Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu
Msanii Profesa Jay amesema baadhi ya Watu wanaowashambulia Wasanii kama Ay na wengine kutokana na kupanda kwenye majukaa ya Vyama vya siasa, hawawatendei haki kwasababu Tanzania ni nchi ya Kidemokrasia.
Kwenye mahojiano maalum na Mtangazaji Millard Ayo, Profesa Jay ameeleza yafuatayo
“Hata Wasanii wenyewe pia wana upande wao na wanaruhusiwa kuwa na upande, Mtu wa CCM au CHADEMA popote anapoweza kuwa, ACT, akawa CUF, akawa NLD, akawa CHAUMMA na vitu vingine kama hivyo kwahiyo ni haki yake ya kimsingi, ameamua kui-support CCM ai-support CCM lakini sisi wengine tumeamua kubaki na CHADEMA kwa sababu ni haki yetu ya kimsingi pia”
“Utaona hata mimi nimesaidiwa sana na Watu wa CCM ingawa mimi niko CHADEMA kwa sababu ubinaadamu unakuwa upo mwanzo kwanza kabla ya vitu vingine kuendelea, cha kwanza ni utu"
"kwahiyo Watu kumshambulia AY kwa kuonekana kwenye majukwaa ya CCM sidhani kama ni haki, hawamtendei haki kwakweli kwa sababu ni haki yake ya kikatiba kuchagua upande anaoona yeye unafaa, hata sisi kuna Wasanii wengi wapo upande wa CHADEMA”
“Mimi pamoja na kwamba nipo CHADEMA lakini pia nilisaidiwa na Watu wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mama Samia Suluhu Hassan yeye alinisimamia matibabu yangu mwanzo mpaka mwisho lakini pia Makamu wa Rais Dr"
"Mpango alituchangia, Waziri Mkuu Majaliwa pamoja na kuja kuniona alituchangia milioni 10, Naibu Waziri Mkuu Dr. Biteko pia alituchangia milioni 10, tulienda Bungeni Dr. Tulia aliongoza Wabunge wakatuchangia milioni 5, lakini pia Katibu Mwenezi wa wakati ule Paul Makonda alituchangia milioni 20, Waziri wa Maji Aweso pia alituchangia milioni 10 yeye na Wizara ya maji”