Professor Nabi aliyewafunga midomo wachambuzi uchwara!!

Professor Nabi aliyewafunga midomo wachambuzi uchwara!!

Song of Solomon

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2021
Posts
2,752
Reaction score
5,609
Mwamba huyu hapa!!

Kwa bahati mbaya anafanya Kazi kwenye nchi ambayo watu wanasubiri ukosee ndiyo wakuzodoe ila ukiwa unafanya mazuri wanafumba macho.

Kwanza ametengeneza timu isiyo na Super star, timu haimtegemei mchezaji mmoja haijalishi unalipwa kiasi gani, una jina kubwa, ulinunuliwa kwa bei gani, unatoka taifa gani.

Mwamba hana maneno wala mbwembwe nyingi bali ameamua kuongea kwa vitendo.

Kipindi anaanza kuanda timu, wengi walimkosoa wakisema timu yake inakata moto kipindi cha pili, wengine wakasema hana tactics za kucheza mechi za kimataifa, mara ooh timu nzima inamtegemea Feisal tu na asipofunga timu haifungi.

Pia kuna maneno mengi ya kejeli yalizungumzwa juu yake hasa na wachambuzi wanaojikuta wao ndiyo wataalam wa soka hapa bongo.

Mwamba Nasreddine Nabi hakuwahi kuwajibu bali alifocus kwenye mipango na malengo yake alijua kuwa akiwasikiliza watamtoa kwenye reli.

Kwa sasa yupo kwenye kilele cha mafanikio ndani ya Klabu ya Yanga, kwani amefanikiwa kuitengeneza timu ya ndoto ya kila shabiki wa Yanga.

Ametengeneza timu ambayo kila anayepewa nafasi ya kuanza kwenye mechi anatoa burudani stahiki kwa wananchi.

Amekuwa mwalimu mzuri wa nidhamu ndani ya Klabu ndiyo maana Saido Ntibanzonkiza alishindwa, Morison anapata shida.

Ni kocha mwenye misimamo yenye tija kwa timu yake ndiyo maana kuna wakati anawaweka bench akina Aziz Ki, Mayele, Moloko, Kisinda, Mwamnyeto na wengineo haijalishi mechi ni ngumu kiasi gani yeye anachojali ni anayecheza siku hiyo aendane na mahitaji ya mechi bhas!!

[emoji117]Robertinho wa Simba SC alijaribu hii kitu siku Moja baada ya mechi kumkataa Chama, weee[emoji38] walimwambia akirudia tena ajue Pasaka itamkuta kwao Brazil[emoji1787][emoji1787]

Hata mashabiki wa Yanga kuna kipindi maneno ya Wachambuzi yalianza kama kuwaingia hivi baadhi yao wakaanza kukosa imani na Nabi ila kwasasa amewafunga midomo, wote wanaimba wimbo mmoja tu (Nabi ni Professor)

Amewajenga kisaikolojia wachezaji wake kiasi cha kujiamini hata wakiwa nyuma kwenye mechi, timu ina fighting Spirit hawakati tamaa, hata ikitokea wamepoteza mechi hauona Yanga ikipoteana.

Mashabiki nao sasahivi Wana imani na Nabi wao, hata mechi ikiwa ngumu kwa upande wao utawaona wakiwa wametulia wakimsikilizia yeye kwasababu wanamuamini sana kwenye kufanya Sub na Mabadiliko ya mifumo ili timu ipate ushindi.

Pia nimpe hongera kwa kukuza na kulea hazina ya taifa pale jangwani, walahu tunaweza kusema kuwa amatuletea mrithi wa John Bocco kwenye kikosi cha taifa Stars.

Ni kocha gani angemuamini kinda kama Clement Mzize kwenye kikosi chenye Mayele, Musonda, Moloko, na Ki??

Huyu ndiye PROFESSOR NASREDDINE NABI Mwamba aliyewaziba midomo wambea wa mitandaoni, redioni, TV na vijiweni. Hawataki kumzungumzia tena kwasababu kwasasa hana doa wanajua kuwa wakimzungumzia watatakiwa kusema mazuri yake pekee kitu ambacho wabongo hatujajaliwa,


Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Umeharibu hapo ulipotafuta mlingano na Simba.Ukiamua kueleza/kumpa sifa mtu,ubanane naye huyohuyo.Halafu,mnatakiwa ku-focus kwenye mechi inayowasubiri.Kila timu,kocha au uongozi una namna yao ya ku-achieve malengo.
 
Umeharibu hapo ulipotafuta mlingano na Simba.Ukiamua kueleza/kumpa sifa mtu,ubanana naye huyohuyo.Halafu,mnatakiwa ku-focus kwenye mechi inayowasubiri.Kila timu,kocha au uongozi una namna yao ya ku-achieve malengo.
Kuna ubaya gani kuwataja Simba ambao ni rivals wetu?

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
NABI SIO PROFESSOR.

NAOMBA TAALUMA ZA WATU ZIHESHIMIWE.

KAMA HUTOJALI UNAWEZA KUBADILISHA HEADING NDIPO WAUNGWANA TUSOME BANDIKO LAKO.

#usipotoshe.

MTAIFAHAMU KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU.
yohana 8:32
Lugha!Hawaijui lugha au wanajipoteza.Kuna lugha mtu akiitwa "le profeseur" ni sawa na kumuita "mwalimu" tu.Na siyo profesa kama wanavyodhani.Waelimishwe.
 
Kitu ambacho watu hatujui ni kuwa waliokuwa wanamkataa nabi kipindi kile ni mashabiki wa simba na wachambuzi uchwara wenye mahaba na simba

Nabi atawafunga simba mpaka waseme kwanini zile billion 20 hazionekani zilipo mpaka leo??😀😀😀😀😀😀😀
 
Kitu ambacho watu hatujui ni kuwa waliokuwa wanamkataa nabi kipindi kile ni mashabiki wa simba na wachambuzi uchwara wenye mahaba na simba

Nabi atawafunga simba mpaka waseme kwanini zile billion 20 hazionekani zilipo mpaka leo??[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Rivals wa Simba ni Al-Ahly,Mamelodi,Horoya,Vipers na wengineo waliopo Klabu Bingwa.Ninyi mtakutana na Simba mtakayoipania kwenye NBC P League au ASFC.Viwango tofauti,nchi moja.
Wewe ni taahira ngoja nikuache mpuuzi sana wewe unataja timu zenye makombe ya champions league wakati wewe NGURUWE ubingwa wako ni kucheza robo final lete medals humu mlizovalishwa kwa kubeba Kombe mjinga wewe

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni taahira ngoja nikuache mpuuzi sana wewe unataja timu zenye makombe ya champions league wakati wewe NGURUWE ubingwa wako ni kucheza robo final lete medals humu mlizovalishwa kwa kubeba Kombe mjinga wewe

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Usitukane.Haikupi afya ya akili.Hautaki kuelezwa ukweli?Vipers wana kombe lipi?Au waliiba jagi lako la ulanzi wakakudanganya wana kombe?
 
Kina farhani walituponda sna kwenye radio zao nakumbuka tulivyocheza na ali hilal hapa dar tukapoteza jmaaa waliturarua mno tokea siku zile sijawasikiliza Tena cmg

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Mnapata wapi muda kuwasikiliza wachambua michele hao?

Juzi Yanga kaongozwa goli 1 na Geita, lipumbavu limoja liliropoka "Geita wameamua kuwaachia Yanga mpira wacheze wanavyotaka ila Geita wanataka point 3 tu" ilihali YANGA waliwazidi hata hao Geita shots on target.

Nilijuta sana kukaa kibanda umiza nikisubiria mpira kipindi cha half time, bora hata ningeenda kuzurura kidogo ndipo nirudi kuangalia kipindi cha pili.

Michambuzi uchwara inaonekana kabisa inashabikia upande gani?

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom