In reality hakuna hili kundi linaloitwa Sukuma Gang, ni just a fictitious group in people's minds za watu waliofilisika kisiasa!. Siamini kama Rais Mama Samia amechukua maamuzi yoyote kwasababu ya dhana hii ya Sukuma Gang, kwasababu Samia sio muflis!. Ila kwa vile baadhi ya waliotumbuliwa ni watu wa JPM, Bashiru, Polepole, Kalemani, Lukuvi, Kabudi, no vizuri Mama akawa muwazi kwanini amewaondoa, nilishauri
Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
P
Pascal Mayalla
MWAKA 2022, Familia ya WATU WAZURI HAWAFI ilitumia nguvu kubwa kumdanganya Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwenye mambo mengi ili kujitengenezea uhalali wa kukaa kwenye nafasi nyeti za uongozi huku wakijua hawana uwezo na nafasi hizo bali kutafuta masiahi binafsi.
Walitumia nafasi hiyo kumhadaa kuwa kuna kundi linaitwa SUKUMA GANG linamhujumu utawala wake kwa hiyo aliondoe kwenye nafasi za uongozi ili wao watawale nafasi zote nyeti serikali kurahisisha mipango yao.
Miongoni mwa viongozi waliotuhumiwa na familia hiyo kwamba eti wanamhujumu Rais Samia ni pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai na lengo la kumuondoa Ndugai ili familia hiyo ilitawale Bunge na kupitisha Sheria mbalimbali ambazo zitawabeba kwenye mambo yao binafsi ikiwemo biashara zao na miradi wenye manufaa nayo kama familia.
Medard Kalemani naye akaondolewa Wizara ya Nishati akapukutishwa na Uongozi wote akiwemo Katibu Mkuu na Watendaji wakuu wa TANESCO ili kufanikisha mambo binafsi ya familia hiyo tunayoyaona sasa.
Mradi mkubwa wa JNHPP ili uvurigike na pesa nyingi ziendelee kulipwa kwa familia hiyo ndio maana Waziri Makamba licha ya kufahamu kuwa wakati Rais Samia anaingia ulikuwa umefikia 52% lakini akaja na takwimu zake kwamba ulikuwa 37% ina maana fedha za 15% ya ujenzi zinakwenda kwenye familia. huku Mwigulu naye akisema ulikuwa 12%.
Dili ya Ruzuku ya mafuta ya bilioni 100 kila mwezi ambayo hadi leo hakuna mtanzania anayejua fedha hizo analipwa nani? ni moja ya manufaa wanayopata familia ya WATU WAZURI HAWAFI.
Wizara ya Ujenzi, Injinia Chamriho akaondolewa ili miradi mikubwa kama SGR, Meli ya MV MWANZA Hapa Kazi, Daraja la Kigongo Busisi nayo icheleweshwe ujenzi wake na iongezewe gharama za ujenzi kwa manufaa ya familia hiyo
Mradi wa SGR kuagiza mabewa ya mtumba huku wakijua Sheria ya Manunuzi ya Umma hairuhusu Serikali kununua kitu cha mtumba kwa sababu hakina garantee wala kujua ubora wake na ndio kwa mara ya kwanza tangu nchi yetu iumbwe Serikali kununua kitu cha mtumba.
Mpaka leo 2022 inamalizika Wizara ya Ujenzi haijajenga hata Kilomita 1 ya barabara mpya ya lami licha ya fedha hizo kuwepo kwenye bajeti kila leo wanazungumzia kumalizia miradi ya JPM tu.
Maeneo yote hayo ukiyafuatilia kwa karibu ndiko ambako familia ya WATU WAZURI HAWAFI ilikowekeza nguvu kubwa kuvuna rasilimali za nchi na ndio chanzo cha kumdanganya Rais kwamba mawaziri hao ni watu wa karibu na JPM.
Lakini wanasahau kwamba Mh Samia Suluhu Hassan ni mtu wa karibu zaidi na JPM ndio maana aliamua kumpa nafasi kubwa kabisa ya Makamu wa Rais japo kuna propaganda kwamba JPM alishinikizwa na Kikwete kumuweka Samia jambo ambalo ukilipima halina ukweli.
Kwa sababu Kikwete alikuwa Rais kwa miaka 10 kama kweli Samia alimuona ni kiongozi mzuri angempa umakamu wa Rais katika kipindi chake ila JPM yeye ndio aliamua kumpa Mh Samia nafasi ya Makamu.
Mkaendesha Kampeni chafu Job Ndugai akaondolewa, IGP Sirro akaondolewa, Prof. Kabudi akaondolewa, Lukuvi akaondolewa, Polepole akaondolewa, Kalemani akaondolewa, Bashiru akaondolewa, Mwita Waitara akondolewa, Mwambe akaondolewa, Chamriho akaondolewa, RC Mwanza Injinia Gabriel akaondolewa, RC Mara Hapi akaondolewa, RC Simiyu Kafulila akaondolewa na wengine wengi Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi kama TRA, TPA, TANESCO na maeneo mengine mengi.
Sasa tunawauliza FAMILIA YA WATU WAZURI HAWAFI kampeni yenu ya SUKUMA GANG watanzania wameigundua kwamba mlilenga nini sasa mwaka 2023 ndio huo unakuja siku 365 mtaishije ikiwa progapanda mliyokuwa mnaitegemea watanzania wameshaijua.