Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
- Thread starter
-
- #21
Rev. Kishoka,
Nimesoma mahala akisema chama chake kina mrengo wa kati, ndio upi huo (wa kati kulia au kushoto)... Au ndio nawe unaanzisha mapinduzi mapya ya kifikra kuunda mrengo wa KATI yaani usiofungamana na upande wowote ila kwa kuzingatia Mazingira na watu wake!
FMES.
Bagamoyo yetu ni vijijini kwa Watanzania, ni mitaani huko mijini. Uhalali na Uimara wetu hautatokana na kumeza maganda ya mayai ya mjusi au kubandika ****** yetu kwenye kuta za ofisi!
Sisi tutatengenezwa kwa ridhaa ya wananchi. Tutawahubiria Wananchi na kuwaonyesha kwa vitendo tunachotaka kufanya kifanyike kwa manufaa yao na kuwashirikisha katika mchakato mzima na wao waamue kama wanatuamini na kutupa ridhaa na dhamana ya kuwaongoza au la.
Kwenda bagamoyo ni sawa na kucheza upatu, mwenzko naye huenda Bagamoyo na kama yeye ataamini kupanda mnazi kinumenyume kichwa chini miguu juu ili wananchi wampende na kumpa kura, hiyo ni shauri yake.
Katika mfumo wa haki na utu, dhamana hutoka kwa watu na si Milingotini kwa Ajuza fulani au Kibabu fulani kinachokusanya ngozi za Mazeruzeru!
Wakuu si tayari kuna chama kinaitwa PPT-Maendeleo? Kama nime kosea nisahihishwe wakuu.
Wakuu si tayari kuna chama kinaitwa PPT-Maendeleo? Kama nime kosea nisahihishwe wakuu.
Well, I can care less what they are called, if no Progressive People's Party of Tanzania, then I am free to use the name. In addition, do they have same principles that I am advocating to Tanzanians?
Jina zuri la chama liwe kwa kiswahili,huo ndo ushauri wangu.
tanzania ina chama cha mapinduzi na chama cha maendeleo na demokrasia (chadema) yote ni ya kiswahili na vinajiendesha kiswahili swahili (samahani kwa zitto, dr. Slaa na mnyika marafiki zangu!)
Duuuh..... wewe Rev. inaonekana ulitoroka na chupa yenye mazazo ya mvinyo jumapili iliyopita wewe!!!! LoL
Kumbe tunapowaona wamekaa kimya tu bila maamuzi yoyote wakati mabomu ya Mbagala yanalipuka inabidi tuwaonee huruma.... maana huchelewi kuta makoo yalikuwa yameziba kwa maganda ya mayai ya mijusi weupe!!!
Tanzania ina Chama cha Mapinduzi na Chama cha Maendeleo na Demokrasia (Chadema) yote ni ya kiswahili na vinajiendesha kiswahili swahili (samahani kwa Zitto, Dr. Slaa na Mnyika marafiki zangu!)
Rev., tayari umeshapata mwanachama hapa! Nitajiunga nawe...
Naomba kuwa mmoja wa ma-strategists wako.
ngosha,
kutumikia umma na utumishi wa jamii ni kujitolea, alimradi kuna maelewano katika timu na kuna msimamo ambo uko wazi na kila mtu anakuwa na nafasi sawa.
Karibu sana kwenye timu, hivyo wewe kadi yako ni nambari 1.
jina linaloeleweka na mass ni advantage...
Lakini tusifanye Utani wakuu zangu hii ya Rev kweli imekaa sawa?
Kwa nini mkuu wangu usijiunge na chama fulani kisha toka humo ukakua kisiasa kabla hutafikia maamuzi kama haya. Kuanzisha chama kipya inachukua nguvu kubwa sana tena fedha nyingi sana unaweza kufilisika kabisaaa kuwavuta maskini wenye njaa.
Rev.
Ok mkuu wangu unaweza nambia tofauti inayowatenganisha mrengo wa TTTP na mirengo mingine (kushoto na Kulia) hasa inapokuja ktk maswala ya jamii..what are the Values, Athics kwani wataalam husema:- In civilized life, law floats in a sea of ethics. Each is indispensable to civilization. Without law, we should be at the mercy of the least scrupulous; without ethics, law could not exist.
Kwa hiyo ni lazima ukanyage nyayo za watu hapa..
Una tafsiri vipi Uzawa, Ushoga, maswala ya ndoa, mirathi, haki za kuabudu..Ni kwa kiwango kipi kwa sababu hadi leo huwa nashindwa sana na ile haki ya watu kuabudu dini waitakayo..mathlan, Je naweza kuabudu dini ya kiasili inayo lenga imani ya mizimu na Uchawi!
Eeeeh banaa wee tayari umeshajiunga mara!... haya na Mzee Mwanakijiji yumo au?Umeuliza swali la msingi sana. Hata hivyo naomba uwe na subira kidogo, ni mengi kuelezea na ni mengi tunajiandaa nayo. Swali lako linajibika, ila ni vyema kama litajibiwa kirefu ili kuondoa mwanya wa kutokuelewa. Mwenyekiti bado anajibu maswali ya wadau wengine mbalimbali waliotangulia kuuliza. Ahsante.
wewe ya kwako no ngapi?
Wewe ndio no 1,halafu huyo unampa no 2,and so and so.
Au wewe huwi member wa chama chako?