Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
- Thread starter
- #121
Huku ni kutucheleweshea ukombozi wetu kwa kuendelea kuzigawa kura za upinzani..! Nchi hii iko kwenye hali ya dharula hatuwezi kuendelea kusubiri..ukombozi unahitajika haraka...basi potelea mbali na mi naanzisha changu!
Kaka Mawazo Matatu aka Sankara,
Ukifanya mambo kwa pupa, bila kujipanga, utaishia kuwa kama vyama vyote vya Upinzani ambavyo leo hii kila mtu ana misukosuko.
Nenda CUF, CHADEMA, TLP, NCCR, UDP kuna kila aina ya rabsha kwa kuwa kila mtu alikuwa anafanya mambo kwa uharaka lakini hawakujijenga kichama na hawakujijenga kwa Watanzania.
Wengi wamekimbilia majukwaani kutokana na Umaarufu waliokuwa nao, kama Sefu Hamad, Agustino Mrema, John Cheyo, Mabere Marando, Christopher Mtikila, Freeman Mbowe, Emmanuel Makaidi, na wengine wengi ambao kutokana na umaarufu wao, uliwavutia watu wengi kujiung na vyama hivyo.
Lakini, tumejifunza na tunaendelea kujifunza kuwa, kuna Wanamapinduzi wengi ambao wamejiunga katika vyama vya Upinzani na hata chama tawala CCM, lakini wakakutana na magenge na vitimbi ambavyo kamwe havijengi chama, wamekuta vyama vikiwa havina nia ya kujijenga na kukubalika kisiasa hata kujiyolea kujenga nchi bila kuwa madarakani.
Nao wananchi walikimbilia kujiunga na vyama hivi si kama tegemeo la ukombozi, bali ni mapenzi na ushawishi wa yule aliye kiongozi mkuu au kutokana na mambo fulani ambayo ni kero za kisiasa. Ndio maana unaona Pemba nzima ni CUF na Kilimanjaro miaka kadha iliyopita ilikuwa ina msukumo mkubwa kati ya CHADEMA, NCCR na TLP.
Nakutakia safari njema katika harakati zako, lakini ujue ukiendeleza pupa, tutakusikia kama kina Mrema na CHADEMA kuwa kuna mfarakano!