Promota mnataka Mandonga afie ulingoni?

Promota mnataka Mandonga afie ulingoni?

Naona tangazo la mchezo wa ngumi, ([emoji3037])

Kati ya Karim Mandonga na Golola Moses kutoka pale Kampala Uganda, tarehe 29 mwezi huu wa July, Kwa kifupi promota anayeandaa hili pambano pamoja na Mandonga mwenyewe aliyekubali hili pambano ni kwamba hawana akili.

Golola Moses ni bondia mkubwa sana pale Uganda japo alianzia kwenye Kik boxer, hata Dulla Mbabe hawezi kumpiga Golola, wajaribu kupitia upya wasifu wa Golola.

Mandonga usipokataa pambano hili ndo unaenda kuwa mwisho wako kucheza tena jukwaani

View attachment 2692468View attachment 2692469
Mwache akapasuliwe anapenda sifa za kijinga sana
 
Tatizo mechii hii tuna hofia uhai wake [emoji3][emoji3][emoji3]hatuko tayar kumpoteza mandoga maana hatujawai kua na mpiganaji kama yeye tz [emoji23][emoji23]
Trust me Mandonga anashinda hili pambano. Either Kwa kununua mechi, kubebwa na majaji au hata labda Golola wa Sasa ni dhaifu kuliko huyo wa enzi hizo.
 
Kule Kigoma , mtu ukiwa na Sura mbaya huwa tunadhan unajua ngumi
 
Mandonga kila dakika 1 anakumbatia.
Kama mwamba ndo anapigana naye ,Basi Karim ajiandae kuyakanyaga
 
Naona tangazo la mchezo wa ngumi, ([emoji3037])

Kati ya Karim Mandonga na Golola Moses kutoka pale Kampala Uganda, tarehe 29 mwezi huu wa July, Kwa kifupi promota anayeandaa hili pambano pamoja na Mandonga mwenyewe aliyekubali hili pambano ni kwamba hawana akili.

Golola Moses ni bondia mkubwa sana pale Uganda japo alianzia kwenye Kik boxer, hata Dulla Mbabe hawezi kumpiga Golola, wajaribu kupitia upya wasifu wa Golola.

Mandonga usipokataa pambano hili ndo unaenda kuwa mwisho wako kucheza tena jukwaani

View attachment 2692468View attachment 2692469
Huyu ni mtu kazi nionavyo mimi
 
Mandonga wewe Mandonga karimu Mandonga Leo umepigika sana yaana umechapwa hapo Kenya na wanyonyi nakuomba tena pambano la tarehe 29 na Golola usipigane nakuomba sana
20230723_135820.jpg
 
Mandonga umeshapata pesa SI haba fanya mambo mengine utakuja fia ulingoni ama upate hitilafu ya ubongo Jana umechezea kichapo heavy na tarehe 29 unataka ukapigane tena?
 
anaitwa Umar Semata, ndie aliemchapa Golola, wala msipagawe na hilo body la Golola

View attachment 2692486

kuna utofauti mkubwa wa kujaza body kwa vyuma ama sindano na kupigana.

Hata gari likiwa kubwa sana dereva mzoefu analipiga rivazi.

Mandonga asishindane na huyu bondia kwenye nguvu, amkabili kwa speed, akili, uzoefu, n.k.
Sasa Mandoga hizo akili na speed za ngumi anazo?
 
Back
Top Bottom