Propaganda ya Sukuma Gang imeishia wapi?

Narudia kusema Rais Samia nafasi anayo kubwa sana ya kurekebisha makosa yake na akawa the best president kuwahi kutokea Tanzania.
Mkuu Mudawote , kwa vile Mama Samia sio malaika, ni binadamu, hivyo anaweza kukosea, unaonaje kama utamtajia makosa yake na kushauri the right thing to do, ili arekebishe awe the best president kuwahi kutokea?.

Ila makosa hayo, yawe ni makosa yake yeye kama Samia na sio yale makosa ya kukoseshwa na wasaidizi wake. Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
P
 
Sukuma gang iwepo tu..ilI Tanzania tupate maendeleo..

Bila hivyo ni business as usual..
 
Kwa sababu wewe ni member wa rukuma gang na responsibility kuwatetea katika social media na ku advance their causes.. Mfano mzuri uli support Uzi wa ndegebya mizigo KiA hata bila kuchunguza kwa umakini sana na ukajivisha joho la uzalendo. Lakini ukiingia youtube ipo clip yake juu yanujio wa ndege ile. Na habari zozote bazo zina undermine mama basi unakuwa unatafuna huku unapuliza..Move on guys jamaa yenu amefariki na siyo kama Yeye alikuwa ni baba wa familia ya kuwa amewacha USIA watoto wake lazima waufuate...na bahati mbaya hatorudi tena
 
kasome kwanza ule waraka wa prof shivj
 
Atafutwe C Musiba huenda anamajibu mazuru.!
 
SUKUMA GANG wapo na wanawasubiri 2025, CCM itapata Urais ila Wabunge iko kazi. akina Tulia,Msambatavangu, Mabula wa Nyamagana, Gwaji boy, Tarime Mjini na Vijijini, Arusha Mjini, Hai, Serengeti nk. wajiandae kuangalia kazi nyingine za kufanya
 
"Mimi na wenzangu tumepikwa vizuri na Mhe. Dokta Magufuli. Hakuna kitakachoharibika. Tutaendeleza pale alipoishia mwenzetu," alisema Rais Samia, Machi 19, 2021 wakati akila kiapo. Katika ujazaji maji wa JNHHP hizo shangwe zioiibuka baada ya Mhe. Rais ku appreciate alichokifanya mtangulizi wake. Na Rais amekuwq akisisitiza hakuna mradi wa kimkakati utakwama.

Tatizo ninalo liona ni watu wa hovyo tu kutaka kuonyesha kuna tofauti# Rais Samia na JPM damdam.🙏🙏🙏
 
Sure, ni hao akina Makamba na wanaomuandalia hotuba. Angalia, kwenye hotuba Dkt Magufuli jina lake halikuwepo kabisa, Rais Samia alichomekea baada ya shangwe kazaa kuibuka.
 
Disemba 22, 2022 wakati wanaJAZA maji Bwawa la Nyerere. alipotajwa JPM
Na hapo ni RUFIJI na watu waliokuwepo pale wote wamesafirishwa kwa uratibu wao maana pale ni porini huwezi kwenda mwenyewe kile kichaka chao cha Wasukuma kikachomwa moto wakabaki wanashangaa tu
 
Pascal Mayalla
MWAKA 2022, Familia ya WATU WAZURI HAWAFI ilitumia nguvu kubwa kumdanganya Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwenye mambo mengi ili kujitengenezea uhalali wa kukaa kwenye nafasi nyeti za uongozi huku wakijua hawana uwezo na nafasi hizo bali kutafuta masiahi binafsi.

Walitumia nafasi hiyo kumhadaa kuwa kuna kundi linaitwa SUKUMA GANG linamhujumu utawala wake kwa hiyo aliondoe kwenye nafasi za uongozi ili wao watawale nafasi zote nyeti serikali kurahisisha mipango yao.

Miongoni mwa viongozi waliotuhumiwa na familia hiyo kwamba eti wanamhujumu Rais Samia ni pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai na lengo la kumuondoa Ndugai ili familia hiyo ilitawale Bunge na kupitisha Sheria mbalimbali ambazo zitawabeba kwenye mambo yao binafsi ikiwemo biashara zao na miradi wenye manufaa nayo kama familia.

Medard Kalemani naye akaondolewa Wizara ya Nishati akapukutishwa na Uongozi wote akiwemo Katibu Mkuu na Watendaji wakuu wa TANESCO ili kufanikisha mambo binafsi ya familia hiyo tunayoyaona sasa.

Mradi mkubwa wa JNHPP ili uvurigike na pesa nyingi ziendelee kulipwa kwa familia hiyo ndio maana Waziri Makamba licha ya kufahamu kuwa wakati Rais Samia anaingia ulikuwa umefikia 52% lakini akaja na takwimu zake kwamba ulikuwa 37% ina maana fedha za 15% ya ujenzi zinakwenda kwenye familia. huku Mwigulu naye akisema ulikuwa 12%.

Dili ya Ruzuku ya mafuta ya bilioni 100 kila mwezi ambayo hadi leo hakuna mtanzania anayejua fedha hizo analipwa nani? ni moja ya manufaa wanayopata familia ya WATU WAZURI HAWAFI.

Wizara ya Ujenzi, Injinia Chamriho akaondolewa ili miradi mikubwa kama SGR, Meli ya MV MWANZA Hapa Kazi, Daraja la Kigongo Busisi nayo icheleweshwe ujenzi wake na iongezewe gharama za ujenzi kwa manufaa ya familia hiyo

Mradi wa SGR kuagiza mabewa ya mtumba huku wakijua Sheria ya Manunuzi ya Umma hairuhusu Serikali kununua kitu cha mtumba kwa sababu hakina garantee wala kujua ubora wake na ndio kwa mara ya kwanza tangu nchi yetu iumbwe Serikali kununua kitu cha mtumba.

Mpaka leo 2022 inamalizika Wizara ya Ujenzi haijajenga hata Kilomita 1 ya barabara mpya ya lami licha ya fedha hizo kuwepo kwenye bajeti kila leo wanazungumzia kumalizia miradi ya JPM tu.

Maeneo yote hayo ukiyafuatilia kwa karibu ndiko ambako familia ya WATU WAZURI HAWAFI ilikowekeza nguvu kubwa kuvuna rasilimali za nchi na ndio chanzo cha kumdanganya Rais kwamba mawaziri hao ni watu wa karibu na JPM.

Lakini wanasahau kwamba Mh Samia Suluhu Hassan ni mtu wa karibu zaidi na JPM ndio maana aliamua kumpa nafasi kubwa kabisa ya Makamu wa Rais japo kuna propaganda kwamba JPM alishinikizwa na Kikwete kumuweka Samia jambo ambalo ukilipima halina ukweli.

Kwa sababu Kikwete alikuwa Rais kwa miaka 10 kama kweli Samia alimuona ni kiongozi mzuri angempa umakamu wa Rais katika kipindi chake ila JPM yeye ndio aliamua kumpa Mh Samia nafasi ya Makamu.

Mkaendesha Kampeni chafu Job Ndugai akaondolewa, IGP Sirro akaondolewa, Prof. Kabudi akaondolewa, Lukuvi akaondolewa, Polepole akaondolewa, Kalemani akaondolewa, Bashiru akaondolewa, Mwita Waitara akondolewa, Mwambe akaondolewa, Chamriho akaondolewa, RC Mwanza Injinia Gabriel akaondolewa, RC Mara Hapi akaondolewa, RC Simiyu Kafulila akaondolewa na wengine wengi Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi kama TRA, TPA, TANESCO na maeneo mengine mengi.

Sasa tunawauliza FAMILIA YA WATU WAZURI HAWAFI kampeni yenu ya SUKUMA GANG watanzania wameigundua kwamba mlilenga nini sasa mwaka 2023 ndio huo unakuja siku 365 mtaishije ikiwa progapanda mliyokuwa mnaitegemea watanzania wameshaijua.
 
Ulivyomtaja lukuvi tu, nimejua wewe ni chawa
 
Ishu ya Sukuma GANG Samia hahusiki kabisa, hiyo ni mbinu ya Familia ya WATU WAZURI HAWAFI ili kuficha uzembe na uwajibikaji wao duni katika kazi pamoja na maslahi binafsi
 
Ishu ya Sukuma GANG Samia hahusiki kabisa, hiyo ni mbinu ya Familia ya WATU WAZURI HAWAFI ili kuficha uzembe na uwajibikaji wao duni katika kazi pamoja na maslahi binafsi
Rais wa JMT ni executive president, mkubwa jalala!, yeye ndiye kila kitu!, huwezi kusema hahusiki.
P
 
Ukitaka watu wasikuseme vibaya ukishakufa, dawa yake ni kutenda mema na haki. Mbona hakuna nyuzi za kumnanga Benjamin Mkapa japo wamekufa kwa tofauti ya miezi la 10 tu? Mbona Ali Hassan Mwinyi japo yuko hai watu hawamsemi?

Acheni watu waseme UOZO wote wa Magufuli ili liwe funzo kwa viongozi waliopo madrakani na watakaopata madraka wajifunze kutenda haki dhidi ya wanao watawala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…