KERO Programu ya Mwendokasi haipatikani kwenye App Store na upatikaji wa kadi bado ni shida

KERO Programu ya Mwendokasi haipatikani kwenye App Store na upatikaji wa kadi bado ni shida

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Abiria wa Mwendokasi ni wengi, lakini upatikanaji wa kadi za usafiri ni changamoto. Hali hii inalazimu baadhi ya abiria kusubiri mtu mwenye kadi na kumuomba awasaidie kuweka fedha ili waweze kutumia huduma.

Pia, watumiaji wa iPhone wanakabiliwa na changamoto ya kutopatikana kwa programu ya Mwendokasi kwenye App Store. Wanapoitafuta kwa ajili ya kuipakua, haionekani.

Tunaomba mamlaka husika kuangalia changamoto hizi na kuboresha huduma ili kurahisisha usafiri kwa abiria.

IMG_2345.png
 
Back
Top Bottom