Project 2015: Mwinyi haoni uharaka wa Katiba Mpya

Mmh namheshimu sana mzee huyu. Ila nadhani anaishi kisiwani bila mawasiliano na nchi inaendaje kama hawezi kuona unuhimu wa katiba mpya na anshauri iwekewe viraka basi naomba nyamaze awaachie wananchi waseme watakalo
 
labda kubadili katiba kutaathiri kurithishana kwa uongozi wa ccm 2015, ndio maana mzee kaona tusubiri kidogo
 
Madai ya katiba ndio yaliyompa ulaji huyu Babu au kasahau pale 1984 hali ya hewa ilipochafuka Zanzibar?
 
It amazes me how far CCM will go regardless of citizens' right's of democracy to get level plain field constitution that looks out for the benefit of the peoples of the United Republic of Tanzania.

With similar zeal (ari), citizens, civil society, media, etc...have to push academically & professionally with resolve for katiba mpya.
 

Mzee wetu Mwinyi tunamheshimu lakini kwa swali lake, 'Why Now', inaonekana huyu mzee na wale wanaomwunga mkono wanakosa kitu muhimu sana katika fikra zao. Hawa hawana mawazo ya kimaendeleo. Ukiwa na mawazo kama hayo huwezi kubadilisha chochote katika maisha yako utabakia kama ulivyo milele. Maana kila wakati utajiuliza 'Why Now', the answer is more than obvious. Because there is a need. Matatizo yetu mengi mwanzo wake ni katiba. Viongozi wanatumia madaraka vibaya, ufisadi, matumizi makubwa ya serikali yasiyokuwa na tija, watoto wa maskini kukosa elimu, watu wa hali ya chini kukosa huduma bora kama matibabu, makazi, n.k; muundo na ukubwa wa serikali usio na tija, n.k. Hivi vyote mwanzo wake ni sheria Mama - Katiba. Unapokuwa na sheria yoyote, inachukua muda mpaka kuja kujua kuwa ina mapungufu fulani, na sasa tumegundua mapungufu makubwa ya katiba yetu.

Mdondoaji unauliza mapungufu ya katiba. Usiwe mvivu wa kusoma. Nenda katafute ripoti ya Jaji Nyalali na Jaji Kisanga. Mambo mengi yameorodheshwa mle. Wewe unayesema hujui mapungufu inawezekana hata kilichoandikwa kwenye katiba hujui pia. Kwa hiyo huna hoja wala hata haki ya kuchangia maana huwezi kuchangia usichokijua.

 
kwa hio ww unaona kuwa watu wa pwani ni watu wa mambo madogo ?


jiulize kwa nn mji mkuu wa tanzania uko pwani na sio bara ?


Duuu. na wewe umetoa mpya. yafaa kuwa thread. Sasa Mji mkuu si waliweka wakoloni? wazaramu na wakwere wako wapi zaidi ya kuwahi chalinze kwa kukosa ubavu wa kukaa mjini?
 
Hungelitegemea mzee wa watu aseme nini! kwake yeye katiba iliyoko ndiyo ilimsaidia kumwingiza madarakani, na ndiyo hivi sasa inamwezesha yeye na familia yake kuishi peponi wakati wengi wa watanzania wanateketea kwa mamilioni kutokana na ufukara wa kutupwa.
 
Kama ambavyo amewaacha wazenji wenzake wakaamua mambo yao wenyewe, yeye naye awaachie watanganyika waamue mambo yao bila kuwekewa vikwazo na wa zenji kama Mwinyi
 
Zakumi,
The hate of men will pass, and dictators die, and the power they took from the people will return to the people. And so long as men die, liberty will never perish Charlie Chaplin"
 
I am always against violence, na nilikuwa mmoja kati ya watu waliolaani kitendo cha mzee huyu kupigwa kofi na hasa nikiangalia umri wa mpigaji wa kofi na huyu mzee tena rais mstaafu, akili yangu ililaani sana.
Leo ninaweza kufunguka macho na kuona sababu hasa zilizomfanya huyo bwana ampige kofi baba huyu. Ni rahisi sana mtu kujikuta umekuwa violent kwa kuwa busara mara nyingine zinaishia watu wengine. Si kwa sababu ya uzee tu, bali kutokuwa na chembe ya busara.
Nina wasi wasi kuwa kama huyu ndiye rais aliyekuwa akiongoza nchi hii na ingawa ni demokrasia kila mtu kutoa mawazo, na haya ni sehemu ya mawazo yake, basi tulikuwa na matatizo makubwa sana. Nasema tulikuwa na rais bogus kabisa, na hasa kutokana na mawazo yake haya ambayo wengine wanasema ni huru lakini ni pumba.
Mungu ibariki Tanzania.
 

Inaonekana hata Cover la Katiba yenyewe hujaiona, potelea mbali maana wengi wa watanzania hawajaiona! Je hujawahi kusikia watu wanadai mgombea binafsi) (Haki ya mtu kuchaguliwa kiongozi bila kupitia vyama? Ukubwa wa mamlaka ya Rais ikiwemo tija ya uteuzi wa wabunge 10 wa viti maalumu! Kuhoji kisheria matokeo yaliyo tangazwa na tume ya uchaguzi? Kazi wa wakuu wa wilaya? nk nk.

Kwenye red nimeshindwa ku-comment kwa sababu hujatoa source wala hujasema walikuwa wanataka nini kibadilishwe ndani ya katiba hii mbofu mbofu! Nakumbuka miaka ile walichoma mabucha ya nguruwe Dar na Mwanza wali vunja mabanda ya nguruwe na kuwauwa huku damu za wanyama hao zikiwarukia kwenye kanzu zao lakini hawakuzivua wala kuzitupa!

Usitake kuhusisha hitaji la katiba mpya na masuala ya kidini kama mtu aliefilisika kifikra. Katiba mpya ni HITAJI la watanzania wenye kuipenda nchi yao yaani wazarendo wa kweli.
 
This brings me back to the point,Mkapa was Tz brilliant leader and reader of the times,because he ruled,he was the best among last 3phases of poor leaders. We need another Nyerere now,lets wait 2015!
 
Huyu mzee wetu tunamheshimu kwelikweli japo kipindi cha uongozi wake aliongoza kiutatautata, ila swala la yeye kutokuona umuhimu wa mabadiliko ya katiba hivi sasa labda ana maslahi yake binafsi na uongozi wa kanchi ketu siku zijazo kama alivyodokeza mchangiaji mmoja kuwa 2015 kijana wake anaweza kujitosa KUGOMBEA UFALME WA KUONGOZA KANCHI KETU NA KUENDELEA kumega neema YA TANGANYIKA
 
Anajua madhara ya katiba mpya!! Kwani ndiyo mwisho wa kupeanda madaraka na kusema ndiyo kwa kila kitu..
 

Mijitu mingine bwana utafikiri ndo kwanza inazinduka kutoka kwenye pipa la komoni, au ndo tuseme hujui kuwa mzee Mwinyi ana agenda yake mfukoni? Je unafahamu ya kuwa jaji Nyalali alianisha sheria 40 kandamizi ndani ya katiba yetu ambazo kwazo akitokea au ikitokea tukapata Rais mlevi hivi wa madaraka nchi hii haiwezikalika. Je unajua katiba yetu inatamka kabisa nchi yetu ni ya ujamaa na kujitegemea je huo ujamaa upo wapi? Acha ujuha wewe mwenye akili za kushikiwa.
 

hivi nyny wa bara mna katiba ? mm sikujua hilo kama mnayo fanyeni hayo mabadiliko myatakayo.

kuhusu katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania umakini unahitajika na ss wazanzibari tunayahitaji sana hayo mabadiliko au muandiko wa katiba mpya maana tuna mengi tu ya kuyataka yasiwemo kwenye hio katiba na hapo huenda mkawa na kazi mbili ndugu zetu, moja ni ya kuandika katiba ya muungano ambayo tutashirikiana na ile ya kuandika katiba ya Jamhuri ya tanganyika
 
Babu kaonja asali sasa anataka kuchonga MZINGA Ameuliza kwa msisitizo KWA NINI LEO nami namuuliza KWA NINI ISIWE LEO? AU iwe kama Kenya au Zenj? Ndipo wakati muafaka? Babu kucheza matida na watoto wadogo haipendezi watu wazima watakushangaa huyu mzee mwenzetu kwani vipi? Leo ndivo ilivyo watu wanakushangaa!! JEE N huyu huyu tuliokuwa tunamheshimu kwa kauli mbiu ya mzee RUKSA Leo kilicho mbadilisha ni NINI? kweli huyu babu haoni huu ni wakati Adhimu kupata katiba inayo kidhi haja ya haya mageuzi ya KISIASA KIJAMII NA KIUCHUMI? Au ana Ajenda nyingine Kama enayo ni haki yake tu Aibainishe kwenye mkutano wa katiba ili wenye nchi waijadili kama wataridhia itakuwemo kwenye katiba MPYA! lazima uelewe babu kuwa vurugu fujo na vita ni mwendelezo wa siasa ni pale matatizo ambayo hayakupatiwa ufumbuzi kisiasa basi fujo machafuko na vita hutokea ili ufumbuzi upatikane baina ya MATABAKA; INSHAALAH!!
 
mzee anavuta sana bangi... angalia macho yake... bangi za uchochoroni.... legalize marijuana ili aweze vuta hadharani
 

Why ammendments and not overhauling?
Kama unakubali ammendments, basi huna sababu ya kuogopa uandishi was katiba mpya.
Unapotosha umma ukidanganya kwamba unapenda mabadiliko , wakati ukweli ni kwamba wewe unafaidika na ubovu wa katiba iliyopo.
Hata Nyerere aliwashangaa akina Mwinyi kwa kuweka viraka kwenye katiba, wakati uwezo wa kubadilisha, nia na ulazima wa kufanya hivyo tunao.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…