Professor Nabi aliyewafunga midomo wachambuzi uchwara!!

Professor Nabi aliyewafunga midomo wachambuzi uchwara!!

super star wa yanga ni mayele na aziz ki, hakuna timu duniani inayokuwa haina key players,lazima timu iwe nawachezaji inaowategemea....pale yanga ukimtoa mayele diarra job na bangala hakuna timu tena pale
Eti hakuna timu pale!!,,unaongea kama kichwa umekiacha ukweni kwako vile,Yanga hakuna superstar kuzidi mwingine pale unatoka moto unaingia moto mwingine..Timy yenu kumfanyia sub chama ni mpaka awe anatoka damu puani bila hivyo kocha akithubutu tu anakuta kashaandaliwa tiketi ya ndege...

Kama uliangalia mechi ya yanga na AS REAL BAMAKO utaona kabisa kipindi cha kwanza Aziz ki gemu ilimkataa kocha ikabidi ambadilishe aingie Aucho na akabadilisha mwenendo wa timu..Yanga hii ina uwezo wa kumuamini Clement Mzize hata katika mechi ngumu ya kusaka point muhimu nyie wapuuzi siku ile mnalazimisha chama acheze hata kama anaumwa halafu unakuja hapa kusema hamna timu pale shenziii
 
Mwamba huyu hapa!!

Kwa bahati mbaya anafanya Kazi kwenye nchi ambayo watu wanasubiri ukosee ndiyo wakuzodoe ila ukiwa unafanya mazuri wanafumba macho.

Kwanza ametengeneza timu isiyo na Super star, timu haimtegemei mchezaji mmoja haijalishi unalipwa kiasi gani, una jina kubwa, ulinunuliwa kwa bei gani, unatoka taifa gani.

Mwamba hana maneno wala mbwembwe nyingi bali ameamua kuongea kwa vitendo.

Kipindi anaanza kuanda timu, wengi walimkosoa wakisema timu yake inakata moto kipindi cha pili, wengine wakasema hana tactics za kucheza mechi za kimataifa, mara ooh timu nzima inamtegemea Feisal tu na asipofunga timu haifungi.

Pia kuna maneno mengi ya kejeli yalizungumzwa juu yake hasa na wachambuzi wanaojikuta wao ndiyo wataalam wa soka hapa bongo.

Mwamba Nasreddine Nabi hakuwahi kuwajibu bali alifocus kwenye mipango na malengo yake alijua kuwa akiwasikiliza watamtoa kwenye reli.

Kwa sasa yupo kwenye kilele cha mafanikio ndani ya Klabu ya Yanga, kwani amefanikiwa kuitengeneza timu ya ndoto ya kila shabiki wa Yanga.

Ametengeneza timu ambayo kila anayepewa nafasi ya kuanza kwenye mechi anatoa burudani stahiki kwa wananchi.

Amekuwa mwalimu mzuri wa nidhamu ndani ya Klabu ndiyo maana Saido Ntibanzonkiza alishindwa, Morison anapata shida.

Ni kocha mwenye misimamo yenye tija kwa timu yake ndiyo maana kuna wakati anawaweka bench akina Aziz Ki, Mayele, Moloko, Kisinda, Mwamnyeto na wengineo haijalishi mechi ni ngumu kiasi gani yeye anachojali ni anayecheza siku hiyo aendane na mahitaji ya mechi bhas!!

[emoji117]Robertinho wa Simba SC alijaribu hii kitu siku Moja baada ya mechi kumkataa Chama, weee[emoji38] walimwambia akirudia tena ajue Pasaka itamkuta kwao Brazil[emoji1787][emoji1787]

Hata mashabiki wa Yanga kuna kipindi maneno ya Wachambuzi yalianza kama kuwaingia hivi baadhi yao wakaanza kukosa imani na Nabi ila kwasasa amewafunga midomo, wote wanaimba wimbo mmoja tu (Nabi ni Professor)

Amewajenga kisaikolojia wachezaji wake kiasi cha kujiamini hata wakiwa nyuma kwenye mechi, timu ina fighting Spirit hawakati tamaa, hata ikitokea wamepoteza mechi hauona Yanga ikipoteana.

Mashabiki nao sasahivi Wana imani na Nabi wao, hata mechi ikiwa ngumu kwa upande wao utawaona wakiwa wametulia wakimsikilizia yeye kwasababu wanamuamini sana kwenye kufanya Sub na Mabadiliko ya mifumo ili timu ipate ushindi.

Pia nimpe hongera kwa kukuza na kulea hazina ya taifa pale jangwani, walahu tunaweza kusema kuwa amatuletea mrithi wa John Bocco kwenye kikosi cha taifa Stars.

Ni kocha gani angemuamini kinda kama Clement Mzize kwenye kikosi chenye Mayele, Musonda, Moloko, na Ki??

Huyu ndiye PROFESSOR NASREDDINE NABI Mwamba aliyewaziba midomo wambea wa mitandaoni, redioni, TV na vijiweni. Hawataki kumzungumzia tena kwasababu kwasasa hana doa wanajua kuwa wakimzungumzia watatakiwa kusema mazuri yake pekee kitu ambacho wabongo hatujajaliwa,


Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Tusimsahau Kaze na ana mchango mkubwa
 
NABI SIO PROFESSOR.

NAOMBA TAALUMA ZA WATU ZIHESHIMIWE.

KAMA HUTOJALI UNAWEZA KUBADILISHA HEADING NDIPO WAUNGWANA TUSOME BANDIKO LAKO.

#usipotoshe.

MTAIFAHAMU KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU.
yohana 8:32
Kulikuwa na profesa Maji marefu mganga na aliekuwa mbunge nae vipi tumlalamikie alitumia vibaya uprofesa?
 
Kwahiyo simba inafanana na al ahly kwa akili yako?
Unaelewa maana ya kufanana kwanza?Wapo katika kombe moja la mabingwa na wanacheza robo fainali.Katika kumi bora Afrika wapo wote.Simba hayupo kundi moja na walio nafasi ya "78+"!Wengi wanaoanzia natasi ya 25 wapo losers cup!
 
Diarra - Metacha
Job - Bacca
Bangala - Mudathir

Sema kingine kolo
Kwa metacha hapo Hamna kitu.
Ukwel usemwe tu Kila timu Ina key players .
Hapo yanga ni mayele na bangala.
Siku wasipocheza hao lazima uone pengo la waz.
Kuna gemu ya shiriisho hao watu walikua nje na mchezo ulikua unaelekea kuwa mgumu ,ikambid kocha aingize mayele ,bangala na wengine hapo mvua ya mgoli ikatokea.

Sema kwavile ushabiki unatuendesha sna basi hatuna budi kukubaliana na akili yenu inavyotaka.
Sisi ni Nan had tuwapinge ,japo ukwel ndio huo.
 
Sasa mpaka litapopatikana wewe utaendelea kuwa loser
At the time being wewe unanizidi Mimi labda ni hayo makombe Yako ya robo na nusu tu
Tumia neno loser vizuri.Ngoja nikukumbushe:Timu zile chovu baada ya kung'olewa Kombe la Mabingwa/klabu Afrika huwa wanatupwa Kombe la Shirikisho(wanashirikiana kulia,kusononeka na kuliwazana pamoja).Nadhani unanielewa.Tumia neno loser mahali na kwa timu stahiki.
 
Kwa metacha hapo Hamna kitu.
Ukwel usemwe tu Kila timu Ina key players .
Hapo yanga ni mayele na bangala.
Siku wasipocheza hao lazima uone pengo la waz.
Kuna gemu ya shiriisho hao watu walikua nje na mchezo ulikua unaelekea kuwa mgumu ,ikambid kocha aingize mayele ,bangala na wengine hapo mvua ya mgoli ikatokea.

Sema kwavile ushabiki unatuendesha sna basi hatuna budi kukubaliana na akili yenu inavyotaka.
Sisi ni Nan had tuwapinge ,japo ukwel ndio huo.
Mlisemaga akitoka feitoto timu haipati matokeo.
 
Asante Kwa masahihisho
Ila una kombe lolote huko CL!?
Acha kuruka ruka ,aliyesema shirikisho ni kombe la looser ni albino wenu na mkamuunga mkono kisa tu yanga haikuwa kwenye mashindano hayo.
Mngekua na akili kipindi anatamka haya mngemkemea kuwa hilo sio kombe la looser bali ni kombe halal na Lina heshima yake.
Akili za uto mnajijua wenyew ,Leo mtapinga hili kesho mtahangaika kulitetea Kwa nguvu zote.
 
Kuna sehemu nimeitaja timu ili ujilinganishe nayo?Nadhani umeelewa maana ya loser kama litumikavyo katika makombe hayo mawili.Ukiendelea mbele ntakueleza hadi "underdog" ni nani hadi sasa.Say amen!
Umedai shirikisho ni mashindano ya waliong'olewa ligi ya mabingwa ndio nikakuuliza pyramid aling'olewa nae? Umeanza kushabikia mpira mwaka gani?
 
Back
Top Bottom