Progressive People's Party of Tanzania

Bado anapata ushauri kutoka kwa Makamba. Akikamilisha tu ajenda yake na CCM natumaini atakuwa na matamanio ya kujiunga nasi. Vipi wewe... kwanini usijiunge nasi bob?!

SteveD na Rev.
Salaam za Heri,
NAOMBA NAMBA WAKUU
 
Rev Kishoka;

Amani iwe juu yako. Mimi kadi yangu ni namba tatu, wewe, Steve na yangu. Unajua namna ya kunipata.

Chama lazima na muhimu kiwe na jina la kiswahili, kumbuka wanachama wetu wengi tunawategemea kutoka vijijini. Vijiji ndo itakuwa ngome kuu, vijiji ndo vinachagua rais na wabunge. Mijini longolongo hawapigi kura, wanashinda tu hapa JF

Kwahiyo basi nashauri kyama kyetu kiwe na jina la Chama cha Maendeleo Ya wananchi Tanzania, au Chama Cha maendeleo Tanzania, au Chama cha Kuwaendeleza wananchi Wa Tanzania -CKWT. Fikiria hilo ila ni muhimu.

Nimependa mrengo wa kati kwasababu tutaweza ku moderate wenye mrengo wa kushoto na kulia.

Main base yetu iwe vijijini na focus ielemee huko.

Tutahitaji fedha kwa ajili ya Kwenda vijijini, inabidi tukae mimi wewe na SteveD tulifanyie kazi hilo.

Watu wenye Migogoro au waliotimuliwa kwenye vyama vyenye migogoro kutokana na migogoro hatuwataki. Kama mtu au kiongozi ana tu join aje akiwa ameachana na chama chake kwa AMANI.

Inabidi tuanzishe vyombo vya habari ambavyo vitalenga zaidi vijijini, namna na ufadhili niachieni nisije kumwaga kuku kwenye mtama wengi bureeeeee!, kwanini pia naomba nisiulizwe.

Kyama kyetu kisiteuwe au kuwapigia kura wakurugenzi wake..... nina sababu na nitaziongelea kwenye kujadili RASIMU ya KATIBA ya chama.

Tunahitaji fedha..... hilo nalo pembeni.

Naomba kuwakilisha maombi na maoni yangu. Ni mategemeo yangu kuwa maombi yangu ya uwanachama yatakubaliwa.

Ndimi mwanachama mtarajiwa namba tatu

FP
 
Hili jina si geni masikioni mwangu.........! humu sio mule alipokuwepo somebody ABUBAKAR? na kile cha MWAKITWANGE kilikuwa kinaitwaje?
naomba kujuzwa...!
Kipo chama kinaitwa PPT-Maendeleo, kinaongozwa na jamaa anaitwa Peter Kuga Mzirai. Ndicho kilisimamisha mgombea mwanamke kwenye nafasi ya uarais uchaguzi mkuu uliopita na ndiye ambaye amerejea CCM hivi majuzi
 


Sikuwahi kufikiria kuwa mwanachama wa chama chochote lakini kwa chama hiki nitakuchukua kadi...!!! Best wishes
 

Good luck :lakini kwa bahati mbaya hukubahatika kujifunza kwa ASP.
 
Jina la chama: Progressive People's Party of Tanzania
Kwa kiswahili: Chama cha Maendeleo Endelevu ya Wananchi
Kwa kifupi: "Wananchi na Maendeleo"

Ushauri;
kwenye makabrasha ya chama twende na hayo majina ya kithungu, lakini mitaani twende na
" Wananchi na Maendeleo"

Ushauri tu!
 

lol, this is some classy humor!! 🙂
 
That's good point to note. Tatizo mojawapo kubwa la upinzani Tanzania limekuwa ni influence kutoka kwa waasisi wa vyama ambao wengi wao ni x-CCM. Hii imesababisha vyama vingi kuwa na sera na katiba zinazofanana na zile za CCM kwa namna fulani hivyo kupoteza maana halisi ya chama cha upinzani. It's about time we have a really opposition party.
Kadi namba nne please!
 
Ushauri;

Core Values;
"-We believe and recognize that every party has played significant role in our national development"

However, we are not satisfied with the result and pace of development, this is the reason why we introduce another party to serve the people of Tanzania.


Hatupo kubeza yale yaliyofanywa na wengine, bali kujenga juu ya yale mazuri na kwa speed ya light.
 

Philosophically, hili sidhani kama ni sahihi sana. Kukubali kutosahihisha yale unayoona mabaya, na ambayo yamekufanya uchukue uamuzi wa kuanzisha chama na harakati zako mpya, si kuuma na kupuliza tu, bali ni kujaribu kuficha maovu ya wale waliopita na kuharibu au kusababisha hayo maovu.

Na pale unapokubali kujenga juu ya mazuri ya hao unaotaka kupingana nao (maana katika siasa hakuna neutrality), swali linaloibuka ni kuwa- kwanini usijiunge huko huko na kuendeleza hayo mazuri kuliko kujifanya unapaka rangi na kujenga partition ndani ya nyumba wakati ukiwa umesimama nje?!!

Mkuu Kasheshe, kuna wakati huwa ni vyema kubomoa au kuanza na msingi. Naamini umeshafikia uamuzi kama huo mara kadhaa pale computer yako inapokuwa kero, badala ya kupatch, unafuta kila kitu na kuanza na OS installation. Katika hili, chukulia kuwa hii PPPT ni OS mpya iliyokuwa designed specifically kuwa very efficient, cheap to run and install kwa mashine inayozeeka na kuwa kero kwa mtumiaji. You get the gist!
 
Mchungaji
Una mikakati gani ya kuvutia wapiga kura?

Huku uswahilini mambo si mchezo ati. Chama chaweza kufa kabla ya kuzaliwa.
 
Waungwana,

Maboksi yamenishinda, narudi nyumbani na narudi kuanzisha chama. John Tendwa naomba ajiandae kwa ujio wa Mchungaji.

Chama changu kinalenga kuleta maendeleo kwa Mtanzania na si kwa kauli tuu bali kwa vitendo.

Akhsanteni,


Kishoka,

Mie wasiwasi wangu ni hapo kwenye maneno "chama changu". Kama kweli kutakuwa na Demokrasia, hivi akaja mtu mwengine mwenye nguvu zaidi ya kushawishi wapiga kura na kutaka kukiteka CHAMA CHAKO kama ambavyo Zitto alitaka kukiteka CHAMA CHA MTEI/Mbowe (CCM?) utakuwa tayari ku-step down na kusubiri kama jamaa ataboronga, basi wanachama wakurudishe tena kwa njia ya demokrasia au uwekwe pembeni milele na ukumbukwe tu kama mtu aliyeleta demokrasia ya kweli Tanzania?

Mie wasiwasi wangu siku zote ni hapo tu. Na miiko gani ya viongozi kama chama mtajiwekea 'in advance'. Hii miko ndiyo itakuwa kama mwanga wa nini kitatokea kama mtashinda uchaguzi. Mtu kama ni FISADI basi mapema kabisa ataambiwa achagua kuwe kiongozi au arudi akaendelee na kuganga njaa/kufanya biashara zake. Wadhamini wote lazima waandikwe na wawekwe wazi na chama kisikubali kupokea hela kubwa kubwa maana nidyo kujitundika kitanzi. Heri kupokea tuseme max. 10 mlns Tsh.

Mwisho kama nilivyosema hapo zamani, chama hiki kiwe chama cha kwanza kufanya mikutano yake hadi ONLINE ili hata wale Watanzania waliokwama kufika kwenye kikao, waweze kuhudhuria hata kama kwa siku hiyo watakuwa kwenye kuvua samaki bwawa la Igombe.

Kama hayo juu, hasa lile la kwanza na MIIKO ya viongozi likiwa limeandikwa na kuwekwa wazi, basi Mchungaji, mie ni MWANACHAMA.
 

Ama kweli wewe unajua kweli kunisoma...umeweza ku relate na maisha halisia ya Mkerewe.

Rev. Kishoka, Steve, Kasheshe, Fairplayer na wengineo nyote..
Nawapeni pongezi sana kwa maamuzi yenu lakini tafadhali nakuombeni kufikiria kitu moja tu..
Kwa nini nyote kwa pamoja msijiunge na Chadema kwanza mkajaribu kukibadilisha kuondoa udhaifu ili kiweze kukabiri vizuri uchjaguzi wa mwaka 2010.
Ninazo sababu muhimu sana ktk mawazo haya kwani wakuu zangu Wananchi wamechoka.. Taifa letu halina muda wa kusubiri Nabii kwa miaka 10 au 20 ijayo..Na kuanzishwa kwa chama hiki kipya hadi kufikia mahala kimesimama sawasawa itachukua muda huo. By then mtaikuta nchi kama Ethiopia ya 1982..
Pili, navyofahamu mimi Chadema inahitaji vijana kama nyie makini ili kuwawezesha kuchukua ushindi wilaya na mikoa ktk uchaguzi mkuu ujao 2010. Na ikiwa mtafanikiwa ni imani yangu kubwa kwamba UMOJA wenu vijana chini ya chama kimoja ndipo pekee mnaweza kuiangusha CCM, laasivyo kugawanyika kwenu ktk makundi hakuwezi kabisa kumwondoa CCM.
Binafsi naamini kwamba kisiasa Adui wa wananchi hivi sasa ni CCM - UONGOZI..nakubaliana na maneno ya mwalimu kimsingi kwamba nchi yetu ili ipate kuendelea inahitaji vitu vinne ARDHI WATU, SIASA SAFI na UONGOZI BORA..katika hayo chama chenu kimechukua uzito zaidi ktk Watu na Mazingira ambayo ni sehemu kubwa ya hekima ya mwalimu.
Lakini maadam tunakosa Siasa safi, siasa inayokana Ubwana na utumwa ndipo nyie mnapokuja na PPPT. Zote hizi ni nyenzo muhimu sana ktk MAHITAJI yetu ya maendeleo lakini kabla hatujafika huko kuna kitu Emergency hapa - Uongozi bora ni TATIZO kubwa, tatizo ambalo linahitaji kuziba Ufa huu kwanza laa sivyo itatubidi tujenge Ukuta mzima..
Matayarisho yenu yote hanakosa kutazama kiini cha TATIZO hili la UONGOZI BORA ambalo ndio sababu kubwa ya kuzaliwa kwa UFISADI... Na UFISADI ndio kilema cha maendeleo yetu kwa ujumla.
Kwa hiyo ningeshauri kuchukua maamuzi ya dharura kwanza, kuondoa hii shida kubwa ya Uongozi bora kwa kuziba nyufa zilizopo. Mkifanikiwa kuchukua majimbo mkiwa na azma moja tu ya kuziba ufa huu mkubwa uliopo ktk uongozi bora bila shaka Ufisadi utakosa nafasi pia na itakuwa rahisi kwenu ku practice kile mnacho preach.
Wakuu zangu DAWA ya Ufisadi ni Uongozi bora, tunahitaji tiba ya haraka na kuwaweka waathirika kwenye karantini ili maradhi haya yasisambae zaidi..kisha ndio pale tutaweza kusimamisha sheria (Vaccine) kwa kutumia Siasa safi ambayo kwa hivi sasa naweza sema bado ipo Lab ikifanyiwa majaribio.
Nawaombeni sana mfikirie hili kwa makini sana mkizingatia zaidi yale yaliyopo usoni mwetu. Ufisadi umekithiri nchini na sidhani kama kuundwa kwa chama kipya ndio Solution ya dharura hii isipokuwa ni ktk malengo ya muda mrefu (long term strategy).. hivi sasa tunahitaji Umeme, Chadema sii Dowans wala Richmond..ni mtambo wa wananchi uliopo na unafanya kazi chini ya kiwango chake, kinachotakiwa ni kufanyiwa ukarabati ambao kwa imani yangu nyie wakandarasi mnaweza kabisa kuwasha hizo Mw zilizopungua na kuiwezesha nchi nzima kutoka kizani for the time being!
 
- Mchungaji usisahau kupitia Bagamoyo lazima ukatengenezwe kidogo mkuu, usione vyaelea vimeundwa yakhe!

Respect.

FMeS!

FMES mimi siamini sana haya mambo lakini hivi ni ukweli ukitaka kuwa mwanasiasa TZ lazima ukatengenezwe
 

I like that, wakikiita hivyo itakuwa sawa kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…