Proof: Binadamu alitengenezwa na Aliens

Proof: Binadamu alitengenezwa na Aliens

Usiniulize swali kabla hujajibu swali langu. Kwa akili yako ya kawaida tu unaona hili ni jibu ? Huwa mna shida gani vijana,nakupa mfano uone kwamba hujajibu swali.

Zurri : Kwema chief ?
Jurjani : Kwema kaka. Mzima ?
Zurri : Paula yupo ?
Jurjani : Hayupo.
Zurri : Imekuwaje leo hayupo ?
Jurjani : Sababu hayupo.

Sasa huu ujinga, unatakiwa uuache. Vipi tamko "hayupo" liwe ndiyo sababu ?

Nimekujibu: kwasababu hayupo

Lakini bado hujaridhishwa na unalazimisha nikupe sababu nyengine..Tena kwa mifano.!

Najibu tena: hayupo kwasababu kafa_ unaonaje.?
 
Nimekujibu: kwasababu hayupo
Hii siyo sababu, hili ni tokeo, sababu ni ile iliyofanya useme hayupo. Kwahiyo ndiyo utuambie hiyo sababu ni ipi.
Lakini bado hujaridhishwa na unalazimisha nikupe sababu nyengine..Tena kwa mifano.!
Nimekupa mfano mwepesi sana, lakini una poteza muda. Haya mambo hamuyawezi, achaneni nayo.

Mfano gani umeutoa katika hili ? Mfano nimeutoa mimi mzee.
Najibu tena: hayupo kwasababu kafa_ unaonaje.?
Usiniulize nauonaje,hapa tuna taka ukweli, labda kama kwako ukweli hauna nafasi na huuzingatii.

Safi, kama uko serious, lazima ujibu swali hili au hoja hii "Thibitisha kama kafa na kipi kimekujulisha kafa ?"
 
Safi, kama uko serious, lazima ujibu swali hili au hoja hii "Thibitisha kama kafa na kipi kimekujulisha kafa ?"
Kilichonijulisha kuwa kafa ni kwasababu hayupo

Na uthibitisho ni wewe kushindwa kithibitisha kuwa yupo
 
Kilichonijulisha kuwa kafa ni kwasababu hayupo

Na uthibitisho ni wewe kushindwa kithibitisha kuwa yupo
Hauko "serious" nikajua utakuwa unajua sababu ya kukana kwako, naona unarudia rudia kukosea.

Sijawahi kushindwa kuthibitisha uwepo wa Mola muumba, na sitoshindwa kufanya hivyo, ila wewe na wakubwa zako hamjawahi kuthibitisha ya kuwa Mola hayupo wala hamtoweza kufanya hivyo, zaidi ya kucheza na maneno bila kuzingatia maana na uhalisia.

Ukija na sababu ya umejuaje kwamba Mola hayupo, na ukija na ithibati ya kuwa Mola kafa. Unistue nikuwekee ushahidi wa kuwa Mola yupo.

Nyinyi inabidi tuwafundishe namna ya kufikiri kwa usahihi, unaposema Mola wetu kafa,ina maana alikuwepo, swali la msingi ni kuwa umejuaje kafa na kipi kilifanya akafa ?

Dondoo ya uwepo wa Mola tunaipata katika vifuatavyo :

1. Self-Evident Truth (Bayyinah)
2. Contingent Facts

Na nyingine nyingi. Nimekuwekea dondoo tu kukuonyesha ya kuwa suala la mimi kuthibitisha ya kuwa Mola yupo ni suala la dakika chache sana.
 
Hauko "serious" nikajua utakuwa unajua sababu ya kukana kwako, naona unarudia rudia kukosea.

Sijawahi kushindwa kuthibitisha uwepo wa Mola muumba, na sitoshindwa kufanya hivyo, ila wewe na wakubwa hamjawahi kuthibitisha ya kuwa Mola hayupo wala hamtoweza kufanya hivyo, zaidi ya kucheza na maneno bila kuzingatia maana na uhalisia.

Ukija na sababu ya umejuaje kwamba Mola hayupo, na ukija na ithibati ya kuwa Mola kafa. Unistue nikuwekee ushahidi wa kuwa Mola yupo.

Nyinyi inabidi tuwafundishe namna ya kufikiri kwa usahihi, unaposema Mola wetu kafa,ina maana alikuwepo, swali la msingi ni kuwa umejuaje kafa na kipi kilifanya akafa ?

Dondoo ya uwepo wa Mola tunaipata katika vifuatavyo :

1. Self-Evident Evident Truth (Bayyinah)
2. Contingent Facts

Na nyingine nyingi. Nimekuwekea dondoo tu kukuonyesha ya kuwa suala la mimi kuthibitisha ya kuwa Mola yupo ni suala la dakika chache sana.
Mungu inawezekana akawepo au asiwepo pia. Hapo ni suala la mtu kusadiki na kuamini tu,sio suala la kujua.
Kadhalika Aliens wanaweza wawepo au wasiwepo.
Lakini suala la uwezo wa binadamu kiakili hili lipo wazi,na SIAMINI kama aliens wanatusaidia katika technology, hayo makubwa ni matokeo ya akili kubwa za wanadamu wachache, kisha wengine tunanufaika
 
Nafikiri hivi pia.
 
Thibitisha hili.
JIBU sahihi kama Mungu yupo au hayupo ni SIJUI.
MUNGU HAYUPO
i)Haijawezekana kuthibitisha bila chembe ya shaka kwa mamia na maelfu ya miaka mpaka sasa,hali inayosababisha watu kuegemea katika "historia" za inasemekana zilizopo katika vitabu mbalimbali.Hali hii huwa inafanya suala hili liwe la mtu binafsi.
ii)Hathibitishi uwepo wake mwenyewe pasipo kusemekana katumia mwanadamu,hali inayoleta mkanganyiko mpaka leo kama hao waliotumika kweli walipata ridhaa kutoka kwa Mungu,au walikuwa na akili nyingi na lengo la kuifanya jamii iwe bora. Yani leo hata tukionana nikakwambia wasiliana na Mungu hata atupe njozi moja ndani ya wakati mmoja ili tuweze kuelezana uthibitisho wake, na zoezi hilo hata basi lifanyike kwa dunia nzima UTAKWAMA.
iii)Yanayowakuta wanaoamini na wasioamini katika maisha ni yaleyale yani shida na raha n.k hakuna exclusive na kukosekana kwa hiyo "exclusive" watu hujificha katika mwamvuli wa MIPANGO YA MUNGU,mathalan kuna viongozi wa imani ambao husema walifunga na kumwombea mtu aponywe gonjwa fulani na akapona lakini unakuta wao walikufa kwa kisukari,cancer e.t.c au utakuta kuna sala mtu anawekewa ataje mara idadi ngumu ya kibinadamu labda mara mia au maelfu na anafuatisha na mwisho anaweza kuambiwa asubiri "mipango ya mungu" au hakuwa na "imaan".
Labda nikuachie swali na wewe, je kwa nini linapokuja suala la Mungu uthibitisho wake umekuwa unategemea kudhihirishwa kupitia binadamu tena mmoja mmoja ambae anakuwa kaitwa "spesheli"?Je hakuna namna Mungu anaweza jidhihirisha mwenyewe kwa wakati mmoja kwa ulimwengu mzima?Kuliko hii ya alizaliwa Saudi Arabia,alizaliwa Israel,alitokea India n.k?
 
Thibitisha hili.
Nikirudi upande wa MUNGU YUPO,hapa nitaenda kirahisi tu, hakujatokea mwanadamu akaenda kinyume na kinachoitwa natural orders,hususan zama hizi.Sasa hapo katika natural orders kama tunasema kuna mwanzo, na mwanzilishi basi INAWEZEKANA aliyeziweka ndio MUNGU.
NB:Mimi bado namtafuta Mungu, lakini katika mipango ya duniani ili niishi bila bugudha na nipate "hali ya kujiskia kama sehemu ya jamii na mwanajamii" huwa najumuika maeneo ya imani.Suala hili huliacha liwe binafsi.
 
JIBU sahihi kama Mungu yupo au hayupo ni SIJUI.
Kielimu na kufata adabu zake, jubu lako la "SIJUI" lilitosha kabisa kukufanya wewe usijadili kuhusu uwepo wa Mola kwa njia yoyote ile zaidi ya kuuliza maswali ujibiwe.
i)Haijawezekana kuthibitisha bila chembe ya shaka kwa mamia na maelfu ya miaka mpaka sasa,hali inayosababisha watu kuegemea katika "historia" za inasemekana zilizopo katika vitabu mbalimbali.Hali hii huwa inafanya suala hili liwe la mtu binafsi.
Hapa nimecheka sana, ipi nafasi ya Historia katika kuupata ukweli ? Jibu rahisi sana, huwezi kurejea ya nyuma bila kurejea historia.

Pili, hizo "Historia za inasemekana" umezipata wapi huku kwetu sijaziona labda hizi mnazo nyinyi mnao mkana Mola pasi kumjua.

Tatu, haijawezekana kuthibitishwa kwa nani ?
 
ii)Hathibitishi uwepo wake mwenyewe pasipo kusemekana katumia mwanadamu,hali inayoleta mkanganyiko mpaka leo kama hao waliotumika kweli walipata ridhaa kutoka kwa Mungu,au walikuwa na akili nyingi na lengo la kuifanya jamii iwe bora. Yani leo hata tukionana nikakwambia wasiliana na Mungu hata atupe njozi moja ndani ya wakati mmoja ili tuweze kuelezana uthibitisho wake, na zoezi hilo hata basi lifanyike kwa dunia nzima UTAKWAMA.
Kama unakubali kabisa ya kuwa dunia ipo katika utaratibu na nidhamu, yaani kuna usiku na mchana, kitu kikirushwa kwenda juu lazima kurudi chini, jua linazama magharibi na kuchomoza mashariki, huu ni utaratibu wake kama alivyoweka utaratibu wa kufikisha ujumbe kwa waja, aliweka utaratibu wa kuwachagua waja fulani miongoni mwa waja wake kisha anawapa ujumbe.

Watu walio kuwa wanatumwa walikuwa wanapewa mambo kwayo hakuna mwanadamu anaweza kuyafanya lwa hali yoyote ile, na ilikuwa hivyo ili kuwashawishi waweze kuukubali ujumbe husika.

Unapotaka mimi leo hii niwasiliane na Mola kwa mtindo unao taka, unao nyesha ya kuwa humjui Mola, sababu taratibu haziko hivyo unavyotaka wewe. Mola alivyo tuumba hakutuacha hivi hivi, aliweka ishara za kumtambua yeye kwa kila kiumbe, ndiyo maana anapotokea mty kumkana ujue anaenda kinyume na asili na silika.
 
Kielimu na kufata adabu zake, jubu lako la "SIJUI" lilitosha kabisa kukufanya wewe usijadili kuhusu uwepo wa Mola kwa njia yoyote ile zaidi ya kuuliza maswali ujibiwe.

Hapa nimecheka sana, ipi nafasi ya Historia katika kuupata ukweli ? Jibu rahisi sana, huwezi kurejea ya nyuma bila kurejea historia.

Pili, hizo "Historia za inasemekana" umezipata wapi huku kwetu sijaziona labda hizi mnazo nyinyi mnao mkana Mola pasi kumjua.

Tatu, haijawezekana kuthibitishwa kwa nani ?
Maswali gani haya sasa, haijaweza kuthibishwa na nani? Kwa hapa kwetu au watu wa mazingira yetu Tanzania ni Waislamu na Wakristo!
Halafu umeshaniweka katika kundi la wasiokubali kama Mungu yupo😂😂.Mi nimesema SIJUI ila najumuika sehemu mainly for "social benefits" kama vile kuwa sehemu ya jamii, na mipango mingine ya kurahisisha maisha.Pamoja na kujifunza huenda kuna siku nikajidhihirishia uwepo wake bila chembe ya shaka.
Lakini wewe unataka kuleta UONGO WA KUJUA UKWELI HALISI
 
iii)Yanayowakuta wanaoamini na wasioamini katika maisha ni yaleyale yani shida na raha n.k hakuna exclusive na kukosekana kwa hiyo "exclusive" watu hujificha katika mwamvuli wa MIPANGO YA MUNGU,mathalan kuna viongozi wa imani ambao husema walifunga na kumwombea mtu aponywe gonjwa fulani na akapona lakini unakuta wao walikufa kwa kisukari,cancer e.t.c au utakuta kuna sala mtu anawekewa ataje mara idadi ngumu ya kibinadamu labda mara mia au maelfu na anafuatisha na mwisho anaweza kuambiwa asubiri "mipango ya mungu" au hakuwa na "imaan".
Kweli humjui Mola ajabu unamjadili hili tatizo ni la kutomua Mola. Katika taratibu za Mola akileta msiba au majanga huwakuta wahusika na waiso husika, kisha hesabu na kulipwa stahiki siku ya malipo, huu ndiyo utaratibu alio uweka.
Labda nikuachie swali na wewe, je kwa nini linapokuja suala la Mungu uthibitisho wake umekuwa unategemea kudhihirishwa kupitia binadamu tena mmoja mmoja ambae anakuwa kaitwa "spesheli"?Je hakuna namna Mungu anaweza jidhihirisha mwenyewe kwa wakati mmoja kwa ulimwengu mzima?Kuliko hii ya alizaliwa Saudi Arabia,alizaliwa Israel,alitokea India n.k?
Umeuliza swali la kitoto sana, uthibitisho wa Mola upo kwa kile mtu, hasa ambaye akili yake na imani take haijachafuliwa na fikra za ukana Mungu na upotoshaji na imani potofu.

Leo hii ukienda kwa mtu yoyote ambaye hajafikiwa na imani yoyote ukimuuliza juu ya uwepo wa Mola hakanushi hilo. Yaani kila mwanadamu ameumbwa na haki ya kukubali uwepo wa Mola isipokuwa tu watu wamechafuliwa fikra zao.

Kadhalika tuna weza kujua uwepo wa Mola muumba kwa kutumia akili, milango ya fahamu, mazingira ba maumbile na ufunuo. Hivi vyote vinathibitisha uwepi wake.

Ushauri wangu ni kuwa, kamwe usije kukanusha jambo ambalo huna elimu nalo, hili ni kosa kubwa sana.
 
Halafu umeshaniweka katika kundi la wasiokubali kama Mungu yupo😂😂.
Naanzia hapa, nimekujibu vile kwa kile ulichokiandika mzee. Kwahiyo wewe jibu hoja.
Lakini wewe unataka kuleta UONGO WA KUJUA UKWELI
Ukweli halisi uko wazi ni kuuchukua tu. Allah katika Qur'aan anawapa changamoto watu wanao mkana ya kuwa wajibu maswali haya :

1. Je wao wametokana pasi na chochote au ?
2. Wao wamejiumba ?

Sasa akili timamu na ikiyo salama haikatai uwepo wa Mola, ukiona una kana tu ujue akili yako haiko salama yaani una matatizo ya kujitakia.
Maswali gani haya sasa, haijaweza kuthibishwa na nani? Kwa hapa kwetu au watu wa mazingira yetu Tanzania ni Waislamu na Wakristo!
Rejea ulichokiandika.
 
Kweli humjui Mola ajabu unamjadili hili tatizo ni la kutomua Mola. Katika taratibu za Mola akileta msiba au majanga huwakuta wahusika na waiso husika, kisha hesabu na kulipwa stahiki siku ya malipo, huu ndiyo utaratibu alio uweka.

Umeuliza swali la kitoto sana, uthibitisho wa Mola upo kwa kile mtu, hasa ambaye akili yake na imani take haijachafuliwa na fikra za ukana Mungu na upotoshaji na imani potofu.

Leo hii ukienda kwa mtu yoyote ambaye hajafikiwa na imani yoyote ukimuuliza juu ya uwepo wa Mola hakanushi hilo. Yaani kila mwanadamu ameumbwa na haki ya kukubali uwepo wa Mola isipokuwa tu watu wamechafuliwa fikra zao.

Kadhalika tuna weza kujua uwepo wa Mola muumba kwa kutumia akili, milango ya fahamu, mazingira ba maumbile na ufunuo. Hivi vyote vinathibitisha uwepi wake.

Ushauri wangu ni kuwa, kamwe usije kukanusha jambo ambalo huna elimu nalo, hili ni kosa kubwa sana.
Sijafanya hilo kosa kubwa, tangu mwanzo nimesema anaweza kuwepo na asiwepo pia☺☺.
Swali la kitoto hilo..?!Hii unafanya mashambulizi mabovu.Mbona kule nilipothibitisha yupo hauongelei.Mkuu kwa maneno machache nakuelezea wewe kuwa ni mtu ambae
"Mungu HAUMJUI ila IMANI unayo pangine THABITI kabisa"
Haya tuache yaendelee ya ALIENS (Hawa nao wanaweza kuwa wapo au hawapo)
 
Kule
Swali la kitoto hilo..?!Hii unafanya mashambulizi mabovu.Mbona kule nilipothibitisha yupo hauongelei.Mkuu kwa maneno machache nakuelezea wewe kuwa ni mtu ambae
Kule sijakujibu kwa sababu umeandika sana dhana, na gagaiko kubwa lilikuwa lipo huku ambapo umeweka nukta nyingi kuonyesha kutokuwepo Mola.
"Mungu HAUMJUI ila IMANI unayo pangine THABITI kabisa
Mimi namjua ndiyo maana naweza kumuelezea, ila wewe usiye mjua, unaona sawa awepo au asiwepi, sasa hatuwezi kufanana. Wewe mpaka leo hii hujui ya kuwa Mola ameweka taratibu zake zisizo badikika, tarstibu ambazo hata wewe leo ukitaka afanye kinyume hafanyi sababu ya taratibu, hapa ndiyo kumezidi kuonyesha wazi ya kuwa unae mzungumzia humjui, na hili ni kosa la jinai katika mawanda ya ELIMU.

Wewe endelea kuweka hoja zako uone kati yangu mimi na wewe,nani hamjui Mola.
Haya tuache yaendelee ya ALIENS (Hawa nao wanaweza kuwa wapo au hawapo)
Wanao amini uwepo wa Aliens, wote ni wavivu wa kufikiri na wapenda "shortcut" na hawana uthibitisho juu ya hilo zaidi ya filamu na habari ambazo katika msingi ya uhakiki wa habari hazi zingatiwi.

Kuamini uwepo wa Aliens na habari zake, ni kuikosea adabu Elimu na kuuhujumu ukweli.
 
JIBU sahihi kama Mungu yupo au hayupo ni SIJUI.
MUNGU HAYUPO
i)Haijawezekana kuthibitisha bila chembe ya shaka kwa mamia na maelfu ya miaka mpaka sasa,hali inayosababisha watu kuegemea katika "historia" za inasemekana zilizopo katika vitabu mbalimbali.Hali hii huwa inafanya suala hili liwe la mtu binafsi.
ii)Hathibitishi uwepo wake mwenyewe pasipo kusemekana katumia mwanadamu,hali inayoleta mkanganyiko mpaka leo kama hao waliotumika kweli walipata ridhaa kutoka kwa Mungu,au walikuwa na akili nyingi na lengo la kuifanya jamii iwe bora. Yani leo hata tukionana nikakwambia wasiliana na Mungu hata atupe njozi moja ndani ya wakati mmoja ili tuweze kuelezana uthibitisho wake, na zoezi hilo hata basi lifanyike kwa dunia nzima UTAKWAMA.
iii)Yanayowakuta wanaoamini na wasioamini katika maisha ni yaleyale yani shida na raha n.k hakuna exclusive na kukosekana kwa hiyo "exclusive" watu hujificha katika mwamvuli wa MIPANGO YA MUNGU,mathalan kuna viongozi wa imani ambao husema walifunga na kumwombea mtu aponywe gonjwa fulani na akapona lakini unakuta wao walikufa kwa kisukari,cancer e.t.c au utakuta kuna sala mtu anawekewa ataje mara idadi ngumu ya kibinadamu labda mara mia au maelfu na anafuatisha na mwisho anaweza kuambiwa asubiri "mipango ya mungu" au hakuwa na "imaan".
Labda nikuachie swali na wewe, je kwa nini linapokuja suala la Mungu uthibitisho wake umekuwa unategemea kudhihirishwa kupitia binadamu tena mmoja mmoja ambae anakuwa kaitwa "spesheli"?Je hakuna namna Mungu anaweza jidhihirisha mwenyewe kwa wakati mmoja kwa ulimwengu mzima?Kuliko hii ya alizaliwa Saudi Arabia,alizaliwa Israel,alitokea India n.k?
Suala la uwepo wa Mungu si jambo la kana kwamba kuna watu kuwa ndio waligundua kuwa kuna Mungu na ndio wakajaza kutueleza.
Ukiangalia kwenye hili suala la kuwepo Mungu utaona point ile kukubali kuamini kuwepo Mungu hivyo hoja za kwamba hakuna uthibitisho na mengine yote yaliyozunguka hili suala ndio hufanya kuwe na maana hasa ya hiyo imani. Kwa jinsi ambavyo tunaelezwa kuhusu huyo Mungu basi kwa akili ya kawaida tu ni kwamba kama angetaka ajiweke dhahiri basi angeweza kufanya hivyo ila hilo halikuwa lengo.

Kwa mtazamo wangu.
 
Natumai humu nyote ni wazima wa afya njema kabisa ,pole kwa yote lakini leo napenda kutoa mchango wangu kidogo kulingana na nilichopata kukiona au kujidhihilisha juu ya swali gumu ambalo limekosa majibu miaka nenda rudi juu ya binadamu alitoka wapi...

Sio lazima ukomaee na mealezo yangu lakini kama una imani yako baki na imani yako lakini kama unahitaji kujifunza mambo basi weka imani yako pembeni upate kujua haya..

=======================

kabla sijaendelea napenda kukufahamisha wewe au wale ambao mnapuuza sana juu ya conspiracy theories na kudai kuwa hazina proof sasa leo unaweza pata kitu hapa..

katika mwili wa kiumbe yoyote yule,kuna kitu iinachoitwa DNA hiki ndo kinachobeba mwongozo wa jinsi utakavyokuja hapa duniani kwa sura ipi,mfumo upi,mwonekano upi,kwa tabia ipi na sifa zote hizi hubebwa na kitu kinachoitwa DNA,

DNA ndo kila kitu kwan imebaba taarifa zote juu ya utengenezaji wa kila kitu ulichonacho mwilini..
killa kitu ulicho nacho mwilini mwako kuna specific genes (jeni) ambayo inahusika na utengenezaji wake,ikitokea jeni inayohusika kutengeneza pua imepata hitilafu ukiwa bado tumboni kwa mama yako basi utengenezwaji wa pua utakosekana na utazaliwa ukiwa huna pua,na ikitokea jeni(gene) inayohusika na kutengeneza remodeling ya sura yako iwe nzuri ila ikapata hitilafu basi utazaliwa ukiwa na sura kama kinyago.

All in all, genes ndo kila kitu katika mwili wa kiumbe yoyote yule,hizi abnormality tunazoziona ni kwa sababu gene zetu zinapata hitilafu mahala fulani kwenye arrangement zake ndani ya DNA sequence..

Arrangement za gene zetu zipo kwenye DNA kwa mfumo wa base pairing rule ,Genes zinaundwa na DNA bases ambazo zipo katika makundi mawili ( purine na pyrimidine ,ambapo purine ni Adenine (A) na Guanine (G) lakini pia pyrimidine ni Cytocine (C),Tymine (T) na Uracil (U).Ila katika namna ya kupair ili kuform gene tunaona kuwa Adenine huwa anapair na Tymine hence A=T katika DNA na kwenye RNA inakuwa A=U Wale waliosoma molecular chemistry na bioloji watakuwa wanalijua hili. lakini pia Cytocine anapair na Guanine hence C=G
View attachment 839829

kwa hiyo purine ana pair na pyrimidine mmoja ili waform complimentary sequence ya kuja kutengenza gene factor control..

Ili tuite kuwa hii ni genetic code( mfumo uliohifadhi taarifa ) ni lazima hizo bases ziwe tatu...mfano wa genetic code ni kama CCU, GAA,GGC,GAC,....na ni lazima ziwe triplet ( Tatu)...

kwa mfano gene inayohusika na utengeneza wa jicho inaundwa na genetic code ya ACG manake itokea mtu akapat effects ( Hitilafu) kwenye arrangement hiyo ya ACG na kuwa AGC hapo tunasema gene imepata mutation na kazi yake ya kutengeneza jicho inapotea kwa hiyo mtu atazaliwa hana jicho

Lakini ukiangalia vizuri kwenye sequence hiyo kuna DNA bases au kwa jina jingine tunaita DNA codes hazipei kutengeneza functional gene( genes zinazohusika kutengeneza mfumo ufanyao kazi)..Zinabaki hivo hivo tu..ni kama asilimia 85 ya DNA bases hazina kazi ya kutengeneza functional amino acid..

So only few percents DNA codes zilizopo kwenye DNA yetu ndo zina gene code zinazotengeneza protein kwa ajili ya kutengeneza specific organ mwilini mwetu kwa wakati maalumu..

SWALI JE": Hizo code zingine zinatengeneza nini au kazi yake ni nini sasa.....??

kiufupi tunapata makundi mawili ya genes hapo,coding genes na non- coding genes,,

Kuna genes zinazopair ili kuunda functional genes( genes zinazofanya kazi na kuleta umbo maalumu mwilini) lakini kuna baadhi ya genes kwenye hoiyo hiyo DNA sequence hazi match (non- coding genes) kutengeneza functional genes,,ni wazi kuwa kila bionadamu ana non- coding genes ambazo hazicode kwa chochote mwilini mwake na kwanini ziwepo wakati hazina kazi..?
View attachment 839830wale watu wa molecular analysis na DNA chemistry nadhani hata nyie mtajiuliza au bila shaka mshajiuliza kwanini non- coding genes zipo tu na hazihusiki kwa chochote,,,

lakini pia
Jozi ya wanasayansi kutoka Kazakhstan wanaamini kuwa aina zetu ziliundwa na mamlaka ya juu, ustaarabu wa mgeni ( Aliens) ambao ama alitaka kuhifadhi ujumbe katika DNA yetu au tu kupanda maisha kwenye sayari nyingine kwa muonekana tofauti wenye idadi flani ya kiwango cha vinasaba elekezi kisha kupandikiza aina nyingine ya vinasaba shirikishi( non- coding bases) ili vitumike kama signal transer kwenye main controller system ya kumwendesha mwanadamu katika maaumuzi ya chaguzo mbali mbali katika maisha yake..

Maxim A. Makukov wa Taasisi ya Astrophysical ya Fesenkov na Vladimir I. Shcherbak kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Farabi Kazakh alitumia miaka 13 akifanya kazi kwa Mradi wa Binadamu wa Genome - ambao ulituma ramani ya DNA ya binadamu katika kutupa picha halisi ya codes zilizopo kwenye DNA ambazo ni functional na ambazo sio functional kwa kucompare usawa na arrangement zilizopo kwenye baadhi ya cell za humanoid Aliens..

Hitimisho lao lilikuwa kwamba wanadamu walitengenezwa na nguvu ya juu, na "seti ya mifumo ya hesabu na lugha ya kibei kutoka mfumo wa nje kabisa wa ufahamu na mpangilio huo uliingizwa ndani ya DNA yetu.
coincidence,,??

Kutokana na kuwepo kwa group la non -coding genes kwenye DNA yetu wanasayansi wamefikia hatua ya kulipa jina la JUNK DNA ,means gene DNA ambazo kazi yake haijulikani bado.

Comparative genomics studies have shown that some of this junk DNA is highly conserved, sometimes over hundreds of millions of years, which suggests that these non-coding regions have undergone positive selection throughout evolution and confer an advantage in terms of preserving or minimizing certain biological traits.
(Uchunguzi wa jenomatiki umeonyesha kwamba baadhi ya DNA hii isiyojumuishwa imeonekana kuhifadhiwa sana katika mfumo wetu wa DNA , na wakati mwingine juu ya mamia ya mamilioni ya miaka, ambayo inaonyesha kuwa baadhi ya sehemu katika hii DNA imeonekana kubeba chembe chembe au vipande toka sehemu au DNA ya viumbe toka Anga za mbali... lakini mabadiliko yatokayo na mazingira huweza kuhifadhi au kupunguza baadhi ya sifa za kibiolojia.)

Kuna baadhi ya tafiti zimekuja kufanyika kwa kuhusisha DNA sequence ya HUMANOID ALIENS na kukuta kuwa seqence ya non- coding genes kwa binadamu zinafanana kidogo na a part of DNA pair genes kwenye HUMANOID ALIEN DNA.

Kwa hiyo inawezkana kabisa human being were programmed na Aliens kwa kazi maalumu na they are watching us for sure,,
View attachment 839838
DID EXTRATERRESTRIALS GENETICALLY ENGINEER HUMANS?

Uumbaji na mageuzi ni nadharia mbili maarufu za jinsi watu walivyokuwa,Ingawa labda ni nadharia zinazoenea zaidi, kuna shule au maelezo mengine yanahitajika kuelezea hili kuwa Binadamu aliundwa na tunaendelea kuprogramiwa na Extraterrestrial beings ( Aliens species).

Nadharia nyingine inachunguza wazo kwamba extraterrestrials manipulated DNA yetu kisha kujenga damu mchanganyiko katika sayari yetu. Kipande cha ushahidi muhimu zaidi kuunga mkono nadharia hii ni kitu kinachojulikana kama Rh.( Factor blood group) ambayo ni aina ya Protein inayopatikana kwenye surface membrane za Cell nyekundu ( RBC) zilizopo kwenye miili yetu...kuna aina mbili za cell nyekundu za damu ,ile yenye Protein juu inafanya damu iitwe Rhesus positive ( Rh +ve) wakati zile cell nyekundu ( RBC) ambazo hazina Protein juu ya ngozi zao zinafanya damu iitwe Rhesu negative( Rh -ve) ..

Uwepo wa kipengele cha (Rhesus factor blood groups ) katika damu ya binadamu hufanya aina ya damu iwe chanya (Rhesus positive), wakati kutokuwepo kwake hufanya iwe hasi(Rhesus negative blood group). Watu wengi ni Rh chanya, na asilimia 15 tu ya idadi ya watu hawana sababu ya Rh.

Sababu ya Rh inaweza kuhusishwa na aina nyingine, hususani upandikizajinwa aina ya control gene factor toka Viumbe wenye uwezo mkubwa katika maarifa japo Ukosefu wa hiyo unaendelea kubaki siri. Hata hivyo, baadhi ya watu wanaamini kuwa inatokana na vitu vya nje. Wengi wanaokataa mgeni ni Rh hasi. ukiangalia kweli ni nadra sana kuwapata watu wenye blood group zenye RHESUS negative na baadaye nasikia lakini kuwa eti huwa wanapotea mazingira ya kutatanisha kama walivyoalbino'''( kwanini tena hapa tunapata watu wenge group jingine lenye kizazi che damu hasi ???)...

Je! Hii ni bahati mbaya? Inaonekana haiwezekani

======================

Researcher David Icke anasema ,Huenda baada ya galactic civilization kwenye planet za mbali huko kuvurugika na kuleta hitilafu kubwa,familia nyingi za Aliens zilipata kutokuelewana na kusababisha mvurugano mkubwa ulioleta destructions za baadhi ya empire zao na kusababisha kusambaratika kwa madini maalumu kama ALMAS,GOLD,URANIUM,NEUTRON,PRUTONIUM,RADIUM ambayo ndo yanatumika kujengea empire zao n.k na kumewapelekea ku design species watakaowasidia kurudisha baadhi ya madini hayo yaliyoangukia kwenye planet mbalimbali ambayo mojawapo ni EARTH,so existance ya human being ni programmed issue by Alien ndo mana wametuwekea signal za kuwasiliana nao,na signal hizo ni non-coding DNA genes bases katika Vinasaba vyetu( DNA)..

Yani wamekuwekea DNA genes zitakazoprogrm mwili wako lakini pia wawe wanapata informations kutoka kwako indirectly.....

Or could we say that,the Earth is just the area with bebris from garactic civilized araes beyond our solar system.....!!!...

Mipango mingi sana inahusisha kuscan DNA zetu ili ziingizwe kwenye Universal Data Base ( UDB)..

lengo lake ni nini sasa,,?/

Kwanini uwepo wa link kati ya human na Alien unafichwa sana ..??
kuna makubaliano makubwa sana kwanini siri hii imeendelea kuwepo .?

Everything is by plan...
kusema kuwa lengo lao ni kufanya ukusanyaji wa madini yaliyopungua kwao au kurudisha baadhi ya madini inaweza ikawa point moja wapo ya kumprogram human being kama second collector wao..lakini pia kumtengeneza kiumbe ambaye atahifadhi traits(vinasaba ) zao kutokana na mlipuko wa gases za radiations mbalimbali kama Radium,prutonium ambazo zilionekana kuathiro mfumo wa miili yao hivyo kufikia wazo la kudesign another species kwa ajili ya kuhuifadhi vinasaba vyao ..

Kuna baadhi ya documentary moja inaelezea kuwa Aliens empire katika baadhi ya high worlds ilivamiwa na cosmic radiation na kuwafanya kuanza kuchange color ya miili yao despite of being interlectual lakini hakuna kigumu mbele ya nature controller..

Baada ya kuvamiwa na hizo cosmic radiations iliwabidi aliens kutafuta ni wapi wataweza pandikiza DNA zao kwa ajili ya kuzuia Mutation( mabadiliko ya miili yao) kwa badae ..

Ndo wakamua kuprogram viumbe ambao waliwaleta katika planet tofauti ikiwemo na dunia hii ili waweze kutunza biological traits zao..

Lakini kwenye sayari zingine inasemekana kuwa hazikuwa nzuri sana kwani mabadiliko zaidi yalionekana kuwaathiri viumbe walioprogramiwa na kufanya kusitisha zoezi hilo lakini ilionekana kuwa dunia ndo Sayari pekee ambayo haikuwa na uwezo wa kuundergo effects za cosmic radiations ambazo zinaleta mutation ya hizo traits za viumbe hao...

Ndo mana inawezekana kabisa kuwa Aliens wameamua kuwekeza hii kind of programing human being hasa dunia hii kwani some traits zao zipo ndani ya miili yetu ndo hizo Non- coding DNA ..

Unajua kama unataka kuhifandhi kitu kwa muda mrefu ni dhahili utaandaa mazingira ya kuweza kumudu hali hiyo..

Ukitaka kupata ukweli huu jaribu kuumiza kichwa kwanin non- coding DNA ndan ya miili yetu..?.

President John Adams passes the Naturalization Act, the first of four pieces of controversial legislation known together as the Alien and Sedition Acts, on this day in 1798.
(Rais John Adams anapitisha Sheria ya Ustawi, kwanza ya vipande vinne vya sheria ya utata inayojulikana kama Mgeni na Matendo ya Utamaduni, leo katika 1798.ambayo iliipa America kibali cha kufanya negotiation na Aliens kwa kazi maalumu lakini mambo yalifanywa siri nzito sana..)

Na kwanini watu wengi wanaofanya kazi kwenye taasisi hizi za siri hasa serikali kama inajihusisha na maswali ya utafiti huwa wanakufa vifo vya ajabu sana,,

Nchi kama marekani yani watu wengi waliopo NASA kila wakisataafu wanarun mental problems na hiyo tunaita MENTAL ABDUCTION ,au wanaishia kuugua magonjwa kama Kiharusi ( Stroke) au Hypertensive diseases au Cardiovascular diseases kama HEART ATTACK,HEART FAILURE ,au BRAIN CANCER ,au CANCER OF UNKNOWN AETIOLOGY,,??

Kwanini watu wengi baada ya kufanya kazi kwenye taasisi hizo za siri wanapojaribu kutoa siri nyingi juu ya mambo yalivyo huwa wanaishia kupata ukichaa,,??

Fuatilia hili kama una ndugu yako anayefanya kazi serikalini hasa serikali za siri lazima kila wakistaafu watapata mental problem ,sio wote ila ni baadhi kulingana na sehemu na kitengo alichokuwa ,,

Hii yote pengine wasije kuanza kulopoka huko nje baada ya kutoka kifungoni..

Aliens are more superior interms of intellectual than human being ,tunaona technologia ikikua kwa kasi jambo ambalo lipo kinyume na utendaji kazi wa ubongo wa sasa wa mwanadumu,..kuna nini nyuma ya pazia,,??

kwanini uwezo wa mwanadamu kufikiri unapungua lakini technolojia inakuwa kwa kasi,,?? kina nani wanaoratibu haya mambo nyuma ya pazia.??

Tusije kweli kuwa tumeprogramiwa na Aliens kuwasaidia kuchukua hayo madini yaliyosambaratika kutoka kwao huko miaka mingi iliyopita na kuwafanya kuuumiza akili sana namna ya kufanya hiyo kazi ya kuanza kutafuta madini underground kwetu ila wakaamua kuprogram species watakaofanya hiyo kazi?? Pengine isiwe point ya kusema tumetengenezwa kuendeleza kizazi cha kukusanya madini bali pia kuhifadhi mfumo wao wa DNA AU VINASABA.
View attachment 839884

Nilipata muda wa kutembelea mradi wa kuzalisha umeme nchini Tanzania unaitwa Kihansi Electrical Project upo Mpakani mwa IFAKARA Wilaya ya kilombero mkoani Morogoro na Iringa
NADHANI ndo mradi uliocomplicated kuliko miradi yote ya umeme iliyopo Tanzania na Africa Mashariki kwa ujumla..

Umeme wa KIHANSI unazaliswa Underground kabsa ,yani kuna mlima mkubwa sana halafu wamechonga tunnel inayoingia ndani ya mlima huo yenye umbali wa kilometre 3 halafu ndo unazama tena chini kwa umbali wa km 2 ndo unafika underground ambako kuna makazi ya watu na mitambo yote,,kule chini ni kama umeingia MLIMAN CITY SHOPPING CENTRE yan mitambo imeegeshwa huko balaaa,..

Sasa nikawa namuuliza Engineer aliyekuwa zamu kuwa hivi ni binadamu kweli aliyehusika hapa au kuna some extra terrestrial ones,,??
aliishia kucheka na kuniambia under collaborations with some people iliwezekana. SASA KWANINI ALISEMA UNDER Collaborations TULIWEZA,HIYO COLLABOLATIO NA NANI..??

Kwa akili yangu sikuweza na sitaweza kuamini kama binadamu angeweza kupata access ya knowledge yote ile maybe sijui lakini..

mwisho,,,
Napenda kuomba mchango wenu wadau wenye ujuzi au uelewa juu ya maelezo mengine juu ya uwepo wa non-coding DNA bases kwenye mwili wetu lakini pia unapaswa ujiulize kuwa ,ni nini kazi ya non- functional genes,??
kwanini utafiti uliofanywa na wanasayansi Area 51 juu ya DNA sequence ya human na Alien ulionekana kufanana kwa percent flani kwenye non -coding genes??

JE; tunaweza kweli kuwa ni programmed species za hao jamaaa,,?

cc
Da vincci Kipanga boy Sokoro waito Bitoz Sticky_fingers George_Mbuligwe Kiranga Humble African zitto junior TIASSA GuDume Francis3 Internal Lee Napoleon

========================

Karibuni......
Lovrly
 
Wewe endelea kuweka hoja zako uone kati yangu mimi na wewe,nani hamjui Mola.

Wanao amini uwepo wa Aliens, wote ni wavivu wa kufikiri na wapenda "shortcut" na hawana uthibitisho juu ya hilo zaidi ya filamu na habari ambazo katika msingi ya uhakiki wa habari hazi zingatiwi.

Kuamini uwepo wa Aliens na habari zake, ni kuikosea adabu Elimu na kuuhujumu ukweli.
Ndio utusaidie kumjua. Yani mtu akisema inawezekana yupo au hayupo au kwa kifupi hajui,anakuwa anafanya makosa katika hayo mawanda ya elimu?Hapana hii sasa ni kuwa judgemental. Hebu rahisisha tu kwa kunielezea unavyomjua,kwa sababu mimi sijapinga kitu ukumbuke hilo.Ila tu nilijaribu kujielezea kwa upande wa uwezekano wa kuwepo au kutokuwepo.Bila shaka ningekuwa NAMJUA AU NAJUA UKWELI THABITI,basi ningeshakuwa katika upande wa kuthibitisha au kutothibitisha.
NISAIDIE, utakuwa umesaidia na wengine pia.
Wala sina lengo la kukupinga ili nishinde. I'M AFTER TRUTH NDUGU YANGU
 
Ndio utusaidie kumjua. Yani mtu akisema inawezekana yupo au hayupo au kwa kifupi hajui,anakuwa anafanya makosa katika hayo mawanda ya elimu?
Bila shaka kabisa, sababu hutakiwi kubahatisha katika elimu. Kielimu ulitakiwa upate uhakika kwanza kisha ueneze habari hizo.
Hebu rahisisha tu kwa kunielezea unavyomjua,kwa sababu mimi sijapinga kitu ukumbuke hilo.
Huwezi kuwa pande zote katika jambo lenye ulazima wa kuwa upande mmoja, huko kuitumia vibaya akili. Bila shaka umenielewa.
Ila tu nilijaribu kujielezea kwa upande wa uwezekano wa kuwepo au kutokuwepo.
Usahihi ulitakiwa uendelee kufanya utafiti mpaka utakapo pata jibu lisilo shaka, na unachokifanya ni aina ya sanaa.
Bila shaka ningekuwa NAMJUA AU NAJUA UKWELI THABITI,basi ningeshakuwa katika upande wa kuthibitisha au kutothibitisha.
Sasa unatakiwa ukae kimya mpaka utakapo ujua ukweli, ndiyo uondoke nao huo ukweli.
NISAIDIE, utakuwa umesaidia na wengine pia.
Msaada wangu unaanzia katika kukuonyesha vipi unatakiwa ufikiri kwa usahihi, nakusaidia kwa kukuuliza maswali yafuatayo :

1. Je kuna kitu ambacho kinaweza kujiumba chenyewe kabla ya kuwepo kwake ?

2. Je kuna kitu kinaweza kuwepo pasi na chochote ?
 
Back
Top Bottom