Professor Nabi aliyewafunga midomo wachambuzi uchwara!!

Professor Nabi aliyewafunga midomo wachambuzi uchwara!!

Sahihi.Sifa zipo.Timu legelege itolewayo mabingwa(walioonekana unfit kuendelea)mwanzomwanzo hutupiliwa mbali kule losers cup.Ila wale watakaoonesha ukakamavu hadi kiwango fulani,hupewa kifuta jasho na kuendelea na mambo mengine.Ndiyo sifa ya loser.
Loser kama pyramid
 
Ndio maana nikakuambia ukiyapinga makatazo ya Allah tunasema hauna akili hapo juu umeandika "madrasa haukufundishwa? " sasa je wewe una uhakika gani ?
Mambo ya madrasa uliyaleta wewe.Sasa,jikite kuhusu losers cup.Tuachane na madrasa.Mimi sikupata utaalamu huo.
 
Ukitaka kujua Nabi mtu badi mpaka sasa kwenye makundi timu imetumia mifumo mitatu, kule Tunisia,plus Mazembe na Bamako ilitumika mifumo miwili tofauti.

Ila jana ndio kaonyesha yy ni wa kipeekee ,Sure boy kacheza dimba la chini Bangala na Aucho wakacheza juu.
 
Loser kama pyramid
Suala la Pyramids nadhani tulijifunza wote jinsi walivyoingia kwenye ushindani wa kombe katika somo la kwanza.Tulipenda zaidi kujua hawa "losers" hupatikanaje na hushiriki kombe gani kwa u-losers wao/unfitnesses wao!
 
Mwamba huyu hapa!!

Kwa bahati mbaya anafanya Kazi kwenye nchi ambayo watu wanasubiri ukosee ndiyo wakuzodoe ila ukiwa unafanya mazuri wanafumba macho.

Kwanza ametengeneza timu isiyo na Super star, timu haimtegemei mchezaji mmoja haijalishi unalipwa kiasi gani, una jina kubwa, ulinunuliwa kwa bei gani, unatoka taifa gani.

Mwamba hana maneno wala mbwembwe nyingi bali ameamua kuongea kwa vitendo.

Kipindi anaanza kuanda timu, wengi walimkosoa wakisema timu yake inakata moto kipindi cha pili, wengine wakasema hana tactics za kucheza mechi za kimataifa, mara ooh timu nzima inamtegemea Feisal tu na asipofunga timu haifungi.

Pia kuna maneno mengi ya kejeli yalizungumzwa juu yake hasa na wachambuzi wanaojikuta wao ndiyo wataalam wa soka hapa bongo.

Mwamba Nasreddine Nabi hakuwahi kuwajibu bali alifocus kwenye mipango na malengo yake alijua kuwa akiwasikiliza watamtoa kwenye reli.

Kwa sasa yupo kwenye kilele cha mafanikio ndani ya Klabu ya Yanga, kwani amefanikiwa kuitengeneza timu ya ndoto ya kila shabiki wa Yanga.

Ametengeneza timu ambayo kila anayepewa nafasi ya kuanza kwenye mechi anatoa burudani stahiki kwa wananchi.

Amekuwa mwalimu mzuri wa nidhamu ndani ya Klabu ndiyo maana Saido Ntibanzonkiza alishindwa, Morison anapata shida.

Ni kocha mwenye misimamo yenye tija kwa timu yake ndiyo maana kuna wakati anawaweka bench akina Aziz Ki, Mayele, Moloko, Kisinda, Mwamnyeto na wengineo haijalishi mechi ni ngumu kiasi gani yeye anachojali ni anayecheza siku hiyo aendane na mahitaji ya mechi bhas!!

[emoji117]Robertinho wa Simba SC alijaribu hii kitu siku Moja baada ya mechi kumkataa Chama, weee[emoji38] walimwambia akirudia tena ajue Pasaka itamkuta kwao Brazil[emoji1787][emoji1787]

Hata mashabiki wa Yanga kuna kipindi maneno ya Wachambuzi yalianza kama kuwaingia hivi baadhi yao wakaanza kukosa imani na Nabi ila kwasasa amewafunga midomo, wote wanaimba wimbo mmoja tu (Nabi ni Professor)

Amewajenga kisaikolojia wachezaji wake kiasi cha kujiamini hata wakiwa nyuma kwenye mechi, timu ina fighting Spirit hawakati tamaa, hata ikitokea wamepoteza mechi hauona Yanga ikipoteana.

Mashabiki nao sasahivi Wana imani na Nabi wao, hata mechi ikiwa ngumu kwa upande wao utawaona wakiwa wametulia wakimsikilizia yeye kwasababu wanamuamini sana kwenye kufanya Sub na Mabadiliko ya mifumo ili timu ipate ushindi.

Pia nimpe hongera kwa kukuza na kulea hazina ya taifa pale jangwani, walahu tunaweza kusema kuwa amatuletea mrithi wa John Bocco kwenye kikosi cha taifa Stars.

Ni kocha gani angemuamini kinda kama Clement Mzize kwenye kikosi chenye Mayele, Musonda, Moloko, na Ki??

Huyu ndiye PROFESSOR NASREDDINE NABI Mwamba aliyewaziba midomo wambea wa mitandaoni, redioni, TV na vijiweni. Hawataki kumzungumzia tena kwasababu kwasasa hana doa wanajua kuwa wakimzungumzia watatakiwa kusema mazuri yake pekee kitu ambacho wabongo hatujajaliwa,


Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
Umeua ndugu
 
NABI SIO PROFESSOR.

NAOMBA TAALUMA ZA WATU ZIHESHIMIWE.

KAMA HUTOJALI UNAWEZA KUBADILISHA HEADING NDIPO WAUNGWANA TUSOME BANDIKO LAKO.

#usipotoshe.

MTAIFAHAMU KWELI NAYO KWELI ITAWAWEKA HURU.
yohana 8:32
Usiniambie mpaka leo hufahamu kama kuna vyeo watu wanapewa kutokana na tu mambo makubwa wanayofanya kwenye jamii iliyo wazunguka!

Na kama hutaki Nabi kuitwa Profesa, basi ukatae pia Joseph Haule kuitwa Profesa J, Steven Ngonyani (RIP) kuitwa Profesa Maji Marefu, nk.
 
Kumbe kucheza ligi moja ni kua rivals?
Inategemea unalielewaje neno rivals na unalisoma kutoka wapi.Kinachokutesa ni kidogo sana kwa kadiri CAF walivyoeleza.Wanacheza/shindana kombe moja u-rivals utakosekanaje?Simba wasubiriwe wakirudi kwenye ASFC ndiyo mjipange kuwaita rivals wenu.Kwa kombe la mabingwa?Hell nooo!
 
Usiniambie mpaka leo hufahamu kama kuna vyeo watu wanapewa kutokana na tu mambo makubwa wanayofanya kwenye jamii iliyo wazunguka!

Na kama hutaki Nabi kuitwa Profesa, basi ukatae pia Joseph Haule kuitwa Profesa J, Steven Ngonyani (RIP) kuitwa Profesa Maji Marefu, nk.
Kama ni kwa muktadha huo,ni sawa.Siongezi neno.
 
Eti hakuna timu pale!!,,unaongea kama kichwa umekiacha ukweni kwako vile,Yanga hakuna superstar kuzidi mwingine pale unatoka moto unaingia moto mwingine..Timy yenu kumfanyia sub chama ni mpaka awe anatoka damu puani bila hivyo kocha akithubutu tu anakuta kashaandaliwa tiketi ya ndege...

Kama uliangalia mechi ya yanga na AS REAL BAMAKO utaona kabisa kipindi cha kwanza Aziz ki gemu ilimkataa kocha ikabidi ambadilishe aingie Aucho na akabadilisha mwenendo wa timu..Yanga hii ina uwezo wa kumuamini Clement Mzize hata katika mechi ngumu ya kusaka point muhimu nyie wapuuzi siku ile mnalazimisha chama acheze hata kama anaumwa halafu unakuja hapa kusema hamna timu pale shenziii
Saa hii na wameongeza na Kanoute Hawa trh 16 April watatafutana sana maana naona kama Nabi ameanza kuwachanganya hata hawajui wamroge nani maana Job yuko nje na Bacca anakichafua
Musonda ndio kama hivyo gari imewaka Shabalala hana amani kabisa
Najua watajivunja kwa Ihefu ili kukwepa kikombe kile Cha Kirumba ila kwenye ligi lazima tukutane ziwe point 11
 
Saa hii na wameongeza na Kanoute Hawa trh 16 April watatafutana sana maana naona kama Nabi ameanza kuwachanganya hata hawajui wamroge nani maana Job yuko nje na Bacca anakichafua
Musonda ndio kama hivyo gari imewaka Shabalala hana amani kabisa
Najua watajivunja kwa Ihefu ili kukwepa kikombe kile Cha Kirumba ila kwenye ligi lazima tukutane ziwe point 11
Ila,kwa akili hizi za kusubiri kuifunga Simba huwa mnaonesha kufeli sana.Hamkui?Zile lugha za..."mimi bila kumfunga mtani sioni raha'...,jaribuni kuzipunguza.Think big,boys!Kujeni na "mamikakati kabambee" ya kusonga mbele kimataifa.Msiangalie pua zenu zinapoishia.
 
Ila,kwa akili hizi za kusubiri kuifunga Simba huwa mnaonesha kufeli sana.Hamkui?Zile lugha za..."mimi bila kumfunga mtani sioni raha'...,jaribuni kuzipunguza.Think big,boys!Kujeni na "mamikakati kabambee" ya kusonga mbele kimataifa.Msiangalie pua zenu zinapoishia.
Unaweza kuwa bingwa bila kumfunga simba?
 
Back
Top Bottom