Project 2015: Mwinyi haoni uharaka wa Katiba Mpya

Maneno mengine uwezi amini kabisa kama yanaweza toka kwa mtu kama huyo,yaani ni vitu vya ajabu sanaaaaaaaaaa

Pamoja na ukweli kua mzee Mwinyi amezeeka lakin hao ambao bado ni vijana pia akili zao bado zinatia mashaka. Wabong hua tunachukia sana kuanalayse mambo na tunapenda kukimbilia kwenye conclusion, badala ya kujibu hoja utamsikia mtu anasema oo ni kwanza Mwinyi ni mzee atakufa kwani kuna atakaebaki hapa duniani milele?

Kwa wale wanaodai katiba mpya hawapendi kua wazi kwa mifano kua labda ni vpengele gani hasa vinahitaji mabadiliko au ni katiba yote. Kama ni katiba yote hakuna clear idea kua gharama zake zitakuaje na maswali mengi.

Sasa ili kujua kama Mwinyi amezeeka au bado tujaribu kujibu point zake pale aliposema.Kwanini mabadiliko yanatakiwa wakati huu? Je kuna uhakika gani kua mabadiliko yatatoa result inayotakiwa? Plus pale aliposema kua wasiwasi wake sana upo ktk njia zinazotumiwa kuleta katiba mpya kuliko hiyo katiba yenyewe.

email.png

Email

printer.png

Print

comment_bubble.png

Comments
 
kwa hio ww unaona kuwa watu wa pwani ni watu wa mambo madogo ?

jiulize kwa nn mji mkuu wa tanzania uko pwani na sio bara ?

Mkoloni aliona ni rahisi kujenga huko. Hivi unafikiri ingekuwa rahisi kujenga mji mkuu Iringa kwa Mkwawa, Tabora kwa Mirambo, Moshi kwa Mangi Meli.......n.k. Huko Pwani ndiyo ilikuwa rahisi kwa waswahili......!!!
 
he is dead living. anaweza kuropoka kitu cho chote, besides he may have less that 10 yrs to live. haoni hasara yo yote ile hata tukichinjana. He has already lived full life.

Pamoja na ukweli kua mzee Mwinyi amezeeka lakin hao ambao bado ni vijana pia akili zao bado zinatia mashaka. Wabong hua tunachukia sana kuanalayse mambo na tunapenda kukimbilia kwenye conclusion, badala ya kujibu hoja utamsikia mtu anasema oo ni kwanza Mwinyi ni mzee atakufa kwani kuna atakaebaki hapa duniani milele?

Kwa wale wanaodai katiba mpya hawapendi kua wazi kwa mifano kua labda ni vpengele gani hasa vinahitaji mabadiliko au ni katiba yote. Kama ni katiba yote hakuna clear idea kua gharama zake zitakuaje na maswali mengi.

Sasa ili kujua kama Mwinyi amezeeka au bado tujaribu kujibu point zake pale aliposema.Kwanini mabadiliko yanatakiwa wakati huu? Je kuna uhakika gani kua mabadiliko yatatoa result inayotakiwa? Plus pale aliposema kua wasiwasi wake sana upo ktk njia zinazotumiwa kuleta katiba mpya kuliko hiyo katiba yenyewe.

email.png

Email

printer.png

Print

comment_bubble.png

Comments
 
huyu naye ndo maana watu walimzaba kibao kwa mivitu yake ya ajabu ajabu..haoni umuhimu wa katiba mpya kwani hata iliyopo hakuwahi kuifuata wakati wa uongozi wake

Kweli; rejea jinsi alivyompa Mzee wa Kiraracha Unaibu PM wakati haujatajwa kwenye Katiba....
 
16th December 2010

email.png

Email

printer.png

Print

comment_bubble.png

Comments

headline_bullet.jpg
CUF`s Lipumba argues it will help democracy

Mwinyi(6).jpg

Retired President Ali Hassan Mwinyi

Retired President Ali Hassan Mwinyi has dismissed the idea of overhauling the country's constitution at this time, asking: "Why now?"
However Civic United Front Chairman Prof Ibrahim Lipumba said a new constitution was vital to meet the present demands.
Mwinyi was responding to questions from a team of journalists who interviewed him in Dar es Salaam yesterday on his stand on the rising calls for a new constitution, in Dar es Salaam.
Mwinyi said he does not support the idea of having a new constitution because the time is not right.
He said before changing the current constitution, Tanzanians should ask themselves in whose interest and for what goal they are seeking the changes.
He however said, there is room for discussions, but he does not support the way some people want to deal with it as hurriedly as if the country is missing something very special.
"What needs do Tanzanians not get today from the current constitution, that it should be changed so fast?" he asked.
"If there are areas in the constitution which need to be changed, then it should be amended" he added.
He cautioned Tanzanians against haste in dealing with the constitution because it may not give them the desired results. "Tanzanians should ask themselves, how many people are demanding for the new constitution. Is it for the elite?"
For his part, Prof Lipumba called upon Tanzanians to join forces in pressing for the new constitution.
He made the call when briefing journalists on the recommendations by party's National Governing council which met for two days in Dar es Salaam.
Prof Lipumba said the new constitution which would have true democratic base to draw up the national development vision for the benefit of the present and future generations was very crucial at this time.
"CUF joins other Tanzanians regardless of their ideologies or status, through democratic ways to demand for a new constitution to meet the current demands," Lipumba said.
He said the council also called on various stakeholders to support the demand for amendment of the Election laws and for an independent Electoral Commission, saying the current was not trusted by mostTanzanians.

MY TAKE:
Mwinyi knows the new constitution will work against his master plan to have his son vie for presidential post come 2015. Also the madudus that he did re Loliondo, IPTL etc will be in jeopardy.
Tumpuuze.....
Ni vizuri kuwaambia hawa wazee kuwa hii nchi sio yao na watoto wao pekee ambao ndio wanafaidi keki ya taifa,wanaogopa katiba mpya sababu wanaogopa kuletwa mahakamani kwa makosa walioyo ya "ruhusu",haturudi nyuma katu kuhusu suala la katiba,hiki ni kizazi kipya ,kila kitabu na zama zake mzee ruksa !1
 
Ngoma Ngumu:

Mimi ni mmoja wa watu wanaotaka mabadiliko ya katiba. Lakini mabadiliko ya hayo yanaweza kufikiwa kwa kufanya amendment ya katiba ya sasa. Hivyo anachosema Mzee Mwinyi kina ukweli na usahihi wake.

Lipumba anadai katiba mpya. Lakini wakati huo huo anao wabunge katika bunge la JMT ambalo wangeweza kutoa hoja ya kubadilisha baadhi ya vipengere. Kwa miaka mingi wabunge hao wamekaa kimya.
 
jiulize kwa nn mji mkuu wa tanzania uko pwani na sio bara ?

ndiyo mammbo madogo yenyewe hayo ninayosema.

yaani dar kuwa pwani basi wazaramo wamebweteka hata kujenga nyumba za maana hawawezi. shule hawataki.

wanafurahia kunywa kahawa chini ya maghorofa ya wahindi.

mtoto ana miaka mitatu anasoma 'chuo'.

watu wa pwani kweli akili zenu na za mbayuwayu sawasawa.
 
Pamoja na ukweli kua mzee Mwinyi amezeeka lakin hao ambao bado ni vijana pia akili zao bado zinatia mashaka. Wabong hua tunachukia sana kuanalayse mambo na tunapenda kukimbilia kwenye conclusion, badala ya kujibu hoja utamsikia mtu anasema oo ni kwanza Mwinyi ni mzee atakufa kwani kuna atakaebaki hapa duniani milele?

Kwa wale wanaodai katiba mpya hawapendi kua wazi kwa mifano kua labda ni vpengele gani hasa vinahitaji mabadiliko au ni katiba yote. Kama ni katiba yote hakuna clear idea kua gharama zake zitakuaje na maswali mengi.

Sasa ili kujua kama Mwinyi amezeeka au bado tujaribu kujibu point zake pale aliposema.Kwanini mabadiliko yanatakiwa wakati huu? Je kuna uhakika gani kua mabadiliko yatatoa result inayotakiwa? Plus pale aliposema kua wasiwasi wake sana upo ktk njia zinazotumiwa kuleta katiba mpya kuliko hiyo katiba yenyewe.

email.png

Email

printer.png

Print

comment_bubble.png

Comments

Msome huyo bwana hapo chinindiyo utapata picha kidogo.

Mwinyi aje na points badala ya kusema kwa nini sasa. Yeye anataka iwe lini kama siyo sasa?? au mpaka afe yeye kwanza??? Kwa mtazamo kama wa Mzee Mwinyi hata 2061 wakati tunatimiza miaka 100 ya uhuru kuna watu watahoji vilevile kwa nini sasa. Yeye hajui kuwa the time of change is now.

Waziri Kombani, ameshindwa kabla hajaanza

Samson Mwigamba

amka2.gif
NIMEKUWA nikijitahidi sana kutoa ushauri kwa watawala (si viongozi) wa nchi hii kutokana na kile ninachokiona huko mbeleni. Ushauri wangu wa bure ni kwa manufaa yao na taifa pia.
Nina wasiwasi kwamba huko tuendako taifa litalazimika kuongeza maradufu bajeti ya mahakama ili kuhimili kesi nyingi za ubadhirifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka, kuwa chanzo cha uvunjikaji wa amani ya nchi, kuiingiza nchi kwenye machafuko, kushiriki ama kusababisha mauaji ya halaiki, uhujumu uchumi, na kadhalika.
Kwa manufaa ya taifa na kwa manufaa ya watawala binafsi nawasihi wasome alama za nyakati na kubadilika. Nakuwa na wasiwasi na ongezeko la wagonjwa wa shinikizo la damu litakalotokea siku watawala walioko madarakani watakapopoteza madaraka.
Ugonjwa ni ugonjwa, hakuna anayependa ugonjwa na matokeo ya ugonjwa yako katikati ya kupona ama kifo. Nawasihi Celina Kombani na vigogo wenzake wote walioko madarakani wanisikilize japo kwa taabu sana na kuyatafakari maneno yangu.
Nawatakia mema, nawatakia kustaafu kwema baadaye ili wale pensheni yao kwa raha ile ile ya mzee Nyerere na mzee Mwinyi. Sitaki wapate shida wala kuipatisha shida serikali ijayo kila wiki kuwe na kiongozi mstaafu anayekwenda kutibiwa nje ya nchi.
Na mimi si mnajimu lakini nashawishika kwamba serikali ijayo baada ya kuanguka kwa ‘watawala’ wetu yaweza kuwa serikali ya wabana matumizi ya serikali kwa hiyo ikaweka hata masharti magumu kwa kiongozi kutibiwa nje ya nchi.

Celina Kombani, Waziri wa Sheria na Katiba, ni miongoni mwa viongozi ambao miaka michache ijayo wanaweza kuugua shinikizo la damu kwa kutoamini kilichotokea. Nasema hivyo kwa sababu ya matamshi aliyoyatoa hivi karibuni kwenye vyombo vya habari.
Waziri Kombani kwanza alisema hakuna haja ya Katiba Mpya eti iliyopo inatosha isipokuwa kama kuna watu wanalalamikia maeneo fulani fulani ya Katiba hiyo basi wapeleke malalamiko yao mezani kwake ili Katiba ifanyiwe marekebisho.
Akaenda mbali zaidi aliposema eti madai ya katiba si ya serikali wala Chama cha Mapinduzi wala wananchi wa taifa hili. Eti madai ya katiba mpya ni ya akina Tundu Lissu na CHADEMA. Akahitimisha kwa kusema serikali haina pesa za kuandika Katiba mpya.
Tatizo la hawa watawala ni kufikiri na kutenda kama Laurent Gbagbo wa Ivory Coast. Siku zote watawala wenye chama kinachoitwa cha mapinduzi wanafikiria mambo matatu makubwa. Kwanza wanafikiria kushinda na kushika dola. Kwao bila kushika dola hakuna CCM na hivyo CCM ni dola na dola ni CCM.
Ndiyo maana hata kauli mbiu zao za uchaguzi zaweza kuwa za aina ile ya “Ushindi ni Lazima”. Pili hufikiria kwamba lolote lenye maslahi na chama chao (maslahi yana maana kukisaidia CCM kubaki madarakani), lazima kienziwe jua liwake ama mvua inyeshe, wananchi watake ama wasitake, kiwe kina maslahi kwa taifa ama hakina maslahi kwa taifa.
Ni kwa sababu hiyo, katiba mbovu, tume nyonge ya uchaguzi, mfumo mbovu wa utawala, na mengineyo watayang’ang’ania hata kama taifa zima linalia. Mwisho siku zote CCM wanafikiri Watanzania ni majuha, wajinga na wasioelewa mambo ya uraia hivyo unaweza kuwapeleka utakavyo.
Nampa pole sana Waziri Kombani. Kwani amelewa mvinyo huo wa chama chake na wala hahitaji kujipa muda wa kufungua masikio asikilize kilio cha Watanzania. Na kilio kisitafsiriwe kama unyonge usio na mwisho.
Paka ni mnyama mpole sana anayeishi na mwanadamu kirafiki mno. Lakini jaribu kumkamata paka halafu ushike ule mkia wake uwe kama unauvunja halafu atafute chance uone atakavyokung’ata na meno na kukujeruhi vibaya. Namshauri Waziri Kombani ajiangalie upya na kuuangalia upya umma wa Watanzania anaowazungumzia.
Anaweza kudhani ni paka marafiki kumbe wameshashikwa mkia na wanatafuta upenyo wa kujinasua na watakapoamua kucharuka si Kombani wala rais wake watakaokuwa salama.
Hoja za Kombani zote ni za ‘kizushi’. Lengo lake kubwa ni kulinda maslahi ya CCM kwa sababu anajua Katiba Mpya ikiandikwa utawala wa kijanja kijanja wa CCM utakuwa hatarini. Anajua kama mwenyekiti wake taifa anavyojua na viongozi wote wakuu wa chama chao wanavyojua kwamba CCM haina mvuto tena kwa wananchi bali inaendelea kuwa madarakani kwa ‘uchakachuaji’ unaowezeshwa na ubovu wa katiba na ubovu mkubwa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Anasemaje kwamba taifa halihitaji katiba mpya wakati akijua kwamba mabadiliko ya katiba ya Zanzibar tu yameiathiri Katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa kiwango ambacho haifai tena kuwekewa viraka. Na hapo sijazungumzia mabadiliko ya kisiasa na kijamii achilia mbali suala la wakati linalotusukuma kuwa na katiba mpya.

Katiba ya Jamhuri imefanyiwa mabadiliko karibu mara 15 na sasa Kombani anadai mabadiliko mengine. Wakati wa kuingia vyama vingi Katiba ibara mbili za katiba yetu (namba 80 na 82) zilifutwa na leo Katiba ina kilema maana ukiisoma ukifika kwenye hizo ibara imeandikwa tu 80. (Imefutwa na sheria namba 4 ya mwaka 1992). Vivyo hivyo kwa ibara namba 82.
Leo Kombani anataka ibara ya kwanza tu ya Katiba iandikwe 1.(Imefutwa 2010 na mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ). Ibara ya pili hivyo hivyo. Sasa ni Katiba ya nchi gani ambayo unaifungua tu unakuta ibara ya kwanza na ya pili hazipo eti zimefanyiwa marekebisho. Ibara ya kwanza inasema: “ Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano” lakini Katiba ya Zanzibar kwa sasa inasomeka: “Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Viraka vitaendelea mpaka ibara ya pili kubadilisha maneno yanayodai kwamba rais wa jamhuri atagawa Zanzibar kwenye mikoa baada ya kushauriana na rais wa Zanzibar kwa kuwa katiba ya Zanzibar sasa inamruhusu rais wa Zanzibar kuigawa ‘nchi’ yake kwenye mikoa bila kushauriana na rais wa jamhuri. Bado hatujazungumzia kwenye ibara hiyo hiyo kuondoka kwa maneno “ Tanzania ni nchi ya kijamaa ya vyama vingi” wakati kiuhalisia nchi haiendeshwi kijamaa bali kibepari tena kwa kufuata soko ‘holela’ wala hata si soko huria. Tutalazimika kubadilisha aidha ibara ya 41 inayotamka: “Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi.

“Hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake”.
Ama tubadilishe ibara ya 107A inayotamka: “Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.” Kasoro nyingine kubwa ya Katiba ni ile inayoihusu Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inazungumziwa na ibara ya 116 hadi 123. Mahakama hiyo sasa haitambuliwi na Katiba ya Zanzibar.
Mimi si mwanasheria, naweza kukiri kwamba ni mbumbumbu wa sheria kama alivyo Waziri wangu wa Sheria na Katiba Celina Kombani. Pengine waziri wa sheria angekuwa mwanasheria mahiri kama Samwel Sitta ama Harrison Mwakyembe asingetoa kauli ya namna hii.
Mimi ni mtaalam masuala ya uhasibu niliyosomea Chuo Kikuu cha Arusha labda na masuala ya uhandisi ambayo niliyasomea kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam. Waziri wangu Kombani ni mtalaam wa masuala ya utawala wa umma (Public Administration) kutoka Chuo cha Mzumbe. Na kimsingi hatuna tofauti kwenye Katiba maana hata yeye anajua kwamba Katiba ina matatizo na ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi, utawala na demokrasia katika nchi yetu.
Tofauti na yeye ni kwamba yeye anajali zaidi maslahi ya watawala wakati mimi naangalia maslahi ya umma mzima wa Tanzania.
Hapa nimegusia tu mambo machache yanayoonyesha matatizo makubwa ndani ya katiba yetu. Sijagusia masuala mengine kama madaraka makubwa ya rais, mgawanyo makini wa madaraka kati ya mihimili mitatu ya dola, na mengineyo mengi.

Nina uhakika kwamba wanasheria wameshaanza na wataendelea kuichambua katiba yetu kama karanga na kutuonyesha kasoro nyingi ambazo zisipofanyiwa kazi sasa huko tuendako inaweza kuleta kasheshe kubwa. Chukulia mfano mdogo tu wa namna mgombea wa upinzani kupitia CHADEMA Dk. Willbrod Slaa alivyojizolea wafuasi nchi nzima halafu mwisho wa uchaguzi akaeleza wazi wazi tena kwa vielelezo kwamba kura zake zimeibiwa na kupewa mgombea aliyetangazwa mshindi na tume ya uchaguzi. Nini kingetokea kama angeamua kuwatangazia wafuasi wake kwamba hakubaliani na matokeo na kwa kuwa katiba haimpi nafasi ya kwenda mahakamani basi tuandamane kama Kenya ama Zimbabwe na kudai haki yetu. Ni nini leo kingeendelea?
Kombani amekalia shangingi ndilo analozunguka nalo wala hajui huku Uswahilini wananchi wanasema nini. Nilibahatika kukaa na Dk. Slaa baada ya mkutano wake wa kampeni pale Karatu. Tulikaa kwenye hoteli moja tukiwa tunazungumzia mchakato wa kampeni za uchaguzi.
Ingawa hatukukaa zaidi ya saa moja, lakini kwa muda huo tayari alishapokea simu nyingi na ujumbe mfupi wa simu kutoka kila pembe ya Tanzania kutoka kwa wafuasi wake. Nyingi zilitoka mkoani Mwanza kwa wafuasi wake na zilisisitiza:“Tumeshapigwa mabomu ya machozi, sasa tumeapa na tunakuambia tuko tayari kutoa damu yetu kwa ajili yako.”
Maneno kama haya ya Kombani wala Kikwete hawayajui. Hawajui kwamba vijana wengi waliochoshwa na utawala wa kina Kombani wako tayari kwa lolote liwalo. Hawa wangeambiwa na Dk. Slaa daini haki yenu, wangepambana na askari wenye bunduki kwa mapanga na marungu. Ingekuwaje?
Ndiyo maana wakati fulani nilimpongeza Dk. Slaa na CHADEMA kwa ustaarabu waliouonyesha wa kudai haki yao kwa njia za kiistaarabu kabisa. Kombani amka sasa na uwaamshe watawala wenzio waliolala. Mtakuja kuumia huko mbeleni.
Mtaugua presha na mnaweza kupoteza hata maisha baadhi yenu kwa uzembe wenu wa kutosoma alama za nyakati. Acha siasa za zamani zimepitwa na wakati. Nakumbuka mwaka jana wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, ulimhamisha ghafla Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu katikati ya mchakato wa uchaguzi.
Habari zikasambaa kwamba ulipata taarifa kutoka kwa vigogo wa chama chako kwamba hatawasaidia kushinda. Habari hizo ziwe ni za kweli ama uwongo hatua yako hiyo ilijaa utata. Na utakumbuka kwamba hata baada ya kuja huyo mpya uliyemleta bado chama chako kiligalagazwa vibaya katika uchaguzi ule.
Mwaka huu katikati ya kampeni za uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, ukiwa bado ni Waziri wa TAMISEMI ukamhamisha ghafla Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha. Habari zikavuma vile vile kwamba ni kwa sababu amekataa kukipendelea chama chako.
Ukaleta mpya, akaanza kwa makeke ya kumpiga faini mgombea ubunge kupitia CHADEMA Godbless Lema, lakini mwisho wa siku Lema alishinda ubunge na halmashauri iko mbioni kwenda CHADEMA. Hayo yakufunue macho kwamba umma ukifika mahali ukashikwa ‘mkia’ huwa kama paka niliyemwelezea huko nyuma. Mbinu za kimafia na tekniki alizopata kuzisema mzee Malecela hazitafua dafu.
Kama ulikuwa ukifuatilia televisheni jikumbushe umma wa wananchi uliosheheni nje ya geti za halmashauri katika maeneo mbalimbali ambako inasemekana mlitaka kuchakachua matokeo kama Arusha, Mwanza, na kwingineko. Tafakari, chukua hatua!
Kisingizio cha serikali kutokuwa na fedha hakiingii akilini. Watanzania wanaomba uwaeleze jambo moja tu: Kuandika Katiba mpya inahitaji shilingi bilioni ngapi na mabilioni yaliyopotezwa na serikali kupitia Dowans, Richmond , IPTL, Meremeta, Deep Green Finance, na ndugu zao wote ni mangapi?

Hivi unapozungumzia katiba unajua unachokizungumzia? Usicheze na roho ya taifa. Katiba ni roho ya taifa lolote duniani. Angalia nchi zote zilizoendelea huko kwa wenzetu ukatazame katiba zao zinavyowatiisha raia wote akiwemo rais ama mfalme ama malkia chini ya amri moja ya kuweka mbele maslahi ya taifa.
Kwenye nchi za wenzetu rais asingeamka tu asubuhi na kukutangaza wewe kuwa waziri wa wizara nyeti kiasi hicho bila kukupitisha bungeni, wabunge wakuchambue kama karanga, waulizie ulikotoka, waangalie CV yako, wachunguze umahiri wako katika mambo ya sheria, waone uadilifu wako na ujasiri wa kutetea maslahi ya taifa na kutekeleza Katiba ya nchi, na mambo mengi kama hayo. Vivyo hivyo kwa waziri wa fedha, mambo ya nje, ulinzi na usalama, ulinzi wa ndani na nyinginezo.

Katika nchi hizo rais hawezi kuteua mwanasheria mahiri mithili ya Samwel Sitta ama Dk. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Afrika Mashariki ama Naibu Waziri wa Ujenzi halafu akawaleta bungeni wapitishwe halafu hapo hapo mtu wa utawala wa umma awe waziri wa sheria na katiba. Katika nchi hizo rais hawezi kujipangia baraza la mawaziri anavyotaka. Kila siku kuna idadi ya mawaziri na manaibu wao. Mara 61, mara 47 mara 50.
Iko siku rais mmoja atalazimika kupoza makovu ya uchaguzi ndani ya CCM na kuteua mawaziri 80 kama si 90. Katiba ndiyo tiba ya yote haya. Ni katiba itakayotupatia mwongozo wa kuseti sera zetu za mambo ya nje, biashara za kimataifa, elimu, huduma za jamii na kadhalika, sera hizo zikabaki kuwa za kitaifa bila kujali anatawala CCM ama CHADEMA. Katiba ikifikia hapo itakuwa imetusaidia sana kuweka dira ya maendeleo na kutukimbiza wakati wengine wanatembea.
Nashauri tusikusikie tena Watanzania ukitueleza habari ya serikali na CCM hawataki Katiba mpya kwa kuwa nchi hii si ya serikali na CCM.
Na wanaodai katiba si CHADEMA tu, ni Watanzania wote wakiwemo wana CCM wa kawaida (achilia mbali ‘wenye’ chama). Tumewasikia majaji wastaafu, Jaji Mkuu aliyepo, rais mstaafu, viongozi wa dini, wasomi na wanazuoni mbalimbali, wanaharakati, na wengineo wengi; wote hao ni CHADEMA? Wote hao ni Tundu Lissu? Pole waziri wangu, umeshindwa kazi kabla ya kuanza!

h.sep3.gif

Nitumie ujumbe kwenye: smwigamba@yahoo.com au 0713953761 au 0767953761
 
Ngoma Ngumu:

Mimi ni mmoja wa watu wanaotaka mabadiliko ya katiba. Lakini mabadiliko ya hayo yanaweza kufikiwa kwa kufanya amendment ya katiba ya sasa. Hivyo anachosema Mzee Mwinyi kina ukweli na usahihi wake.

Lipumba anadai katiba mpya. Lakini wakati huo huo anao wabunge katika bunge la JMT ambalo wangeweza kutoa hoja ya kubadilisha baadhi ya vipengere. Kwa miaka mingi wabunge hao wamekaa kimya.

mkuu hapo kwenye red.

Jaji Kisanga (kumbuka mapendekezo ya tume ya jaji Kisanga) amesema hivi..." Katiba ya sasa ni shati lenye viraka vingi na haliwezi kumwenea mvaaji tena".

My Question: Kiraka kipi kitolewe kwenye katiba, na kiwekwe kiraka kipi? kwa nini lisinunuliwe shati jingine?
 
16th December 2010

MY TAKE:
Mwinyi knows the new constitution will work against his master plan to have his son vie for presidential post come 2015. Also the madudus that he did re Loliondo, IPTL etc will be in jeopardy.
Tumpuuze.....

Alichogusia Nyumbu (bold/underlined) ndiyo ukweli.
Niliwahi kuambiwa hizi habari na 'reliable source' nikayapuuza.. japo mtu aliyeyasema, kwa nafasi yake, is someone I should relly on over 95%!!
Kwa huu msimamo wa huyu mzee..naona amepanick ghafla!
When I flash back and connect the dots, certainly something underground (really a serious one) is going on entirely for the benefits of the lineage..
 
ndiyo mammbo madogo yenyewe hayo ninayosema.

yaani dar kuwa pwani basi wazaramo wamebweteka hata kujenga nyumba za maana hawawezi. shule hawataki.

wanafurahia kunywa kahawa chini ya maghorofa ya wahindi.

mtoto ana miaka mitatu anasoma 'chuo'.

watu wa pwani kweli akili zenu na za mbayuwayu sawasawa.

Acha matusi hapa. Wewe huko kwenu umejenga? Katika Tanzania mtu anayejisu kuwa kajenga kwao ni Mchagga, Mhaya na Mnyakyusa. Wengine hamna tofauti.

Thread ni kuhusu mawazo ya Mzee Mwinyi. Na mzee yupo sahihi. Katiba ni historical documents. Kwa nchi kama Tanzania ambayo ina amani na utawala wa kiraia toka uhuru kinachotakiwa ni mabadiliko ya vipengere vya katiba (amendments) na sio katiba mpya.
 
Labda Mzee Mwinyi anataka katiba mpya ije the Kenya au Zimbabwe way!!!
 
Huyu Mwinyi siyo uzee, ndivyo alivyo tangu zamani. Kwani U-Rais wake ulileta nini kipya.

Ndo maana alitwangwa makofi uzeeni. Natamani angepewa makofi mengine.
 
mkuu hapo kwenye red.

Jaji Kisanga (kumbuka mapendekezo ya tume ya jaji Kisanga) amesema hivi..." Katiba ya sasa ni shati lenye viraka vingi na haliwezi kumwenea mvaaji tena".

My Question: Kiraka kipi kitolewe kwenye katiba, na kiwekwe kiraka kipi? kwa nini lisinunuliwe shati jingine?

Hili tuweze kutathmini viraka hivyo kuwa ni vingi naomba naomba orodha ya viraka 20 tu kabla ya kuendelea kuchangia hoja yako.
 
Mwinyi kwa maneno yake mwenyewe alisema yeye ni kichuguu au sasa kishajiona ni mlima???
 
Msome huyo bwana hapo chinindiyo utapata picha kidogo.

Hili tuweze kutathmini viraka hivyo kuwa ni vingi naomba naomba orodha ya viraka 20 tu kabla ya kuendelea kuchangia hoja yako.

Msome huyo bwana hapo chinindiyo utapata picha kidogo.

Waziri Kombani, ameshindwa kabla hajaanza

Samson Mwigamba

amka2.gif
NIMEKUWA nikijitahidi sana kutoa ushauri kwa watawala (si viongozi) wa nchi hii kutokana na kile ninachokiona huko mbeleni. Ushauri wangu wa bure ni kwa manufaa yao na taifa pia.
Nina wasiwasi kwamba huko tuendako taifa litalazimika kuongeza maradufu bajeti ya mahakama ili kuhimili kesi nyingi za ubadhirifu wa mali ya umma, matumizi mabaya ya madaraka, kuwa chanzo cha uvunjikaji wa amani ya nchi, kuiingiza nchi kwenye machafuko, kushiriki ama kusababisha mauaji ya halaiki, uhujumu uchumi, na kadhalika.
Kwa manufaa ya taifa na kwa manufaa ya watawala binafsi nawasihi wasome alama za nyakati na kubadilika. Nakuwa na wasiwasi na ongezeko la wagonjwa wa shinikizo la damu litakalotokea siku watawala walioko madarakani watakapopoteza madaraka.
Ugonjwa ni ugonjwa, hakuna anayependa ugonjwa na matokeo ya ugonjwa yako katikati ya kupona ama kifo. Nawasihi Celina Kombani na vigogo wenzake wote walioko madarakani wanisikilize japo kwa taabu sana na kuyatafakari maneno yangu.
Nawatakia mema, nawatakia kustaafu kwema baadaye ili wale pensheni yao kwa raha ile ile ya mzee Nyerere na mzee Mwinyi. Sitaki wapate shida wala kuipatisha shida serikali ijayo kila wiki kuwe na kiongozi mstaafu anayekwenda kutibiwa nje ya nchi.
Na mimi si mnajimu lakini nashawishika kwamba serikali ijayo baada ya kuanguka kwa ‘watawala' wetu yaweza kuwa serikali ya wabana matumizi ya serikali kwa hiyo ikaweka hata masharti magumu kwa kiongozi kutibiwa nje ya nchi.

Celina Kombani, Waziri wa Sheria na Katiba, ni miongoni mwa viongozi ambao miaka michache ijayo wanaweza kuugua shinikizo la damu kwa kutoamini kilichotokea. Nasema hivyo kwa sababu ya matamshi aliyoyatoa hivi karibuni kwenye vyombo vya habari.
Waziri Kombani kwanza alisema hakuna haja ya Katiba Mpya eti iliyopo inatosha isipokuwa kama kuna watu wanalalamikia maeneo fulani fulani ya Katiba hiyo basi wapeleke malalamiko yao mezani kwake ili Katiba ifanyiwe marekebisho.
Akaenda mbali zaidi aliposema eti madai ya katiba si ya serikali wala Chama cha Mapinduzi wala wananchi wa taifa hili. Eti madai ya katiba mpya ni ya akina Tundu Lissu na CHADEMA. Akahitimisha kwa kusema serikali haina pesa za kuandika Katiba mpya.
Tatizo la hawa watawala ni kufikiri na kutenda kama Laurent Gbagbo wa Ivory Coast. Siku zote watawala wenye chama kinachoitwa cha mapinduzi wanafikiria mambo matatu makubwa. Kwanza wanafikiria kushinda na kushika dola. Kwao bila kushika dola hakuna CCM na hivyo CCM ni dola na dola ni CCM.
Ndiyo maana hata kauli mbiu zao za uchaguzi zaweza kuwa za aina ile ya "Ushindi ni Lazima". Pili hufikiria kwamba lolote lenye maslahi na chama chao (maslahi yana maana kukisaidia CCM kubaki madarakani), lazima kienziwe jua liwake ama mvua inyeshe, wananchi watake ama wasitake, kiwe kina maslahi kwa taifa ama hakina maslahi kwa taifa.
Ni kwa sababu hiyo, katiba mbovu, tume nyonge ya uchaguzi, mfumo mbovu wa utawala, na mengineyo watayang'ang'ania hata kama taifa zima linalia. Mwisho siku zote CCM wanafikiri Watanzania ni majuha, wajinga na wasioelewa mambo ya uraia hivyo unaweza kuwapeleka utakavyo.
Nampa pole sana Waziri Kombani. Kwani amelewa mvinyo huo wa chama chake na wala hahitaji kujipa muda wa kufungua masikio asikilize kilio cha Watanzania. Na kilio kisitafsiriwe kama unyonge usio na mwisho.
Paka ni mnyama mpole sana anayeishi na mwanadamu kirafiki mno. Lakini jaribu kumkamata paka halafu ushike ule mkia wake uwe kama unauvunja halafu atafute chance uone atakavyokung'ata na meno na kukujeruhi vibaya. Namshauri Waziri Kombani ajiangalie upya na kuuangalia upya umma wa Watanzania anaowazungumzia.
Anaweza kudhani ni paka marafiki kumbe wameshashikwa mkia na wanatafuta upenyo wa kujinasua na watakapoamua kucharuka si Kombani wala rais wake watakaokuwa salama.
Hoja za Kombani zote ni za ‘kizushi'. Lengo lake kubwa ni kulinda maslahi ya CCM kwa sababu anajua Katiba Mpya ikiandikwa utawala wa kijanja kijanja wa CCM utakuwa hatarini. Anajua kama mwenyekiti wake taifa anavyojua na viongozi wote wakuu wa chama chao wanavyojua kwamba CCM haina mvuto tena kwa wananchi bali inaendelea kuwa madarakani kwa ‘uchakachuaji' unaowezeshwa na ubovu wa katiba na ubovu mkubwa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Anasemaje kwamba taifa halihitaji katiba mpya wakati akijua kwamba mabadiliko ya katiba ya Zanzibar tu yameiathiri Katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa kiwango ambacho haifai tena kuwekewa viraka. Na hapo sijazungumzia mabadiliko ya kisiasa na kijamii achilia mbali suala la wakati linalotusukuma kuwa na katiba mpya.

Katiba ya Jamhuri imefanyiwa mabadiliko karibu mara 15 na sasa Kombani anadai mabadiliko mengine. Wakati wa kuingia vyama vingi Katiba ibara mbili za katiba yetu (namba 80 na 82) zilifutwa na leo Katiba ina kilema maana ukiisoma ukifika kwenye hizo ibara imeandikwa tu 80. (Imefutwa na sheria namba 4 ya mwaka 1992). Vivyo hivyo kwa ibara namba 82.
Leo Kombani anataka ibara ya kwanza tu ya Katiba iandikwe 1.(Imefutwa 2010 na mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ). Ibara ya pili hivyo hivyo. Sasa ni Katiba ya nchi gani ambayo unaifungua tu unakuta ibara ya kwanza na ya pili hazipo eti zimefanyiwa marekebisho. Ibara ya kwanza inasema: " Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano" lakini Katiba ya Zanzibar kwa sasa inasomeka: "Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Viraka vitaendelea mpaka ibara ya pili kubadilisha maneno yanayodai kwamba rais wa jamhuri atagawa Zanzibar kwenye mikoa baada ya kushauriana na rais wa Zanzibar kwa kuwa katiba ya Zanzibar sasa inamruhusu rais wa Zanzibar kuigawa ‘nchi' yake kwenye mikoa bila kushauriana na rais wa jamhuri. Bado hatujazungumzia kwenye ibara hiyo hiyo kuondoka kwa maneno " Tanzania ni nchi ya kijamaa ya vyama vingi" wakati kiuhalisia nchi haiendeshwi kijamaa bali kibepari tena kwa kufuata soko ‘holela' wala hata si soko huria. Tutalazimika kubadilisha aidha ibara ya 41 inayotamka: "Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi.

"Hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake".
Ama tubadilishe ibara ya 107A inayotamka: "Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki." Kasoro nyingine kubwa ya Katiba ni ile inayoihusu Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inazungumziwa na ibara ya 116 hadi 123. Mahakama hiyo sasa haitambuliwi na Katiba ya Zanzibar.
Mimi si mwanasheria, naweza kukiri kwamba ni mbumbumbu wa sheria kama alivyo Waziri wangu wa Sheria na Katiba Celina Kombani. Pengine waziri wa sheria angekuwa mwanasheria mahiri kama Samwel Sitta ama Harrison Mwakyembe asingetoa kauli ya namna hii.
Mimi ni mtaalam masuala ya uhasibu niliyosomea Chuo Kikuu cha Arusha labda na masuala ya uhandisi ambayo niliyasomea kwenye Taasisi ya Teknolojia ya Dar es salaam. Waziri wangu Kombani ni mtalaam wa masuala ya utawala wa umma (Public Administration) kutoka Chuo cha Mzumbe. Na kimsingi hatuna tofauti kwenye Katiba maana hata yeye anajua kwamba Katiba ina matatizo na ni kikwazo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi, utawala na demokrasia katika nchi yetu.
Tofauti na yeye ni kwamba yeye anajali zaidi maslahi ya watawala wakati mimi naangalia maslahi ya umma mzima wa Tanzania.
Hapa nimegusia tu mambo machache yanayoonyesha matatizo makubwa ndani ya katiba yetu. Sijagusia masuala mengine kama madaraka makubwa ya rais, mgawanyo makini wa madaraka kati ya mihimili mitatu ya dola, na mengineyo mengi.

Nina uhakika kwamba wanasheria wameshaanza na wataendelea kuichambua katiba yetu kama karanga na kutuonyesha kasoro nyingi ambazo zisipofanyiwa kazi sasa huko tuendako inaweza kuleta kasheshe kubwa. Chukulia mfano mdogo tu wa namna mgombea wa upinzani kupitia CHADEMA Dk. Willbrod Slaa alivyojizolea wafuasi nchi nzima halafu mwisho wa uchaguzi akaeleza wazi wazi tena kwa vielelezo kwamba kura zake zimeibiwa na kupewa mgombea aliyetangazwa mshindi na tume ya uchaguzi. Nini kingetokea kama angeamua kuwatangazia wafuasi wake kwamba hakubaliani na matokeo na kwa kuwa katiba haimpi nafasi ya kwenda mahakamani basi tuandamane kama Kenya ama Zimbabwe na kudai haki yetu. Ni nini leo kingeendelea?
Kombani amekalia shangingi ndilo analozunguka nalo wala hajui huku Uswahilini wananchi wanasema nini. Nilibahatika kukaa na Dk. Slaa baada ya mkutano wake wa kampeni pale Karatu. Tulikaa kwenye hoteli moja tukiwa tunazungumzia mchakato wa kampeni za uchaguzi.
Ingawa hatukukaa zaidi ya saa moja, lakini kwa muda huo tayari alishapokea simu nyingi na ujumbe mfupi wa simu kutoka kila pembe ya Tanzania kutoka kwa wafuasi wake. Nyingi zilitoka mkoani Mwanza kwa wafuasi wake na zilisisitiza:"Tumeshapigwa mabomu ya machozi, sasa tumeapa na tunakuambia tuko tayari kutoa damu yetu kwa ajili yako."
Maneno kama haya ya Kombani wala Kikwete hawayajui. Hawajui kwamba vijana wengi waliochoshwa na utawala wa kina Kombani wako tayari kwa lolote liwalo. Hawa wangeambiwa na Dk. Slaa daini haki yenu, wangepambana na askari wenye bunduki kwa mapanga na marungu. Ingekuwaje?
Ndiyo maana wakati fulani nilimpongeza Dk. Slaa na CHADEMA kwa ustaarabu waliouonyesha wa kudai haki yao kwa njia za kiistaarabu kabisa. Kombani amka sasa na uwaamshe watawala wenzio waliolala. Mtakuja kuumia huko mbeleni.
Mtaugua presha na mnaweza kupoteza hata maisha baadhi yenu kwa uzembe wenu wa kutosoma alama za nyakati. Acha siasa za zamani zimepitwa na wakati. Nakumbuka mwaka jana wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji, ulimhamisha ghafla Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu katikati ya mchakato wa uchaguzi.
Habari zikasambaa kwamba ulipata taarifa kutoka kwa vigogo wa chama chako kwamba hatawasaidia kushinda. Habari hizo ziwe ni za kweli ama uwongo hatua yako hiyo ilijaa utata. Na utakumbuka kwamba hata baada ya kuja huyo mpya uliyemleta bado chama chako kiligalagazwa vibaya katika uchaguzi ule.
Mwaka huu katikati ya kampeni za uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani, ukiwa bado ni Waziri wa TAMISEMI ukamhamisha ghafla Mkurugenzi wa Manispaa ya Arusha. Habari zikavuma vile vile kwamba ni kwa sababu amekataa kukipendelea chama chako.
Ukaleta mpya, akaanza kwa makeke ya kumpiga faini mgombea ubunge kupitia CHADEMA Godbless Lema, lakini mwisho wa siku Lema alishinda ubunge na halmashauri iko mbioni kwenda CHADEMA. Hayo yakufunue macho kwamba umma ukifika mahali ukashikwa ‘mkia' huwa kama paka niliyemwelezea huko nyuma. Mbinu za kimafia na tekniki alizopata kuzisema mzee Malecela hazitafua dafu.
Kama ulikuwa ukifuatilia televisheni jikumbushe umma wa wananchi uliosheheni nje ya geti za halmashauri katika maeneo mbalimbali ambako inasemekana mlitaka kuchakachua matokeo kama Arusha, Mwanza, na kwingineko. Tafakari, chukua hatua!
Kisingizio cha serikali kutokuwa na fedha hakiingii akilini. Watanzania wanaomba uwaeleze jambo moja tu: Kuandika Katiba mpya inahitaji shilingi bilioni ngapi na mabilioni yaliyopotezwa na serikali kupitia Dowans, Richmond , IPTL, Meremeta, Deep Green Finance, na ndugu zao wote ni mangapi?

Hivi unapozungumzia katiba unajua unachokizungumzia? Usicheze na roho ya taifa. Katiba ni roho ya taifa lolote duniani. Angalia nchi zote zilizoendelea huko kwa wenzetu ukatazame katiba zao zinavyowatiisha raia wote akiwemo rais ama mfalme ama malkia chini ya amri moja ya kuweka mbele maslahi ya taifa.
Kwenye nchi za wenzetu rais asingeamka tu asubuhi na kukutangaza wewe kuwa waziri wa wizara nyeti kiasi hicho bila kukupitisha bungeni, wabunge wakuchambue kama karanga, waulizie ulikotoka, waangalie CV yako, wachunguze umahiri wako katika mambo ya sheria, waone uadilifu wako na ujasiri wa kutetea maslahi ya taifa na kutekeleza Katiba ya nchi, na mambo mengi kama hayo. Vivyo hivyo kwa waziri wa fedha, mambo ya nje, ulinzi na usalama, ulinzi wa ndani na nyinginezo.

Katika nchi hizo rais hawezi kuteua mwanasheria mahiri mithili ya Samwel Sitta ama Dk. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Afrika Mashariki ama Naibu Waziri wa Ujenzi halafu akawaleta bungeni wapitishwe halafu hapo hapo mtu wa utawala wa umma awe waziri wa sheria na katiba. Katika nchi hizo rais hawezi kujipangia baraza la mawaziri anavyotaka. Kila siku kuna idadi ya mawaziri na manaibu wao. Mara 61, mara 47 mara 50.
Iko siku rais mmoja atalazimika kupoza makovu ya uchaguzi ndani ya CCM na kuteua mawaziri 80 kama si 90. Katiba ndiyo tiba ya yote haya. Ni katiba itakayotupatia mwongozo wa kuseti sera zetu za mambo ya nje, biashara za kimataifa, elimu, huduma za jamii na kadhalika, sera hizo zikabaki kuwa za kitaifa bila kujali anatawala CCM ama CHADEMA. Katiba ikifikia hapo itakuwa imetusaidia sana kuweka dira ya maendeleo na kutukimbiza wakati wengine wanatembea.
Nashauri tusikusikie tena Watanzania ukitueleza habari ya serikali na CCM hawataki Katiba mpya kwa kuwa nchi hii si ya serikali na CCM.
Na wanaodai katiba si CHADEMA tu, ni Watanzania wote wakiwemo wana CCM wa kawaida (achilia mbali ‘wenye' chama). Tumewasikia majaji wastaafu, Jaji Mkuu aliyepo, rais mstaafu, viongozi wa dini, wasomi na wanazuoni mbalimbali, wanaharakati, na wengineo wengi; wote hao ni CHADEMA? Wote hao ni Tundu Lissu? Pole waziri wangu, umeshindwa kazi kabla ya kuanza!

h.sep3.gif

Nitumie ujumbe kwenye: smwigamba@yahoo.com au 0713953761 au 0767953761
 
Msome huyo bwana hapo chinindiyo utapata picha kidogo.

Mr. Zero:

Nimesoma hicho kipande. Kudai katiba mpya bila kuelewa mapungufu ya katiba ya sasa ni ujinga uliokomaa. Katiba ni living document. Hivyo hata katiba mpya anayodai itabidi ifanyiwe amendments kwa sababu hakuna katiba itakayokuja na kuwa kamili.

Katiba sio Msahafu au Biblia. Hivyo kama kutakuwepo na mabadiliko kwenye katiba yoyote, kwanini basi mabadiliko hayo yasifanyike sasa.
 
Uongozi sio UFALME wa kuridhishana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mwinyi ndio timu ya uchakachuaji tangu lini atakubali katiba mpya wakati hii ya sasa inalinda uozo wanaoendelea nao wao pamoja na watoto wao wamegeuza nchi hii ya kisultani na kitumwa. Katiba ya sasa inawalinda wao na familia zao sasa unategemea mwinyi aseme nini jamani tuwe great thinker. Huyu mzee anajua maovu yake anaogopa kinga ikiondolewa atachapwa viboko. Wamezoea kutuona watanzania vibweka na mabwege na wavivu wa kufikiri. Ndio maana nasema wana jf kazi yetu kubwa iwe ni kusambaza ukweli kwa watanzania wote tuwape katiba ya sasa na kasoro zake na tuwe na rasimu ya katiba mpya.
 
Mr. Zero:

Nimesoma hicho kipande. Kudai katiba mpya bila kuelewa mapungufu ya katiba ya sasa ni ujinga uliokomaa. Katiba ni living document. Hivyo hata katiba mpya anayodai itabidi ifanyiwe amendments kwa sababu hakuna katiba itakayokuja na kuwa kamili.

Katiba sio Msahafu au Biblia. Hivyo kama kutakuwepo na mabadiliko kwenye katiba yoyote, kwanini basi mabadiliko hayo yasifanyike sasa.

Zakumi,

May be hujasoma hicho kipande vizuri maana kimezungumzia kwa kiasi mapungufu ya katiba. Pia jamaa anaonyesha mapungufu ya katiba toka kipengerecha kwanza.

Kwa vile umekubali kuwa katiba si msaafu au biblia hivyo inaweza kubadilishwa. Kwa nini sasa hukubali kuibadilisha yote badala yake unataka vipengele tu. Sasa labda na wewe ungetusaidia hivyo vipengere unavyofikiri vinapaswa kubadilishwa. Ingawa binafsi sijawahi kuipitia katiba lakini uchambuzi unaonekana kuwa katiba yetu ina contradiction nyingi na ina mapungufu mengi. Vilevile ni katiba ya mkoloni.
 
Back
Top Bottom