Kwanza nakushukuru sana mleta hii threads,ila hata mimi naona kama wapenda mageuzi ya kweli tumechezewa shere,inabidi CHADEMA waliangalie hili kwa umakini na walitolee TAMKO,
Kwa faida ya Watanzania wote, nadhan tungeenda mbali zaidi kwa kutaja hata nafasi wanazoshika hao wanachama hai wa CCM,walijichomeka/waliochomekwa (hasa wale wanaoshika nyadhifa kubwa ndani ya chama kipindi hiki) kwenye makundi mengine nje ya lile la Vyama vyenye usajili wa kudumu,,
Mimi naanza kwa kutaja nafasi zao wanazoshika sasa katika chama cha CCM
Mzee Hassan Mohamed Wakasuvi-M/kiti CCM Mkoa wa Tabora
Bi Jesca Msambatavangu-M/kiti wa CCM-Mkoa wa Iringa
Paulo Makonda -Katibu wa UVCCM-Taifa,Uhamasishaji na Chipukizi
Mtabibu Zainabu Amir Gama-huyu alikuwa mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini kipitia CCM,bunge lililopita.
Pia ni kweli mtu kama Kajubi Mukajangwa wa Baraza la Habari ana malengo sawa na watu vyama vya siasa?...
Hapa kuna USANII wa KUTISHA!!