Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Ni wapi mzalendo anapokuwa msaliti na mtetea anachokiamini anapoitwa Kibaraka, na ni wakati gani hayo maneno yanakuwa propaganda za kumtoa mtu kwenye mstari ?
Mpaka pale tutakapoanza kusikiliza ni nini kimesemwa na sio nani kasema, na vilevile tutakapotaka kujenga umoja na utaifa (ubinadamu) na sio kujenga usisi na wao, ndipo tutapata masuluhisho ya kudumu na sio kuhalalisha kile tunachokifanya kwa wakati husika..
Je kila mtu mwenye utaifa tofauti na sisi ni beberu ? na kila mwenye utaifa sawa na sisi ni mzalendo kama atakubaliana na sisi na akitupinga basi ni msaliti ? Je akikubaliana kifikra na beberu basi ni kibaraka? au inabidi asaliti nafsi yake na msimamo wake sababu tu unafanana na wa Beberu?
Ukiona mtu haukubaliani nae kifikra je ukubaliane nae ili uisaliti nafsi au utofautiane nae na uitwe msaliti? na hapo utakuwa unasaliti nini ikiwa anachokifanya unaona sio sawa? (na ni njia ipi utumie ili kupingana nae na usiwe msaliti).
Tukiendelea kuwagawa watu kwa kuwaita majina kwamba ni wasaliti au vibaraka sababu wana misimamo tofauti ni hatari kubwa ambayo itapelekea kukosa mawazo mbadala (watu kama Galileo waliitwa wasaliti na wasiofaa kwa kusimamia jambo ambalo kwa wakati ule lilionekana ni la uongo lakini kumbe likaja kuwa ni la ukweli) na hata hao ambao wanasimamia jambo hata kama sio kweli badala ya kuwaita wasaliti basi tuonyeshe kwanini wasemalo sio kweli na sio kuwaondolea utu wao na kuwapaka matope mbele ya jamii ili iwachukie (kwa kufanya hivyo tutajenga jamii ya watu waoga wakuuliza maswali na kukubaliana na kila jambo).
Vilevile hao tunaowaita wasaliti bado ni raia wenzetu binadamu wenzetu, wanachangia maendeleo kutumia kodi zao ambazo wote tunafaidika nazo, hivyo basi kuliko kuwagawa/kuwatenga/kuwatukana tubishane nao kwa hoja na sio matusi na kebehi, sababu ni wenzetu na huenda sisi tunaojiona tupo sawa ndio tunakosea.
Pia tukumbuke sio kila jambo linalosemwa na tunaowaona ni mabeberu/vibaraka au wasaliti ni baya na kila afanyalo mzalendo ni zuri, kwahiyo tukumbuke kuangalia ni nini kimesemwa na sio nani kasema. Na ukishakuwa kiongozi ni kiongozi wa wote hata wale ambao unaona ni wasaliti na njia njema ni kuwarudisha kundini kwa hoja na sio kuzidi kuwatenga na kufanya wengine wawatenge, hapo ni kujenga taifa lenye mpasuko na sio umoja.
Wasaalam.
By Mjamaa AKA KeyserSoze