Progressive People's Party of Tanzania

Halafu masuala ya majimbo nyinyi mnasemaje?
Mahakama ya kadhi??
Sera yenu ya ardhi na mikataba ya madini ipo vipi?
 
Eeeeh banaa wee tayari umeshajiunga mara!... haya na Mzee Mwanakijiji yumo au?

Bado anapata ushauri kutoka kwa Makamba. Akikamilisha tu ajenda yake na CCM natumaini atakuwa na matamanio ya kujiunga nasi. Vipi wewe... kwanini usijiunge nasi bob?!
 
Siasa siziwezi mkuu.. mimi domo kaya tu, ni mmoja wa Watanzania waumini tunaosubiri Nabii!
 
Halafu masuala ya majimbo nyinyi mnasemaje?
Mahakama ya kadhi??
Sera yenu ya ardhi na mikataba ya madini ipo vipi?

Tutafafanua na kuelezea sera zetu kadiri tunavyo nakshanaksha na kukamilisha hatua za usajili. Mengi yaliyo kwenye misimamo yetu hayatofautiana na mengi yenye msingi wa kutumikia Tanzania na kwa manufaa ya Watananzania mliyoyasoma hapa jamvini. Maswali ya sera tungelipenda kuyajibu kwa kirefu ili kupunguza ambiguity maana ni maswala nyeti.
 

Mkandara,

Tanzania ya sasa si ya mwaka 1960, 1070 au 1990.

Mimi nilikuwa nikiwasikiliza kina Bembeya Jazz, Sosoliso, Nuta, Atomic, Juwata, OSS, New Edition, Elton John, Burning Spear na Dennis Brown.

Leo hii kuna Ali Kiba, Lady Jaydee, Sean Kingston, Rhihanna, TPain na Coldplay.

Mimi nilikuwa kuchezea manati, chandimu, matairi ya magari, kombolela, kuchunga mbuzi, kufyeka nyasi na kadhalika. Barua tulikuwa tunatumia karatasi za kawaida na bahasha kama si zile airform za buluu. Leo hii wanatumi Wii, PS3, simu za mkononi, email na facebook.

Hivyo, kuna mambo ambayo yamebadilika na ni lazima yashirikishwe si kwa ajili ya kukidhi matakwa ya watu, bali ni kukiri na kukubali kuwa dunia imebadilika.

Lakini msingi mkuu ni Sheria, Kanuni na Katiba. Je zinasemaje? je ni kwa ajili ya ridhaa ya Wananchi ili kuwe na haki na mazingira salama yenye kuduumisha utu?

Leo naweza kusema eti Ushoga ni marufuku, lakini Uhujumu unafanyika bila tatizo na Serikali ikalie kooni mashoga na was enge, lakini wanaoliibia Taifa wanapeta na sheria zinawapa baraka na kutoa mianya. Je tutaeleweka?

Kila aliye Raia wa Tanzania atakuwa na haki sawa na atatumikiwa na PPPT. Wale ambao ni wageni, nao watakuwa na haki sawa za kimsingi kama chakula, nyumba, afya, elimu na kufuatia tamko la Umoja wa Mataifa.

Tofauti itakuwa ni katika utambuzi wa kisheria ambao utamlinda Mzawa katika masuala ambayo ni kwa ajili ya Usalama na Ustawi wa Taifa, na kwa wageni wawe wameweza kufikia na kupita vipengele na viwango maalum vilivyowekwa.

Kama unaongelea kwa mantiki ya Machinga wa Kichina kuwa na nafasi sawa na Machinga wa kutoka Handeni, hapo hapatakuwa na ruhusa kwa mgeni mkazi kuja kujifanyia kila anachotaka bila kuwa na masharti kadhaa ya kihamiaji na kwa mujibu wa sheria za kazi ambazo zitamruhusu Mgeni Mkazi akafanye shughuli zake.
 


Steve D,

Nashukuru kwa kumjibu Bwana Mkubwa ambaye naona ana munkari kutaka kujua masuala kadhaa ambayo ni kero za wananchi bila kupitia upya nilichokisema kuwa PPPT ni kwa ajili ya Watanzania na kitafanya kazi kwa ridhaa ya Watanzania na kwa manufaa ya Watanzania bila kujali upande gani wa muungano wanakotoka, dini, jinsia, umri, elimu au lolote lile.

Kama Bwana Mkubwa akichukua muda akarudia kusoma tunayoyasema hapa, ataelewa na kupata majibu tosha kwa maswali yake.
 

Naona kama ujio wa Nabii Moses aliyetumwa na Mungu kuja kuwaodoa wana wa Israel jangwani umefika, tumeteseka sana Rev tupeleke kwenye nchi ya asali na maziwa, tushirikiane kuondoa shule zisizo na madawati, kuondoa hospitali zisizo na drip, tumiliki rasilimali zetu, tujue haki zetu za msingi za kiraia na za kikatiba. Twakusubiri tuondoke nchi ya Farao.
 
Rev. Kishoka,
Mkuu nitakuomba maelezo zaidi kuhusiana na vitu hivyo kwani umechukua case ambayo ni rahisi sana, pasipo kuelezea tatizo moja kwa sheria yake..Sidhani kama vyama vingine vinaukubali Ufisadi, hata hiyo CCM yenyewe isipokuwa ni viongozi wake wanaopindisha sheria. Kwa mfano Rostam anaweza jiunga na chama chako akijua uharamu wa Ufisadi lakini kutokana na nguvu ya shetani (fedha) tukarudi kule kule.

Mimi sina upinzani na mashoga ila ni ktk kufahamu msimamo wa chama chako tunapozungumzia Watu na Mazingira. Najaribu kuona upo karibu sana na upande gani pamoja na kwamba wananchi hawana elimu juu ya mrengo..Ningependa sana ukianzia hapo kiasi kwamba wananchi wapate kuuliza maswali haya haya vyama vingine ili tuweze kuziona tofauti za kiitikadi baina ya vyama. Hapo ndipo tutaanza kupiga kura kwa kutazama wapi tunapelekwa kuliko kuchagua dereva..
Ndio mwanzo wa kuelewa kitu kwani hata mimi napotaka kwenda mwanza huanza kuchagua kampuni ya Bus ambayo naelewa vizuri ratiba yao, kisha ndio dereva ni nani hufuata.
 

Mkandara sioni utani hata kidogo hii manifesto ni tight, big shout kwa reverend, hata nabii musa aliposema anawatoa wana wa israel jangwa wanyewe hawakuamini na sisi vivyo hivyo, tuamini hii ili tuende kwenye nchi ya amani, nchi tuliyoahidiwa nchi yamaziwa na usali.
 

Do it,, pholosophise and think it wisely, tunafunga mizigo hivi tulipo safari ianza, ndugu yangu sipo where are join the bandwagon, banda la babu yako lile ndio mwanzo wa kuondoka, neema kwa bibi inakuja.
 
jina linaloeleweka na mass ni advantage...

Jina sio tatizo, watu wako result oriented, wanataka mabadiliko kwenda kwenye nchi ya ahadi. Kwao jina halitatui matatizo yao hata kidogo, ila matatizo ni mtazamo na malengo ya kweli ya chama. Mbona wananchi hao hao wanatamka majina magumu ya dawa eg klorofeniko ni kwa sababu dawa hio inawasaidia, hawataweza kusahau PPPT, kitu kinachokusaidia sawa na chama hicho wananchi hawawezi kusahau.
 

tunnasuburi manifesto hiyo kwa hamu
 

umevuka kihunzi cha kwanza, seems you are not selfish, to tou what matters is the right people fighting a genuine cause. Thanks rev. Mimi sihitaji kuona fimbo inageuka nyoka, nafunga mizigo kujitayarisha na safari kwenda kwenye kwenye nchi ya ahadi
 

Mkuu wangu kwanza mnabidi mfikirie Watanzania walio wengi.. Huyo mama yangu mkulima nikimwambia Progressive People's Party of Tanzania, atauliza eeeh ndio nini hiyo Pogolesivu!..kaazi mpya!
Wakuu wapo wengi sana, jaribuni pia kutumia jina la kiswahili amini maneno yangu mna deal na Wadanganyika!
 
Siasa siziwezi mkuu.. mimi domo kaya tu, ni mmoja wa Watanzania waumini tunaosubiri Nabii!

Ndo huyu ameletwa kutupeleka kwenye nchi ya ahadi, lakini makandara, domo kaya nayo ni sehemu ya siasa
 
Ndo huyu ameletwa kutupeleka kwenye nchi ya ahadi, lakini makandara, domo kaya nayo ni sehemu ya siasa
Hapana mkuu wangu nitakwambia kitu kimoja, huko kwetu ukiwa unatembea usiku wa manane basi unajifanya kuimba kwa sauti kubwa ili mradi kuondoa woga..Kma mlevi vile, lakini ukiona Unyasi tu kutikisika unatoka timu ukifikiria nyoka..
Ndio mimi navyoziogopa Siasa za Bongo!
 

Huo ndio ushujaa anayetembea usiku ni mwamba kwani wakati huo wengi wamelala. Kuimba sio tija ones presence must be felt and in other tribes inasaidia kufukuza vinyemelezi kwenye mji wako.Kushtuka mtu akiona ujani goes to the principle that do not trust anyone. Basing on the above therefore kelele zako zina maana sana sio za bure wala sio za woga.
 
Sidhani kama Tanzania inahitaji vyama .......nafikiri tatizo ni nani wanaongoza vyama.
 

kama jina ni refu basi kifupi chake PIPIPI TI, PIPIPITI au PIPI PITI, hakuna mtanzania atayeshindwa mbona wanatamka majina ya ajabu tu ya wajukuu wao, ( ashley, precious, joylyn,xenia ) wanaowaona mara moja kwa miaka mitatu na hawasahau sembuse chama ambacho kitawaleltea maendeleo ya kweli na watakuwa nacho 24/7???.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…