NgimbaErick

Senior Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
108
Reaction score
167
Hello, je umeanzisha Kampuni au Biashara mpya na unatamani kuwa na website itakayobeba kampuni au biashara yako? au unayo Kampuni au Biashara muda mrefu tu, lakini umekuwa ukitamani kuwa na Website ili kukuza unachofanya?

Basi, naomba kusema kuwa nafasi ndio hii sasa, ya kubadilisha Biashara yako kwenda viwango vingine kwa kutumia Mtandao (internet).

Kwa Tsh. 370,000 tu, ntakutengenezea Website ya Kipekee na ya Kisasa, ambayo itafanya watu wengi waiamini Kampuni au Biashara yako.


Tegemea Kunufaika na Haya Mara Baada ya Kuwa na Website Nzuri na ya Kisasa.

  • Kampuni au Biashara yako Kutambulika na Watu Wengi Kupitia Mtandao
  • Watu Kukuamini Mara 10 Zaidi
  • Kuifanya Kampuni yako kuwa Mbele ya Washindani Wako
  • Kuwapa Msaada wa Masaa 24 Wateja Wako bila ya kufanya kazi ya ziada
  • Kuitangaza Biashara Yako bila Kufanya Kazi yoyote
  • Kupata Wateja na Wafuasi Wapya kwa Urahisi kila Mahali
  • Kukusanya Taarifa za Wateja au Wafuasi wako kwa urahisi zaidi, kwa maendeleo ya unachokifanya
  • Kuboresha Kile Unachofanya kupitia Maoni ya Wateja Wako kwenye Website n.k


Website hiyo itahusisha:
  1. Kurasa 1 mpaka 3
  2. Muonekano wa Kipekee (sio template)
  3. Kukutengenezea Content Mpya
  4. Emails za Biashara
  5. Ramani ya Google (kuonesha ofisi yako kwa watu)
  6. Huduma ya SEO (Kukusaidia kuonekana Google mapema)
  7. Kuunganisha Fomu ya Mawasiliano
  8. Na mengine mengi ya ziada ...


Gharama za Huduma ya Hosting na Domain ni juu yako, kwani hizo ni sawa na Mafuta kwenye Gari ... huwa zinapatikana kwa gharama ndogo kama Tsh. 150,000 tu kwa Mwaka Mzima!

MUHIMU: Huitaji kusubiri usajili wa Biashara ili kumiliki Website mtandaoni, huu ni ulimwengu mwingine unaojitegemea. Kwahiyo ondoa shaka kabisa.


Kwa Huduma au Maelezo Zaidi, Napatikana kwa Mawasiliano haya;

Simu namba: 0787 140 943
Email: hello@erickngimba.tech
Website: www.erickngimba.tech

BAADHI YA KAZI ZANGU


Tekorex Co. - TAZAMA WEBSITE

1.




2.




3.



Capital Machinery Company ltd - TAZAMA WEBSITE

1.




2.




3.




Erick Ngimba - TAZAMA WEBSITE



 
Je biashara ya mtaji gani inayohitajika kuwa katika website
 
Unaweza kutuwekea links za site ulizowahi kutengeneza?
 
Unazungumzia aina ipi ya biashara mkuu!?

Mimi nina duka la Mangi, nawezaje kujitangaza akati wateja wangu wanapatikana ndani ya eneo langu?
 
Gharama ya kulipia website kwa mwaka ni kiasi gani???
 
Unazungumzia aina ipi ya biashara mkuu!?

Mimi nina duka la Mangi, nawezaje kujitangaza akati wateja wangu wanapatikana ndani ya eneo langu?
unavyoiona biashara yako basi ndivyo ilivyo, sijfahamu una mipango gani... lakini kama mpango wako ni kufikia watu wachache wanaokuzunguka basi haina haja.. ila kama una mipango ya kuwa supplier mkubwa basi andaa mipango ya kufika juu, usiangalie hali uliyonayo sasa ivi tazama unapokwenda...

wapo wengi walioanza kama wewe, na wapo mbali sasa.... na sijasema ni lazima kila biashara kuwa na website, ila ni muhimu kwa dunia ya leo ukiwa kama mfanyabiashara mwenye malengo ya kukua kiuchumi.
 
Mkuu hiyo Website yako ya mafunzo malizia somo kuunganisha domain na host kama ahadi yako
Sawa sawa, nitajitahidi ndani ya wiki ijayo nimalize kila kitu nianze somo jingine... maana nlikuwa busy kidogo,,
 
Sawa sawa, nitajitahidi ndani ya wiki ijayo nimalize kila kitu nianze somo jingine... maana nlikuwa busy kidogo,,
Bwana Erick hongera sana naona kazi ya TanV ipo vizuri.

Hebu niambie kutengeneza website km hiyo unacharge sh ngapi??

Je web inaweza kuwa na contents nyingi zaidi ya hapo?

Je kwa kumiliki website yangu naweza kupata mapato kwa watu kuitembelea??Je waweza kutoa mfano hapa wa kile mtu anachoweza kuingiza kwa idadi gani ya watumiaji wanaoitembelea.

Naomba kuwasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

1. Hapo mwanzo nlikuwa nikicharge baada ya kazi kuisha ndiyo napiga mahesabu... lakini sasa ivi nimeamua kuweka packages ili kuweka urahisi kwa wote.

so, iko ivi:

- Local Businesses and Small Companies: Tsh. 340,000 ( inachukua siku 3 mpaka 7)
- Blog: Tsh. 380,000 ( Inachukua siku 5 mpaka 9 )
- Organizations and Institutions: Tsh. 460,000 ( inachukua siku 5 mpaka 11 )
- Ecommerce site: Tsh. 570,000 ( inachukua siku 10 mpaka 15 )


2. Website inaweza ikawa na content nyingi utakavyo wewe, tena inapendeza zaidi.

3. Ndiyo, unaweza ukaingiza kipato kwa watu kuitembelea tu.. kuna namna mbili.
a. Unaweza ukajiunga na Adsense, ambapo Google wataruhusu watu watumie website yako kutupia matangazo yako na kisha wanakulipa automatic, na kiasi unacholipwa wanaamua Google wenyewe.
b. Unaweza ukawa kama influencer endapo website yako itakuwa inatembelewa na watu wengi, kwamba ukaruhusu watu kuja kutangaza kwenye website yako, ila gharama unazipanga wewe mwenyewe.


4. Mfano.... Ntakupa mfano kwa Adsense makadirio yao, ila inabidi ufahamu kwamba hawaangalii idadi ya watumiaji wanaoitembelea..
- Wanaangalia ni mara ngapi page yako ya website imeangaliwa, hata kama unatembelewa na wastani watu 200 kwa mwezi, lakini wanaifungua page za website yako, zenye matangazo, mara tano kwa siku, basi itahesabika umetembelewa mara 1000 kwa siku, au mara 30,000 kwa mwezi..... Hivyo watakulipa kwa kuangalia ni mara ngapi ukurasa wa website yako umeangaliwa.

- pia wanatazama sana na website yako inajihusisha na nini, yani.. website inayohusika na mambo ya afya malipo yake ni tofauti na website inayohusika na mambo ya michezo.

- Vile vile na wanaangalia na Taifa unalotokea, malipo kwa wamarekani sio sawa na waafrika hata kama mnapata idadi sawa kwa mwezi, kwa sababu marekani watu wanauwezekano mkubwa wa kubonyeza hayo matangazo (Higher Conversion Rate) kuliko watu wa afrika.
- Google ads, wastani wanalipa %68 kwa mwenye website, yani mtu akilipia 100 kwa google ili atangaziwe biashara yake, basi 68 inakwenda kwa mwenye website, ambapo tangazo liliwekwa.

- kwa kawaida Adsense hulipa $0.10 mpaka $0.30 kila mara ukurasa wa website yako wenye matangazo utakapoangaliwa hata kama mtu huyo huyo akaufungua ukurasa huo mara tano. Lakini wastani ni $0.18 , kwahiyo kama ukurasa wako utatazamwa mara 30,000 kwa mwezi inamaana utalipwa, $5,400.
 
Hivi unaijua adsense vizur??
endelea kutngenezs website kijana google hawawez kukulipa kiasi hicho kwa kila views watu eote wenye adsense wangekuwa wanaendesha Range mjini.
 
Hivi unaijua adsense vizur??
endelea kutngenezs website kijana google hawawez kukulipa kiasi hicho kwa kila views watu eote wenye adsense wangekuwa wanaendesha Range mjini.
Acha kupinga brother leta data. Hizo ni taarifa nlizozikuta kwenye Page yao ya adsense so we una taarifa zipi ...

kumbuka kama huna traffic wa kutosha usitegemee vikubwa tena kama visitors wako wanatokea hapa ndani au nchi za afrika ndo kabisa huwezi kulipwa sawa na mtu anayepokea traffic wa nchi zilizoendelea.
 
Adsense yangu ya kwanza ilikuwa approved mwaka 2013 mwez wa 8 nikiwa nasubr kuingia university na kuanzia hapo ndo nikaanza kujifunza zaid online programs so hyo adsense tushavuta sana hela western union tena kpnd cha nyuma mpaka proxy tulikuwa tunatumia na account hazifungw tofaut na sasa.
Adsense imekuwa ngumu sana now days kupga mzigo mkubwa labda kwa dola 100 kama una traffic ya kueleweka utapata kwa mwez.
Ndo maana weng wenye blog za mwanzo walipga chn wengne tukaamia kwenye affiliate marketing so Am talkin what i'm practice.
siku hz ili upate sana pesa kwa adsense lazma ukubali kusoma sana SEO lacvyo itakuwa tu historia kupata pesa mtandaon, kwa yyte mwenye blog atakubaliana na mm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…