Kuweka hizi kampuni kwenye hizi nchi inamaanisha they're good in technology than us
Uwekezaji wa Microsoft au Meta kufungua ofisi za kikanda Kenya hauhusiani moja kwa moja na utofauti wa bidhaa zao kati ya Kenya na Tanzania. Hizi ni ofisi za usimamizi wa kanda, si vituo vya kuzalisha bidhaa tofauti kwa kila nchi.
Sababu kubwa ya kampuni kama hizi kuchagua eneo fulani ni mazingira ya kibiashara na kiteknolojia—yaani, miundombinu ya IT ipo vizr, sera za serikali, upatikanaji wa wataalamu wa teknolojia(software developers), na mazingira ya ushindani wa kibiashara. Kenya imefanikiwa kujijenga kama kitovu cha tech Afrika Mashariki kwa sababu ya juhudi za serikali, uwekezaji wa sekta binafsi, na ushawishi wa diaspora yao. Tanzania, kwa upande mwingine, bado ina nafasi ya kuboresha utangazaji wake kama kituo cha kiteknolojia na kuvutia zaidi wawekezaji wakubwa japo tunakubali Kenya imetushinda.
Huwezi kuona kampuni kubwa ikiwekeza mahali ambapo hakuna mazingira mazuri ya ukuaji wa biashara zao. Ni kama mkulima anavyotafuta ardhi yenye rutuba kabla ya kuanza kilimo—mavuno yanaendana na mazingira.