Progressive People's Party of Tanzania

Progressive People's Party of Tanzania

Huku ni kutucheleweshea ukombozi wetu kwa kuendelea kuzigawa kura za upinzani..! Nchi hii iko kwenye hali ya dharula hatuwezi kuendelea kusubiri..ukombozi unahitajika haraka...basi potelea mbali na mi naanzisha changu!

Kaka Mawazo Matatu aka Sankara,

Ukifanya mambo kwa pupa, bila kujipanga, utaishia kuwa kama vyama vyote vya Upinzani ambavyo leo hii kila mtu ana misukosuko.

Nenda CUF, CHADEMA, TLP, NCCR, UDP kuna kila aina ya rabsha kwa kuwa kila mtu alikuwa anafanya mambo kwa uharaka lakini hawakujijenga kichama na hawakujijenga kwa Watanzania.

Wengi wamekimbilia majukwaani kutokana na Umaarufu waliokuwa nao, kama Sefu Hamad, Agustino Mrema, John Cheyo, Mabere Marando, Christopher Mtikila, Freeman Mbowe, Emmanuel Makaidi, na wengine wengi ambao kutokana na umaarufu wao, uliwavutia watu wengi kujiung na vyama hivyo.

Lakini, tumejifunza na tunaendelea kujifunza kuwa, kuna Wanamapinduzi wengi ambao wamejiunga katika vyama vya Upinzani na hata chama tawala CCM, lakini wakakutana na magenge na vitimbi ambavyo kamwe havijengi chama, wamekuta vyama vikiwa havina nia ya kujijenga na kukubalika kisiasa hata kujiyolea kujenga nchi bila kuwa madarakani.

Nao wananchi walikimbilia kujiunga na vyama hivi si kama tegemeo la ukombozi, bali ni mapenzi na ushawishi wa yule aliye kiongozi mkuu au kutokana na mambo fulani ambayo ni kero za kisiasa. Ndio maana unaona Pemba nzima ni CUF na Kilimanjaro miaka kadha iliyopita ilikuwa ina msukumo mkubwa kati ya CHADEMA, NCCR na TLP.

Nakutakia safari njema katika harakati zako, lakini ujue ukiendeleza pupa, tutakusikia kama kina Mrema na CHADEMA kuwa kuna mfarakano!
 
Tumeusoma mchango wako hapa jamvini, msimamo wako na potential uliyonayo ni ya matamanio kwetu na natumaini kwa Watanzania wote. Tunakupatia mwaliko maalum kujiunga nasi. Ni matumaini yetu kwamba utakuwa moja ya nguzo imara katika kufanikisha na kutekeleza sera za kilimo na uchumi. Karibu sana Zakumi!

SteveD:

Naona ziara aliyofanya Rev. Kishoka kutembelea motherland hivi karibuni imembadilisha kutoka mcha Mungu mpaka kumlilia shetani Lowassa kurudi madarakani hili vitu fulani vifanyika. Na sasa yupo mbioni kuanzisha chama cha siasa.

Kuhusu sera za kilimo na uchumi, hakuna kipya. Matatizo ni kuwa watu wanapanga vizuri na baadaye kuhamua kufanya vingine. Ukimuona mtu anakwenda ch00ni na kuhamua kushusha kifaru pembeni wakati choo kipo safi, ujue huyo ana matatizo mengine. Hivyo kujengea choo kipya haitamsaidia.
 
- Mchungaji usisahau kupitia Bagamoyo lazima ukatengenezwe kidogo mkuu, usione vyaelea vimeundwa yakhe!

Respect.

FMeS!

Mchungaji Bagamoyo imepitwa na wakati usijali kuhusu hayo ukifanya na kumaanisha uliyoyasema ipo new knowledge ya kutembea juu ya maji bila kuzama. Mimi ndo ntakuwa katika kamati ya ufundi na master mind wa mambo ya ki spiritual mpaka tufagie kila uvungu ndani ya nchi yetu; huko Bagamoyo watapiga magoti mchana kweupeeeeee na kuomba upya usajili. Wataaminije tusipowaonyesha? Kwahiyo songa mbele mwanzo wa ngoma ni lele; ni heri kufa ukiitetea nchi yako kuliko kufa ukibeba mabox ya waliotutumikisha kifikra na kivitendo.
 
Kutakuwa na taratibu gani za kufikia maamuzi mazito ya chama, mfano uteuzi wa viongozi kitaifa? Je, kabla ya vikao vya jumla ni taratibu gani zitakuwapo ili kuwezesha vikao vikuu kufanyika?

Kijunjwe:

Nadhani mwaka jana ulifuatilia jinsi Obama na MaCain walivyoteuliwa na kushirki kwenye uchaguzi wa rais hapa US. Katika process nzima sikuona vikao vya kamati kuu au halmashauri kuu. Sisemi kuwa watanzania waige hii process, lakini ukiondoa mentality kuwa CC and NEC are the only ways, you will probably find something better.
 
Mchungaji napenda kuamini kuwa hii ni thread uliyoileta kupima upepo tu! Ila kuna kitu kimoja ambacho mimi nafikiria ndio hasa kizuizi cha demokrasia ya kweli TZ nacho ni CCM. Hawa ni kama ukuta mkubwa ambao bila kuunganisha nguvu zetu si rahisi kuuangusha! Ili tuweze ku break through kuelekea Demokrasia ya kweli Tanzania lazima CCM ianguke kwanza! Iwe kwa kumegeka au kwa kuanguka nzimanzima kama ilivyo! Na hilo linawezakana tu kama tutakua na muungano wa hiali wa vyama vya upinzani au baada ya kufa kwa vyama vidogo vidogo vya upinzani kwa kumezwa na vyama vikubwa ili kubaki na vyama vichache(viwili ama vitatu) vya upinzani vyenye nguvu!
Sijui kama umejiuliza kitu kimoja kikubwa kabla ya kuwaza kuanzisha chama kipya

Umejiuliza ni rasilimali gani unahitaji na utazipata vipi? kwa gharama gani? kuanzisha chama hadi kikawa na mtandao mkubwa wa kutosha kuenea Tanzania nzima na kuwa na mwakilishi kwenye kila kaya 10 za Tanzania ili kuweza kulingana ama kukabiliana na mtandao walionao CCM.? Kumbuka vyama vya upinzani vina miaka 17 na hadi leo havijaweza hili?
 
Ingekuwa vyama ni kuwa mtu unatamka tuu kiwe na kikawa leo tungekuwa navyo vingi sana.

Hata juzi nilisoma kuwa kipo kipya kimesajiliwa na kauli mbiu yake ni kilimo kwanza.
 
SteveD:

Naona ziara aliyofanya Rev. Kishoka kutembelea motherland hivi karibuni imembadilisha kutoka mcha Mungu mpaka kumlilia shetani Lowassa kurudi madarakani hili vitu fulani vifanyika. Na sasa yupo mbioni kuanzisha chama cha siasa.

Kuhusu sera za kilimo na uchumi, hakuna kipya. Matatizo ni kuwa watu wanapanga vizuri na baadaye kuhamua kufanya vingine. Ukimuona mtu anakwenda ch00ni na kuhamua kushusha kifaru pembeni wakati choo kipo safi, ujue huyo ana matatizo mengine. Hivyo kujengea choo kipya haitamsaidia.

Zakumi,

Kama ni kunitusi, basi leo umenitusi.

Nimekwenda nyumbani nikajionea. CCM wanashambulina, wanaoneana haya, wanadanganya umma wa Tanzania. CHADEMA hawaaminiani, TLP wako likizo, kidogo CUF ndio walikuwa wakililia daftari la wapiga kura Serikali za mitaa.

Sasa mbaya zaidi, Watanzania wameamua kuridhika na tabu, mateso, kero na shida, na wala hawajali kulalamika, wao Liwalo Liwe!
 
Mchungaji;

Hatua ya Kwanza ya kwenda kwenye mafanikio ni kuwa na ndoto. Na maadamu ndoto yako ina vision yenye matumaini tofauti na zile za vyama vya mfukoni, nadhani sasa ni wakati wa kusonga mbele.

Ukweli kuwa uchungu wako wa Nchi hii umeonekana hapa jamvini kupitia mabandiko yako tofauti, hii inatia moyo kuwa nia yako ni thabit.

Wazo: Ni vema Chama kikawa na Jina la Kiswahili ili kieleweke hadi Vijijini kwa Jina rahisi.

Tuko pamoja.

Ikifika kwenye kuweka mikakati ya Kushinda Uchaguzi, (I Dont know when), Nitafute, I am good on that and I am giving you my 100% Support.
 
Zakumi,

Kama ni kunitusi, basi leo umenitusi.

Nimekwenda nyumbani nikajionea. CCM wanashambulina, wanaoneana haya, wanadanganya umma wa Tanzania. CHADEMA hawaaminiani, TLP wako likizo, kidogo CUF ndio walikuwa wakililia daftari la wapiga kura Serikali za mitaa.

Sasa mbaya zaidi, Watanzania wameamua kuridhika na tabu, mateso, kero na shida, na wala hawajali kulalamika, wao Liwalo Liwe!

Rev. Kishoka:

Samahani mkuu. Sikuwa na nia ya kutukana bali ziara yako ilikuwa ni reflection ya ziara niliyofanya mwaka jana.

Niliporudi tu na kutulia nikasema what the heck, nika-submit application yangu ya kubadilisha uraia.
 
Chama chako kina tofauti gani na PPT-Maendeleo cha Peter Mziray?
 
Vyama vya mtandaoni, je?unajua kuwa Tanzania ni asilimia 12 tuu ndio wenye umeme?
Je?wajua kuwa watu wenye uwezo wa kutumia kompyuta ni asilimia 6 tuu ya watanzania wote?

Jiulize wenye internet ni wangapi hapo, then endelea na kuanzisha chama chako cha kwenye mtandao.

Ila kama wewe ni mchungaji mwenye maadili unakaribishwa CUF, CHAMA CHA WANANCHI ILI TUUNGANISHE NGUVU PAMOJA.
 
Vyama vya mtandaoni, je?unajua kuwa Tanzania ni asilimia 12 tuu ndio wenye umeme?
Je?wajua kuwa watu wenye uwezo wa kutumia kompyuta ni asilimia 6 tuu ya watanzania wote?

Jiulize wenye internet ni wangapi hapo, then endelea na kuanzisha chama chako cha kwenye mtandao.

Ila kama wewe ni mchungaji mwenye maadili unakaribishwa CUF, CHAMA CHA WANANCHI ILI TUUNGANISHE NGUVU PAMOJA.

Hakisawa naona amerudi baada ya ile skendo yake ya kubandika JF kabla ya kuwa member.
 
Mkandara,

Umeshawahi kuisikia ile hadithi ya Mpanzi ambayo bwana yesu aliitoa? Hekaya hii iko kwenye Injili ya Matayo mlango wa 13 na nanukuu sehemu hii ambayo ndiyo naifananisha na sababu ya sisi kuanzisha PPPT.

3And he spake many things unto them in parables, saying, Behold, a sower went forth to sow;
4And when he sowed, some seeds fell by the way side, and the fowls came and devoured them up:
5Some fell upon stony places, where they had not much earth: and forthwith they sprung up, because they had no deepness of earth:
6And when the sun was up, they were scorched; and because they had no root, they withered away.
7And some fell among thorns; and the thorns sprung up, and choked them:
8But other fell into good ground, and brought forth fruit, some an hundredfold, some sixtyfold, some thirtyfold. 9Who hath ears to hear, let him hear

Sisi PPPT tunataka tuwe mbegu bora na tuwe Mpanzi aliyepanda mbegu bora na si mbegu iliyoangukia kwenye miiba au ardhi isiyo na rutuba.

Tunataka tufanye kazi yetu kwa umakini, hivyo wakati wa mavuno, matunda bora yaonekane na kuneemesha jamii.
 
Umekwisha kisajili chama chako? Ops Hiki chama?
 
Mkandara,

Umeshawahi kuisikia ile hadithi ya Mpanzi ambayo bwana yesu aliitoa? Hekaya hii iko kwenye Injili ya Matayo mlango wa 13 na nanukuu sehemu hii ambayo ndiyo naifananisha na sababu ya sisi kuanzisha PPPT.



Sisi PPPT tunataka tuwe mbegu bora na tuwe Mpanzi aliyepanda mbegu bora na si mbegu iliyoangukia kwenye miiba au ardhi isiyo na rutuba.

Tunataka tufanye kazi yetu kwa umakini, hivyo wakati wa mavuno, matunda bora yaonekane na kuneemesha jamii.
Hiyo Hadithi ninaifahamu sana ila mkuu mchungaji hapa kidogo umenichanganya.. Unaposema uwe mbegu na Mpanzi mnaweza kuwa yote haya mawili kivipi?..
Pili, Hivi unayodai yanawezekana kweli maanake hata Yesu mwenye kila nguvu ya uwezo, anatuhakikishia baadhi ya mbegu ziliangukia juu ya jiwe. Sasa kama ni Mpanzi ni lazima ufahamu kuna mbegu hazitaota, Na kama nyie mbegu ni lazima kuwepo na Mpanzi, Mpanzi ambaye ana baraka kubwa ya uhakika kiasi cha asilimia 99% kama Yesu.
 
Mkandara & Kishoka:

Mnaanza kuzidisha longolongo. Ingawaje mi ni mchunguliaji, nina hamu sana na hiyo next step.
 
Mkandara,

Sisi ni mbegu iliyopandwa kwenye rutuba, haikuangukia kwenye miiba, au kwenye ukame na jua kulikausha. Tumejipiga vifua na kugeuka kuwa mbegu iliyoangukia kwenye udongo wa rutuba. Tulichojifunza kutoka wa Waasisi wa nchi yetu na kwingineko hata ughaibuni kunatufanya kuwa mbegu bora maana tuna moyo wa kuleta maendeleo kwa Taifa na si kwa nafsi zetu pekee.

Kama tungekuwa ni wabinafsi, tungeendelea kubeba maboksi na kuzimumunya kuku za KFC na McDonald na kuwaacha Watanzania wasote. Lakini ile mbegu ya Uanamapinduzi iliyopandwa ndani ya mioyo yetu, ndiyo inatufanya tujitolee na kuunganisha mikono na kuanza kazi mpya.

Nafasi yetu kama Mpanzi ni kuwa nasi ni zamu yetu kusia mbegu na kuzalisha. Ndio maana tunalichukulia jukumu hili kwa mkao tofauti. Badala ya sisi kusia mbegu na zingine zikapeperuka kwenye miiba au kuangukia kwenye ardhi kavu na magugu, sisi tunadhamiria kupanda mbegu za Uanamapinduzi, kujitolea, ufanisi na kujitegemea kwa Watanzania wote bila kujali walikotoka au wanaloamini.

Tumejifunza mengi kutoka kwako kaka, Watu na Mazingira, sisi tutalifanyia kazi na ndio maana tunasema, hatutakimbilia Ubunge au Ikulu, bali ni kujenga mfumo wenye rutuba kwa manufaa ya Watanzania wote.
 
Rev. Kishoka:

Samahani mkuu. Sikuwa na nia ya kutukana bali ziara yako ilikuwa ni reflection ya ziara niliyofanya mwaka jana.

Niliporudi tu na kutulia nikasema what the heck, nika-submit application yangu ya kubadilisha uraia.

Shemeji yako alinishikia bango akasema nigeuke Tai, nikamuambia nitabakia Twiga.

Unaweza kukata tamaa kama huna ujasiri.

Kwenye ombi lako la hatua zitakazofuata, endelea kujumuika nasi kwenye majadiliano haya.
 
Mkuu kama nilivyo ahidi nitakaa na kulifikiria hili swala vizuri ndiyo nije nichangie.

Mkuu kwanza it takes more than just simple idea to make something work. It is the follow through that is most important. Mtu unaweza ukawa na idea ya picha nzuri kichwani lakini ukiichora isitokee kama ulivyo waza. Cha kujiuliza ni ume jiandaa vipi kufollow through? Na kumbuka kuwa lawama kubwa CCM inayo beba sasa ni kuto kutekeleza ahadi zake.

Chama chochote cha siasa kina hitaji pesa za kujiendesha. Tuwe wa kweli bila pesa hauwezi kuendesha chama. Sasa mkuu ume jiandaaje linapo kuja swala la kuendesha chama? Kama ni funds zako mwenyewe unazo za kutosha? Kama kuna other sources hizo source zingine ni zipi na zinaeleweka? Maana mambo haya mengine they can come back to haunt you vibaya sana.

Chama ni team work na kama unavyo jua there is know "U" in team. Sasa wewe utakua na nafasi gani katika chama na ni watu gani umepanga kuwa weka kwenye safu yako? Je moja kwa moja una jiweka kwenye "kiti kikuu" cha chama au kutakua na uchaguzi kwanza? Je kama itaonekana mwingine anafaa kuwa mwenyekiti upo tayari kumuachia uongozi katika chama ulicho kiasisi mwenyewe?

Ume tupa rough summary ya chama chako lakini bado hauja tuwekea katiba kamili na ilani ya chama chako. Nadhani ingekua vyema tukajua kwa kirefu zaidi kuhusu katiba na mipango ya chama chako. Pamoja na kwamba umeweka kwa kifupi mipango yako kwa Watanzania je chama chako kimejiandaa vipi kurithi matatizo ambayo yapo? iwe kwenye ngazi ya kata mpaka uongozi wa juu wa nchi.

Je umefanya research na kugundua Watanzania wana taka nini na ni vitu gani vitafanya chama chako kikubalike? Je mmejiandaa vipi kuongea na wananchi wa kawaida? In short mnaijui reality on the ground?

Mwisho kabisa mimi kama kijana nabidi nijiulize chama chako kina mikakati gani na vijana? Je chama chako kita tumiaje vipaji vya vijana mbali mbali? Je mtaandaaaje vijana wa chama chenu kuwa viongozi vizuri wa baadae?

Nadhani kwa sasa ni haya tu. Nikipata vingine vya kuongezea nita bandika post nyingine. Mungu akubariki mkuu na aku tangulie.
 
Back
Top Bottom