watakubaliana nalo maana wanafaidika sana na makosa ya refa
 
Refa mtawalaumu bure kabisa. Tatizo hamtaki kuwaamini wanasukumwa sukumwa na TFF kutokana na shinikizo la team hizo mbili.

Na wao wanakosa kujiamini wakichezesha mechi hizo sababu hawaaminiwi pia.
 
Back
Top Bottom