Professor Nabi Akiri Kikosi ni Kipana, Kupanga kikosi ni Kazi nzito

Professor Nabi Akiri Kikosi ni Kipana, Kupanga kikosi ni Kazi nzito

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
KOCHA wa Yanga, Nasreddine Nabi amechekelea aliposikia rasmi mshambuliaji wake Stephane Aziz KI, ameshatua nchini na kutambulishwa lakini akafichua na jeshi alilonalo kuna kazi nzito msimu ujao.

Akizungumza na Mwanaspoti kwa njia ya simu akiwa Tunisia alipokwenda kwa mapumziko mafupi, Nabi alisema amekuwa na amani ya moyo baada ya kumuona Azizi KI akitambulishwa na sasa rasmi atakuwa naye kwa msimu ujao.

Nabi alisema Azizi KI ni mshambuliaji bora ambaye anakwenda kukamilisha ubora mkubwa ambao watakuwa nao kwa msimu ujao katika safu yao ya ushambuliaji.

“Niliwaambia kwamba atafika, nilihakikishiwa na Ghalib (Said) kabla ya kuondoka hapo Tanzania, mchezaji mwingine bora ameongezeka katika kikosi chetu,” alisema Nabi na kuongeza;

“Naamini ujio wa Azizi KI utatupa nguvu nyingine kubwa sana kuekekea msimu ujao ambao nauona utakuwa mgumu zaidi, kila timu inajipanga sawasawa, tutakuwa na safu bora ya ushambuliaji kwa ujio wa mchezaji huyu.”

Aidha Nabi alisema akiangalia usajili wao mpya na mastaa waliosalia kutakuwa na ushindani mkubwa wa nafasi kazi ambayo itaongeza presha kubwa hata kwao makocha

Alisema amekuwa akijaribu kupanga timu hiyo kwenye makaratasi lakini amebaini sio kazi rahisi kwa kuwa wana timu bora zaidi kuekekea msimu ujao.

“Niko hapa nyumbani kuna wakati najaribu kutengeneza mipanmgo yangu kulingana na wachezaji tulionao lakini nikwambie tuna timu kubwa kuna presha kubwa pia kupanga hii timu,” alisema Nabi na kuongeza;

“Nafahamu sio kila wakati unaweza kuwa nao wote wakiwa kwenye ubora lakini pia kuna wakati watakuwepo wote na mbaya zaidi wakawa wote wanataka kucheza lazima uwe na saikolojia nzuri kwa kuzungumza na mchezaji anayebai nje, tuna timu bora sana.”

Yanga inatarajia kuanza kambi ikiwa jiji Dar es Salaam kujiandaa na msimu mpya kabla ya kukipuiga Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Agosti 13, ikiwa ni wiki moja tangu ifanye Wiki ya Wananchi.
 
Timu ikiwa na Nyota wengi inaongeza ushindani na ubora kwenye kikosi.

Kazi ya kocha wa timu kubwa ni pamoja na kukutana na shinikizo kubwa kutoka Kwa wachezaji, mashabiki na viongozi.

Tunaomba Tff waanze mapema mchakato wa maboresho ya viwanja.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] akae ajue mshahara atalipwa kwa awamu, huyo mchezaji anaemsema, kakomba kibubu choteee.
 
nchi hii ngumu sana, hivi uprof wa Nabi ameupatia wapi
Unauliza maswali gani wewe! Mbona huulizi sababu za Mwanamuziki nguli nchini Joseph Haule kujiita Profesa J?

Kama unaona ni rahisi, basi jaribu kujiita Profesa, halafu uone kama kuna mtu atashtuka.

Nabi anaitwa Profesa kwa sababu ya mapinduzi aliyo yafanya tangu ajiunge na Wananchi! Imagine timu yake imemaliza ligi bila ya kufungwa! Timu yake imeifunga timu yako ya simba mara 2 ndani ya msimu! Timu inacheza mchezo mzuri!

Halafu unaumia kabisa Nabi kuitwa Profesa! Uko sawa kweli?
 
KOCHA wa Yanga, Nasreddine Nabi amechekelea aliposikia rasmi mshambuliaji wake Stephane Aziz KI, ameshatua...
Ngoma ikiwambwa sana matokeo yake hupasuka, huyu mnayemsifia leo kwa mbwembwe nyingi mtakuja kumtukana siku sio nyingi... tusome alama za nyakati..
 
Unauliza maswali gani wewe! Mbona huulizi sababu za Mwanamuziki nguli nchini Joseph Haule kujiita Profesa J?

Kama unaona ni rahisi, basi jaribu kujiita Profesa, halafu uone kama kuna mtu atashtuka.

Nabi anaitwa Profesa kwa sababu ya mapinduzi aliyo yafanya tangu ajiunge na Wananchi! Imagine timu yake imemaliza ligi bila ya kufungwa! Timu yake imeifunga timu yako ya simba mara 2 ndani ya msimu! Timu inacheza mchezo mzuri!

Halafu unaumia kabisa Nabi kuitwa Profesa! Uko sawa kweli?
Kama nmekuelewa vizuri Yan baada ya kuja Yanga tu akawa profesa ghafla au
 
Unauliza maswali gani wewe! Mbona huulizi sababu za Mwanamuziki nguli nchini Joseph Haule kujiita Profesa J?

Kama unaona ni rahisi, basi jaribu kujiita Profesa, halafu uone kama kuna mtu atashtuka.
😆😆😆 Nimecheka sana sio kwa jibu hili
 
Kama nmekuelewa vizuri Yan baada ya kuja Yanga tu akawa profesa ghafla au
Uko sahihi kabisa. Na usisahau haya majina hutungwa na wale watangazaji wetu wa Azam na hasa yule Baraka Mpenja.

Mbwembwe nyingi, mpaka jina linazoeleka. Yaani kama vile wanavyomuita Mzamiru Yassin kiungo punda! Dokta Khalid Aucho, Mk14, Screen protector, nk.
 
Ngoma ikiwambwa sana matokeo yake hupasuka, huyu mnayemsifia leo kwa mbwembwe nyingi mtakuja kumtukana siku sio nyingi... tusome alama za nyakati..
Hilo Mkurugenzi mbona liko wazi kabisa duniani kote! Muda ukifika kwa Profesa kuondoka, ataondoka tu! Na Yanga itaendelea kubaki.

Hatokuwa mwalimu milele pale Yanga! Ataondoka kwa namna gani, itajulikana wakati huo huo. Ila kwa sasa wacha aendelee kufurahia matunda ya kazi yake.
 
Back
Top Bottom