Proof: Binadamu alitengenezwa na Aliens


Nimekujibu: kwasababu hayupo

Lakini bado hujaridhishwa na unalazimisha nikupe sababu nyengine..Tena kwa mifano.!

Najibu tena: hayupo kwasababu kafa_ unaonaje.?
 
Nimekujibu: kwasababu hayupo
Hii siyo sababu, hili ni tokeo, sababu ni ile iliyofanya useme hayupo. Kwahiyo ndiyo utuambie hiyo sababu ni ipi.
Lakini bado hujaridhishwa na unalazimisha nikupe sababu nyengine..Tena kwa mifano.!
Nimekupa mfano mwepesi sana, lakini una poteza muda. Haya mambo hamuyawezi, achaneni nayo.

Mfano gani umeutoa katika hili ? Mfano nimeutoa mimi mzee.
Najibu tena: hayupo kwasababu kafa_ unaonaje.?
Usiniulize nauonaje,hapa tuna taka ukweli, labda kama kwako ukweli hauna nafasi na huuzingatii.

Safi, kama uko serious, lazima ujibu swali hili au hoja hii "Thibitisha kama kafa na kipi kimekujulisha kafa ?"
 
Safi, kama uko serious, lazima ujibu swali hili au hoja hii "Thibitisha kama kafa na kipi kimekujulisha kafa ?"
Kilichonijulisha kuwa kafa ni kwasababu hayupo

Na uthibitisho ni wewe kushindwa kithibitisha kuwa yupo
 
Kilichonijulisha kuwa kafa ni kwasababu hayupo

Na uthibitisho ni wewe kushindwa kithibitisha kuwa yupo
Hauko "serious" nikajua utakuwa unajua sababu ya kukana kwako, naona unarudia rudia kukosea.

Sijawahi kushindwa kuthibitisha uwepo wa Mola muumba, na sitoshindwa kufanya hivyo, ila wewe na wakubwa zako hamjawahi kuthibitisha ya kuwa Mola hayupo wala hamtoweza kufanya hivyo, zaidi ya kucheza na maneno bila kuzingatia maana na uhalisia.

Ukija na sababu ya umejuaje kwamba Mola hayupo, na ukija na ithibati ya kuwa Mola kafa. Unistue nikuwekee ushahidi wa kuwa Mola yupo.

Nyinyi inabidi tuwafundishe namna ya kufikiri kwa usahihi, unaposema Mola wetu kafa,ina maana alikuwepo, swali la msingi ni kuwa umejuaje kafa na kipi kilifanya akafa ?

Dondoo ya uwepo wa Mola tunaipata katika vifuatavyo :

1. Self-Evident Truth (Bayyinah)
2. Contingent Facts

Na nyingine nyingi. Nimekuwekea dondoo tu kukuonyesha ya kuwa suala la mimi kuthibitisha ya kuwa Mola yupo ni suala la dakika chache sana.
 
Mungu inawezekana akawepo au asiwepo pia. Hapo ni suala la mtu kusadiki na kuamini tu,sio suala la kujua.
Kadhalika Aliens wanaweza wawepo au wasiwepo.
Lakini suala la uwezo wa binadamu kiakili hili lipo wazi,na SIAMINI kama aliens wanatusaidia katika technology, hayo makubwa ni matokeo ya akili kubwa za wanadamu wachache, kisha wengine tunanufaika
 
Nafikiri hivi pia.
 
Thibitisha hili.
JIBU sahihi kama Mungu yupo au hayupo ni SIJUI.
MUNGU HAYUPO
i)Haijawezekana kuthibitisha bila chembe ya shaka kwa mamia na maelfu ya miaka mpaka sasa,hali inayosababisha watu kuegemea katika "historia" za inasemekana zilizopo katika vitabu mbalimbali.Hali hii huwa inafanya suala hili liwe la mtu binafsi.
ii)Hathibitishi uwepo wake mwenyewe pasipo kusemekana katumia mwanadamu,hali inayoleta mkanganyiko mpaka leo kama hao waliotumika kweli walipata ridhaa kutoka kwa Mungu,au walikuwa na akili nyingi na lengo la kuifanya jamii iwe bora. Yani leo hata tukionana nikakwambia wasiliana na Mungu hata atupe njozi moja ndani ya wakati mmoja ili tuweze kuelezana uthibitisho wake, na zoezi hilo hata basi lifanyike kwa dunia nzima UTAKWAMA.
iii)Yanayowakuta wanaoamini na wasioamini katika maisha ni yaleyale yani shida na raha n.k hakuna exclusive na kukosekana kwa hiyo "exclusive" watu hujificha katika mwamvuli wa MIPANGO YA MUNGU,mathalan kuna viongozi wa imani ambao husema walifunga na kumwombea mtu aponywe gonjwa fulani na akapona lakini unakuta wao walikufa kwa kisukari,cancer e.t.c au utakuta kuna sala mtu anawekewa ataje mara idadi ngumu ya kibinadamu labda mara mia au maelfu na anafuatisha na mwisho anaweza kuambiwa asubiri "mipango ya mungu" au hakuwa na "imaan".
Labda nikuachie swali na wewe, je kwa nini linapokuja suala la Mungu uthibitisho wake umekuwa unategemea kudhihirishwa kupitia binadamu tena mmoja mmoja ambae anakuwa kaitwa "spesheli"?Je hakuna namna Mungu anaweza jidhihirisha mwenyewe kwa wakati mmoja kwa ulimwengu mzima?Kuliko hii ya alizaliwa Saudi Arabia,alizaliwa Israel,alitokea India n.k?
 
Thibitisha hili.
Nikirudi upande wa MUNGU YUPO,hapa nitaenda kirahisi tu, hakujatokea mwanadamu akaenda kinyume na kinachoitwa natural orders,hususan zama hizi.Sasa hapo katika natural orders kama tunasema kuna mwanzo, na mwanzilishi basi INAWEZEKANA aliyeziweka ndio MUNGU.
NB:Mimi bado namtafuta Mungu, lakini katika mipango ya duniani ili niishi bila bugudha na nipate "hali ya kujiskia kama sehemu ya jamii na mwanajamii" huwa najumuika maeneo ya imani.Suala hili huliacha liwe binafsi.
 
JIBU sahihi kama Mungu yupo au hayupo ni SIJUI.
Kielimu na kufata adabu zake, jubu lako la "SIJUI" lilitosha kabisa kukufanya wewe usijadili kuhusu uwepo wa Mola kwa njia yoyote ile zaidi ya kuuliza maswali ujibiwe.
i)Haijawezekana kuthibitisha bila chembe ya shaka kwa mamia na maelfu ya miaka mpaka sasa,hali inayosababisha watu kuegemea katika "historia" za inasemekana zilizopo katika vitabu mbalimbali.Hali hii huwa inafanya suala hili liwe la mtu binafsi.
Hapa nimecheka sana, ipi nafasi ya Historia katika kuupata ukweli ? Jibu rahisi sana, huwezi kurejea ya nyuma bila kurejea historia.

Pili, hizo "Historia za inasemekana" umezipata wapi huku kwetu sijaziona labda hizi mnazo nyinyi mnao mkana Mola pasi kumjua.

Tatu, haijawezekana kuthibitishwa kwa nani ?
 
Kama unakubali kabisa ya kuwa dunia ipo katika utaratibu na nidhamu, yaani kuna usiku na mchana, kitu kikirushwa kwenda juu lazima kurudi chini, jua linazama magharibi na kuchomoza mashariki, huu ni utaratibu wake kama alivyoweka utaratibu wa kufikisha ujumbe kwa waja, aliweka utaratibu wa kuwachagua waja fulani miongoni mwa waja wake kisha anawapa ujumbe.

Watu walio kuwa wanatumwa walikuwa wanapewa mambo kwayo hakuna mwanadamu anaweza kuyafanya lwa hali yoyote ile, na ilikuwa hivyo ili kuwashawishi waweze kuukubali ujumbe husika.

Unapotaka mimi leo hii niwasiliane na Mola kwa mtindo unao taka, unao nyesha ya kuwa humjui Mola, sababu taratibu haziko hivyo unavyotaka wewe. Mola alivyo tuumba hakutuacha hivi hivi, aliweka ishara za kumtambua yeye kwa kila kiumbe, ndiyo maana anapotokea mty kumkana ujue anaenda kinyume na asili na silika.
 
Maswali gani haya sasa, haijaweza kuthibishwa na nani? Kwa hapa kwetu au watu wa mazingira yetu Tanzania ni Waislamu na Wakristo!
Halafu umeshaniweka katika kundi la wasiokubali kama Mungu yupo😂😂.Mi nimesema SIJUI ila najumuika sehemu mainly for "social benefits" kama vile kuwa sehemu ya jamii, na mipango mingine ya kurahisisha maisha.Pamoja na kujifunza huenda kuna siku nikajidhihirishia uwepo wake bila chembe ya shaka.
Lakini wewe unataka kuleta UONGO WA KUJUA UKWELI HALISI
 
Kweli humjui Mola ajabu unamjadili hili tatizo ni la kutomua Mola. Katika taratibu za Mola akileta msiba au majanga huwakuta wahusika na waiso husika, kisha hesabu na kulipwa stahiki siku ya malipo, huu ndiyo utaratibu alio uweka.
Umeuliza swali la kitoto sana, uthibitisho wa Mola upo kwa kile mtu, hasa ambaye akili yake na imani take haijachafuliwa na fikra za ukana Mungu na upotoshaji na imani potofu.

Leo hii ukienda kwa mtu yoyote ambaye hajafikiwa na imani yoyote ukimuuliza juu ya uwepo wa Mola hakanushi hilo. Yaani kila mwanadamu ameumbwa na haki ya kukubali uwepo wa Mola isipokuwa tu watu wamechafuliwa fikra zao.

Kadhalika tuna weza kujua uwepo wa Mola muumba kwa kutumia akili, milango ya fahamu, mazingira ba maumbile na ufunuo. Hivi vyote vinathibitisha uwepi wake.

Ushauri wangu ni kuwa, kamwe usije kukanusha jambo ambalo huna elimu nalo, hili ni kosa kubwa sana.
 
Halafu umeshaniweka katika kundi la wasiokubali kama Mungu yupo😂😂.
Naanzia hapa, nimekujibu vile kwa kile ulichokiandika mzee. Kwahiyo wewe jibu hoja.
Lakini wewe unataka kuleta UONGO WA KUJUA UKWELI
Ukweli halisi uko wazi ni kuuchukua tu. Allah katika Qur'aan anawapa changamoto watu wanao mkana ya kuwa wajibu maswali haya :

1. Je wao wametokana pasi na chochote au ?
2. Wao wamejiumba ?

Sasa akili timamu na ikiyo salama haikatai uwepo wa Mola, ukiona una kana tu ujue akili yako haiko salama yaani una matatizo ya kujitakia.
Maswali gani haya sasa, haijaweza kuthibishwa na nani? Kwa hapa kwetu au watu wa mazingira yetu Tanzania ni Waislamu na Wakristo!
Rejea ulichokiandika.
 
Sijafanya hilo kosa kubwa, tangu mwanzo nimesema anaweza kuwepo na asiwepo pia☺☺.
Swali la kitoto hilo..?!Hii unafanya mashambulizi mabovu.Mbona kule nilipothibitisha yupo hauongelei.Mkuu kwa maneno machache nakuelezea wewe kuwa ni mtu ambae
"Mungu HAUMJUI ila IMANI unayo pangine THABITI kabisa"
Haya tuache yaendelee ya ALIENS (Hawa nao wanaweza kuwa wapo au hawapo)
 
Kule
Swali la kitoto hilo..?!Hii unafanya mashambulizi mabovu.Mbona kule nilipothibitisha yupo hauongelei.Mkuu kwa maneno machache nakuelezea wewe kuwa ni mtu ambae
Kule sijakujibu kwa sababu umeandika sana dhana, na gagaiko kubwa lilikuwa lipo huku ambapo umeweka nukta nyingi kuonyesha kutokuwepo Mola.
"Mungu HAUMJUI ila IMANI unayo pangine THABITI kabisa
Mimi namjua ndiyo maana naweza kumuelezea, ila wewe usiye mjua, unaona sawa awepo au asiwepi, sasa hatuwezi kufanana. Wewe mpaka leo hii hujui ya kuwa Mola ameweka taratibu zake zisizo badikika, tarstibu ambazo hata wewe leo ukitaka afanye kinyume hafanyi sababu ya taratibu, hapa ndiyo kumezidi kuonyesha wazi ya kuwa unae mzungumzia humjui, na hili ni kosa la jinai katika mawanda ya ELIMU.

Wewe endelea kuweka hoja zako uone kati yangu mimi na wewe,nani hamjui Mola.
Haya tuache yaendelee ya ALIENS (Hawa nao wanaweza kuwa wapo au hawapo)
Wanao amini uwepo wa Aliens, wote ni wavivu wa kufikiri na wapenda "shortcut" na hawana uthibitisho juu ya hilo zaidi ya filamu na habari ambazo katika msingi ya uhakiki wa habari hazi zingatiwi.

Kuamini uwepo wa Aliens na habari zake, ni kuikosea adabu Elimu na kuuhujumu ukweli.
 
Suala la uwepo wa Mungu si jambo la kana kwamba kuna watu kuwa ndio waligundua kuwa kuna Mungu na ndio wakajaza kutueleza.
Ukiangalia kwenye hili suala la kuwepo Mungu utaona point ile kukubali kuamini kuwepo Mungu hivyo hoja za kwamba hakuna uthibitisho na mengine yote yaliyozunguka hili suala ndio hufanya kuwe na maana hasa ya hiyo imani. Kwa jinsi ambavyo tunaelezwa kuhusu huyo Mungu basi kwa akili ya kawaida tu ni kwamba kama angetaka ajiweke dhahiri basi angeweza kufanya hivyo ila hilo halikuwa lengo.

Kwa mtazamo wangu.
 
Lovrly
 
Ndio utusaidie kumjua. Yani mtu akisema inawezekana yupo au hayupo au kwa kifupi hajui,anakuwa anafanya makosa katika hayo mawanda ya elimu?Hapana hii sasa ni kuwa judgemental. Hebu rahisisha tu kwa kunielezea unavyomjua,kwa sababu mimi sijapinga kitu ukumbuke hilo.Ila tu nilijaribu kujielezea kwa upande wa uwezekano wa kuwepo au kutokuwepo.Bila shaka ningekuwa NAMJUA AU NAJUA UKWELI THABITI,basi ningeshakuwa katika upande wa kuthibitisha au kutothibitisha.
NISAIDIE, utakuwa umesaidia na wengine pia.
Wala sina lengo la kukupinga ili nishinde. I'M AFTER TRUTH NDUGU YANGU
 
Ndio utusaidie kumjua. Yani mtu akisema inawezekana yupo au hayupo au kwa kifupi hajui,anakuwa anafanya makosa katika hayo mawanda ya elimu?
Bila shaka kabisa, sababu hutakiwi kubahatisha katika elimu. Kielimu ulitakiwa upate uhakika kwanza kisha ueneze habari hizo.
Hebu rahisisha tu kwa kunielezea unavyomjua,kwa sababu mimi sijapinga kitu ukumbuke hilo.
Huwezi kuwa pande zote katika jambo lenye ulazima wa kuwa upande mmoja, huko kuitumia vibaya akili. Bila shaka umenielewa.
Ila tu nilijaribu kujielezea kwa upande wa uwezekano wa kuwepo au kutokuwepo.
Usahihi ulitakiwa uendelee kufanya utafiti mpaka utakapo pata jibu lisilo shaka, na unachokifanya ni aina ya sanaa.
Bila shaka ningekuwa NAMJUA AU NAJUA UKWELI THABITI,basi ningeshakuwa katika upande wa kuthibitisha au kutothibitisha.
Sasa unatakiwa ukae kimya mpaka utakapo ujua ukweli, ndiyo uondoke nao huo ukweli.
NISAIDIE, utakuwa umesaidia na wengine pia.
Msaada wangu unaanzia katika kukuonyesha vipi unatakiwa ufikiri kwa usahihi, nakusaidia kwa kukuuliza maswali yafuatayo :

1. Je kuna kitu ambacho kinaweza kujiumba chenyewe kabla ya kuwepo kwake ?

2. Je kuna kitu kinaweza kuwepo pasi na chochote ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…