Kishoka,
Mie wasiwasi wangu ni hapo kwenye maneno "chama changu". Kama kweli kutakuwa na Demokrasia, hivi akaja mtu mwengine mwenye nguvu zaidi ya kushawishi wapiga kura na kutaka kukiteka CHAMA CHAKO kama ambavyo Zitto alitaka kukiteka CHAMA CHA MTEI/Mbowe (CCM?) utakuwa tayari ku-step down na kusubiri kama jamaa ataboronga, basi wanachama wakurudishe tena kwa njia ya demokrasia au uwekwe pembeni milele na ukumbukwe tu kama mtu aliyeleta demokrasia ya kweli Tanzania?
Mie wasiwasi wangu siku zote ni hapo tu. Na miiko gani ya viongozi kama chama mtajiwekea 'in advance'. Hii miko ndiyo itakuwa kama mwanga wa nini kitatokea kama mtashinda uchaguzi. Mtu kama ni FISADI basi mapema kabisa ataambiwa achagua kuwe kiongozi au arudi akaendelee na kuganga njaa/kufanya biashara zake. Wadhamini wote lazima waandikwe na wawekwe wazi na chama kisikubali kupokea hela kubwa kubwa maana nidyo kujitundika kitanzi. Heri kupokea tuseme max. 10 mlns Tsh.
Mwisho kama nilivyosema hapo zamani, chama hiki kiwe chama cha kwanza kufanya mikutano yake hadi ONLINE ili hata wale Watanzania waliokwama kufika kwenye kikao, waweze kuhudhuria hata kama kwa siku hiyo watakuwa kwenye kuvua samaki bwawa la Igombe.
Kama hayo juu, hasa lile la kwanza na MIIKO ya viongozi likiwa limeandikwa na kuwekwa wazi, basi Mchungaji, mie ni MWANACHAMA.
Sikonge,
Niliposema chama Changu hakina mana kuwa nakimiliki au ni changu pekee. Ni changu kwa maana ya mapenzi yangu, sawa na vile Yanga yangu na Nyerere Wangu.
Nilipoandika hapo nilikuwa pekee, wamejiunga Steve D, Omutwale, Fair Player, hata Kasheshe anaegemea kujitolea na Mkandara anania thabiti kujiunga.
Sasa ukisoma majibu yangu ya baadaye, ndio maana nikasema Steve D atapewa kadi Nambari Wani, na mimi ya kwangu itakuwa nambari elfu moja. Aidha nimeainisha kwa kutamka chama chetu huko mbele.
Kuhusu maadili au ni nani awe mwanachama, tutaangalia kwa undani kuwa ni mtu wa namna gani anayekuja jiunga na chama chetu.
Badala ya kukurupuka kutoa kadi na kujitangaza eti tumepata kadi 20 kutoka CHADEMA, 50 kutoka CCM au 100 kutoka CUF na TLP, sisi wote wanaotaka kuwa wanachama watawasilisha maombi yao, watafanyiwa usaili ili kujua ni watu wa namna gani kwa kupima kama wanaamini itikadi na nia ya chama, kama kweli ni Wazalendo wenye nia ya kufanikisha malengo ya Chama ambayo ni kumtumikia Mwananchi na zaidi ni kuwajua kiunagaubaga chimbuko la msisimko wao wa kuvutiwa na kujiunga na PPPT.
Zaidi, tuwaweka mizani na usaili wa kujua mwanzo wa maato si ya Chama pekee, bali hata ya Wanachama wetu kwa kuhakikisha kwa kutumia vitendo kuwa Watakaochaguliwa kuwa viongozi, wanaweka wazi maisha yao, kuanzia ajira, mapato, mali, mahusiano ya jamii na kila kitu ili tuondokane na ugonjwa ambao umevishika vyama vingine.
Nia si kukata kuwa na Wanachama au kuwa na njozi za Utopia za kuwa na watu TIMILIFU wasio na kasoro, bali nia ni kupunguza shida za huko mbeleni na makosa yaliyofanywa na vyama vingine ambavyo vilikimbilia kukumbatia Wanachama ambao walikuwa wanajiunga ndani ya vyama hivyo kwa utashi na masuala ya ubinafsi na si kwa manufaa ya Watanzania na kulijenga Taifa.
Watakao ingia chamani watapigwa msasa ili waishi kwa mfano katika mitaa yao, na watakapoanza kwenda sambaza habari kwa wananchi kuhusu chama, itawapasa wajue misingi halisi ya chama na kukielewa kinagaubaga.
Kama vile watu wanavyopelekwa Madras au Mafundisho ya Kipaimara au hata kubattizwa, ndivyo sisi tutakavyoanza kujijenga kwa kuhakikisha kuwa anayejiunga, hafanyi kwa ajili ya ushabiki tuu, bali ana amini kile kinachosemwa na chama na yu tayari kusaidiana na Wanachama wenzake kuijenga upya Tanzania.
Lengo si kuchuja wanaotaka kuwa wanachama, bali ni kuwa na wanachama ambao watajua fika kuwa wajibu wao mkuu ni kumtumikia Mtanzania kwa Manufaa ya Tanzania kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Katiba ya Tanzania.