Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,752
- 5,609
Mwamba huyu hapa!!
Kwa bahati mbaya anafanya Kazi kwenye nchi ambayo watu wanasubiri ukosee ndiyo wakuzodoe ila ukiwa unafanya mazuri wanafumba macho.
Kwanza ametengeneza timu isiyo na Super star, timu haimtegemei mchezaji mmoja haijalishi unalipwa kiasi gani, una jina kubwa, ulinunuliwa kwa bei gani, unatoka taifa gani.
Mwamba hana maneno wala mbwembwe nyingi bali ameamua kuongea kwa vitendo.
Kipindi anaanza kuanda timu, wengi walimkosoa wakisema timu yake inakata moto kipindi cha pili, wengine wakasema hana tactics za kucheza mechi za kimataifa, mara ooh timu nzima inamtegemea Feisal tu na asipofunga timu haifungi.
Pia kuna maneno mengi ya kejeli yalizungumzwa juu yake hasa na wachambuzi wanaojikuta wao ndiyo wataalam wa soka hapa bongo.
Mwamba Nasreddine Nabi hakuwahi kuwajibu bali alifocus kwenye mipango na malengo yake alijua kuwa akiwasikiliza watamtoa kwenye reli.
Kwa sasa yupo kwenye kilele cha mafanikio ndani ya Klabu ya Yanga, kwani amefanikiwa kuitengeneza timu ya ndoto ya kila shabiki wa Yanga.
Ametengeneza timu ambayo kila anayepewa nafasi ya kuanza kwenye mechi anatoa burudani stahiki kwa wananchi.
Amekuwa mwalimu mzuri wa nidhamu ndani ya Klabu ndiyo maana Saido Ntibanzonkiza alishindwa, Morison anapata shida.
Ni kocha mwenye misimamo yenye tija kwa timu yake ndiyo maana kuna wakati anawaweka bench akina Aziz Ki, Mayele, Moloko, Kisinda, Mwamnyeto na wengineo haijalishi mechi ni ngumu kiasi gani yeye anachojali ni anayecheza siku hiyo aendane na mahitaji ya mechi bhas!!
[emoji117]Robertinho wa Simba SC alijaribu hii kitu siku Moja baada ya mechi kumkataa Chama, weee[emoji38] walimwambia akirudia tena ajue Pasaka itamkuta kwao Brazil[emoji1787][emoji1787]
Hata mashabiki wa Yanga kuna kipindi maneno ya Wachambuzi yalianza kama kuwaingia hivi baadhi yao wakaanza kukosa imani na Nabi ila kwasasa amewafunga midomo, wote wanaimba wimbo mmoja tu (Nabi ni Professor)
Amewajenga kisaikolojia wachezaji wake kiasi cha kujiamini hata wakiwa nyuma kwenye mechi, timu ina fighting Spirit hawakati tamaa, hata ikitokea wamepoteza mechi hauona Yanga ikipoteana.
Mashabiki nao sasahivi Wana imani na Nabi wao, hata mechi ikiwa ngumu kwa upande wao utawaona wakiwa wametulia wakimsikilizia yeye kwasababu wanamuamini sana kwenye kufanya Sub na Mabadiliko ya mifumo ili timu ipate ushindi.
Pia nimpe hongera kwa kukuza na kulea hazina ya taifa pale jangwani, walahu tunaweza kusema kuwa amatuletea mrithi wa John Bocco kwenye kikosi cha taifa Stars.
Ni kocha gani angemuamini kinda kama Clement Mzize kwenye kikosi chenye Mayele, Musonda, Moloko, na Ki??
Huyu ndiye PROFESSOR NASREDDINE NABI Mwamba aliyewaziba midomo wambea wa mitandaoni, redioni, TV na vijiweni. Hawataki kumzungumzia tena kwasababu kwasasa hana doa wanajua kuwa wakimzungumzia watatakiwa kusema mazuri yake pekee kitu ambacho wabongo hatujajaliwa,
Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app