Kama ni kutokuelewana mngeyamalizia huko huko KKKT kimya kimya,lakini kama kuna Washarika hadi wanabeba mabango wanamtaka Mchungaji wao huo ni Mtifuano tena mkubwa.Bado hujanielewa. Halafu hakuna mtifuano, ni kutokuelewana tu.
Yani kuna mpaka kwaya ya Kijitonyamaa ilirekodi nyimbo kali sanaaa enzi hizoo means Usharika upo vizuri toka kitambooo...!Acheni siasa kanisani. Nyie mmeijua KKKT Kijitonyama leo, mnalazimisha wengine wawa sikilize. KKKT Kijitonyama ilikiwa inajaa mpaka nje, kabla ya huyo Kimaro. Halafu Hilo jengo la kitega uchumi kalijenga Nani?. Usidharau ambachao kwa msala upitao. Kijitonyama ilikuwa maarufu enzi na enzi, huyu katumia umaarufu wa kijitonyama kujijengea jina.
Hawezi sia Mpinga kristo...Mnanishangaza sana.
Hata Yesu aliwasifu mafarisayo kwa kuwatolea mfano wanafunzi wake kuwa;
" Haki yenu isipozidi haki ya mafarisayo kamwe hamtauona ufalme wa Mungu"
Hapo kuwasifia waislanu katika eneo wanalofanya vizuri kuna tatizo?
Nimegundua Wakristo wengi ni zero katika ufahamu wa neno la Mungu.
Na ipo bado....Mseme, msiseme. Kila taasisi duniani ina taratibu na miongozo yake. Huyu mchungaji hakuondolewa kwa bahati mbaya. Kuna maneno amehubiri yasiyofaa kwa utaratibu wa kanisa lake.
Ni muhimu tujue kuwa mahubiri ya mihemiko wakati mwingine huwa hayatakiwi na kanisa kulingana na sera na taratibu zao.
Ile ni taasisi. KKKT. Ndio kaondoka. Anayetakanaondoke nae.
Kanisa Katoliki yanawakumba. Askofu Milingo wa Zambia wa Katoliki alianza hivyo akaondokewa akaishia kuanzisha kanisa lake.
Kila taasisi ina siri, mbinu, majukumu na kila kitu. Ukikengeuka unaondolewa tu.
Nani alijua Zito angetoka CHADEMA.
UZUSHI..Amepiga simu polisi kuomba usaidizi ili aweze kuanzisha ibada ya masifu ya asubuhi kesho asubuhi, anapiga piga simu ovyo kusumbua wazee wa watu kuulizia hali ilivyo baada ya kufanikiwa kutoroka kanisani
Wala hainishangazi kuna mmoja soon ataanza kupiga assalamualaikum....Kuna askofu mstaafu mmoja wa KKKT nilimsikia Redioni akisema huwa anasali nusu ya Sala ya Salamu Maria. Hii ilimtokea wakati anafanya PhD yake, profesa wake alimpa afanye review maandishi ya Martin Luther na Papa Benedict XVI kuhusu Maria. Alivyomaliza hiyo kazi akijua kumbe huko kote alikosoma alifundishwa vitu tofauti tu, hatimaye akaanza kusali hiyo salamu Maria.
Muumiini mmoja anaabudu akiwa kwenye mti na mwingine akiwa kwenye kivuli ndani ya jengo zuri, yupi mwenye uwezekano wa kukua kiroho kirahisi zaidi, assuming imani zao ziko sawa?Vuongozi wengi sana siku hizi pamoja na waumini wao wanaangalia zaidi ya kimwili kama miradi na uwekezaji na kusahau kujijenga na kukua kiroho
Mhimili Usioonekana Tayari Umeingia Hapo Ile Video Umeiona Na Kuisikia
Kama familia ni Taasisi kanisa linashindwaje kuwa Taasisi?Hii dhana ya ukubwa kuliko taasisi kwani kanisa ni mali ya mtu,au genge la watu?. Kanisa sio jengo, ni mwili wa Kristo ambapo watu wenye imani juu Kristo wanaamua ku team up na kumtafuta Mungu hata kwa kupapasa wakamwone sasa kuwa na kiongozi mwenye kuonyesha njia imekuwa nogwa?. Mwenye kanisa ni Mungu, mwenye roho za watu ni Mungu.
Sahihi Sana Hilo ,alijisahau Sana Hadi kuanza kuwasifu wakatoliki na waisalmu hadharani eti ,roma Catholic wako vzr so wat aende uko sasa
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kwenye hizi rules, naipenda sana rule namba 21!Kwenye kitabu cha 48 rules of power , rules ya kwanza inasema.NEVER OUTSHINE YOUR MASTER.
Kiutaratibu hapo alikosea. Huwez kuponda wanaokupa platform. Aonywe, kisha apelekwe huko umisioni Mwaneromango akajifunze zaidi**Sahihi Sana Hilo ,alijisahau Sana Hadi kuanza kuwasifu wakatoliki na waisalmu hadharani eti ,roma Catholic wako vzr so wat aende uko sasa
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kwa hiyo kama ni taasisi maovu kama yapo na yanainekana yanatakiwa yafunikwe na yasikemewe??Kama familia ni Taasisi kanisa linashindwaje kuwa Taasisi?
Unaelewa maana ya Taasisi au unatapika ujinga.
Inashangaza sana mtu kutengwa kisa kusifia binadamu wenzake kwa sababu tuu ya kutofautiana kiimani.Kuna shida gani akisema ivyo mkuu? Wakristo wote tunapenda na hatubaguani..... hata waislamu tunawapenda pia maana wao pia hawatubagui kuwasifia ni kosa? Mnaharibu sana kuweka matabaka.... mungu anatupenda wote
Tunafanya mkakati afungue kanisa lake pembeni ya KKKT kijitonyama palepale 🤐Tena chuki kubwa mnoo hapo wameshatafuta namna ya kumwangusha na hatokaa apate upenyo wa kuyafanya yale aliyoyafanya kijitonyama....labda aanzishe mwendo kivyake na si chini ya taasisi tena
Hivi kumbe ni project zake binafsi, mimi najua ni project za kanisa na zimejengwa kwa nguvu ya michango ya waumini na ni utaratibu wa makanisa yote ya KKKT hata hapa mbezi beach tuna similar projects na zinafadhiliwa na michango ya washarikaTujikumbushe, projects kadhaa ambazo Mchungaji Dkt. Kimaro amezifanya akiwa Mchungaji Kiongozi, KKKT Usharika wa Kijitonyama,
1. School of Healing (Morning & Evening Glory) -Youtube Channel (mwanzoni ikiwa Eliona Kimaro TV baadae KKKT Usharika wa Kijtonyama) inayowafikia watu wote Duniani.
2. TAMASHA LA MBINGU KUJAA SIFA (kila mwaka)
3. Jengo jipya la Sunday School (lililogharimu yapata takribani 200m TZS)
4. Ununuzi wa Kiwanja pembezoni mwa kanisa yapata 300m TZS
5. Kusomesha yatima yapata 100
6. World Pray Online (WPO), Call Centre ya maombi masaa 24, siku 7 za wiki.
NB: Ikumbukwe waliokuwa wanasali hizo Morning & Evening Glory wengi hawakuwa waumini wa KKKT bali wa madhehebu mengine na Waislam kuondoka kwake Dkt Kimaro tutarajie mabadiliko kiasi.
***Mchungaji Kiongozi (Mpya) Anna apewe ushirikiano kuendeleza alipoishia Dkt Kimaro.