Prophet Sanga 2022: Niliona mawe yenye moto,nikaona bendera ya Tanzania ikipita katika moto, ikakaa, tuombe

Prophet Sanga 2022: Niliona mawe yenye moto,nikaona bendera ya Tanzania ikipita katika moto, ikakaa, tuombe

Nabii aende kumuombea Pengo ..
Aache project yake ya kulazimisha Phili Mpango awe Rais mwaka 2025...

Mama ni dhaifu hatuwezi kuendelea kurejeshwa nyuma.Mama size yake ni Zanzibar Tanganyika ni kubwa sana inahitaji Kiongozi msomi kama Mpango na zaidi ya yote Mwanamke kutawala bado sana tunalazimisha tu.Huo ndio ukweli wa mambo.
 
"Nilikuwa katika maombi katika misitu ya Kibaha, Mungu aliniuliza unaona nini, nikajibu naona kitu, mawe ya moto mawe yenye moto yamegeuka kuwa mekundu yakija Tanzania" - Prophet Sanga.

"Mwaka 2023, huu ni mwaka gani!? Mwaka 2022, sasa mwaka 2023 kwenda 2024, zaidi mwaka 2023 naona watu kutoka magharibi ya Tanzania wakileta mtafaruku katika hili Taifa, hawa ni watu kutoka magharibi wakija katikati wataleta mtafaruku mkubwa" - Prophet Sanga.

"Nikaona moto, Mungu akasema namuona shetani akipanda kitu katikati yenu kutoka watu wa magharibi, magharibi ni wapi!? naiona bendera ya Tanzania ikipita katikati ya moto, tunatakiwa tuombe bendera hii isiungue, kama bendera hii ikiungua hakutabaki mwanasiasa ataebaki salama" - Prophet Sanga.

"Kabla sijaona bendera ya Tanzania ikipita katika moto, niliona mawe ya moto yakija Tanzania, na baadaye nikaona bendera ya nchi yangu ikipita katika moto" - Prophet Sanga.

"Kama tutaungana kama taifa tukaomba bendera ya Tanzania itapita katika moto bila kuungua lakini tusipoomba tutashuhudia kifo tena, unabii unapotolewa tunapaswa kuukubali na kuingia kwenye maombi" - Prophet Sanga.

"Sina mashaka na alichonionyesha Mungu, pitia historia yangu, kama hatutaomba unabii huu utawakumbusha, naiona bendera ya Tanzania ikipita katika moto na ikakaa, naviona vifo, Mimi na wewe tunaweza kusimama na kuomba, kama unajiona mwenye hekima unataka kuthibitisha, subiri ifike 2023 na utathibitisha" - Prophet Sanga.

"Kama hatutaomba na Mimi kama ulivyowewe nitasubiri kuona hili litokee katika ulimwengu wa kawaida baada ya kuona ikitokea katika ulimwengu wa kiroho" - Prophet Sanga.

"Kuna watu watakufa, wataobaki wataunda kundi la pembe tatu lenye pembe saba, nani anaweza kunionyesha pembe tatu yenye pembe sana" - Prophet Sanga.
Kwamba Sukuma gang watafanyaje? Maana ndio Wanaishi Magharibi 😁😁
 
Hawa wakinga wamechoka kufanya mauza uza ya mali wamehamia kwenye dini!! Mauchawi tu hayo ya akina Sanga
 
Mama ni dhaifu hatuwezi kuendelea kurejeshwa nyuma.Mama size yake ni Zanzibar Tanganyika ni kubwa sana inahitaji Kiongozi msomi kama Mpango na zaidi ya yote Mwanamke kutawala bado sana tunalazimisha tu.Huo ndio ukweli wa mambo.
we mjinga zaifu ni mamaako labda
 
..."Mwaka 2023, huu ni mwaka gani!? Mwaka 2022, sasa mwaka 2023 kwenda 2024, zaidi mwaka 2023 naona watu kutoka magharibi ya Tanzania wakileta mtafaruku katika hili Taifa, hawa ni watu kutoka magharibi wakija katikati wataleta mtafaruku mkubwa" - Prophet Sanga."....
Mungu atasingiziwa na jina lake kutumika sana for the political gain.

Tukitumia akili zetu vizuri, kuna point imebuniwa kitaalamna inaenda kuleta effect kubwa kwa Taifa.

Kuna jamii ya watu inatafutwa ubaya na kwa kupitia jina la Mungu wanaandaliwa kisaikolojia.

Ndani ntiti
Nje ntiti
 
Mama ni dhaifu hatuwezi kuendelea kurejeshwa nyuma.Mama size yake ni Zanzibar Tanganyika ni kubwa sana inahitaji Kiongozi msomi kama Mpango na zaidi ya yote Mwanamke kutawala bado sana tunalazimisha tu.Huo ndio ukweli wa mambo.
Mutaendelea tu kurejeshwa nyuma huyu munae mpaka 2030 Inshallah
 
Sawa pro tumeskia ..wakuelewa tumeidaka hii. Wale wakusubiri kinuke wajekutoa political na intellectual fact za mchongo nao pia wameipata na wameanza taaaarii.
 
KANISA LIPO KWA AJILI YA KUTETEA HAKI NA MASLAHI WATU WOTE KATIKA JAMII!

Wapendwa Watanzania!
Kuna watu wanalalamika kuwa sisi maaskofu tunamuandama Rais Samia kwa kuwa yeye ni Muislamu. Wanalalamikia matamko ya kupinga Mkataba wa Bandari wakidai kuwa tumefanya hivyo kwa kuwa Rais Rais Samia ni Muislamu. Wanasema hatukumpinga Rais Magufuli kwa kuwa yeye alikuwa ni Mkristo. Huo ni uwongo ambao usingestahili kujibiwa na Askofu. Lakini kwa kuwa kuna baadhi ya watu hawakufuatilia au wamesahau, basi tumeona tuwakumbushe.

Hakuna taasisi ambayo iliuandama utawala wa Magufuli kama Kanisa. Ushahidi wa haya ni:

1. Mwaka 2018 Kanisa Katoliki lilitoa Waraka wa Pasaka ambao ulimchukiza sana Magufuli

2. Mwaka 2018: Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) pia lilitoa Waraka wa Pasaka uliomchukiza sana Rais Magufuli.

3. Askofu Severine Niwemugizi wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Rulenge-Ngara aliandamwa sana kwa sababu aliionya serikali ya Magufuli.

4. Rev. Fr. Sabah (RIP) wa Kanisa Katoliki naye aliandamwa sana na utawala wa Magufuli.

5. Askofu Zakaria Kakobe wa Full Gospel Bible Fellowship aliandamwa sana na utawala wa Magufuli baada ya yeye kuukaripia.

6. Askofu Emmaus Mwamakula wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania aliandamwa sana na hata kuwekwa kizuizini baada kupinga udikiteta wa utawala wa Magufuli.

7. Askofu Dkt. Stephen Munga wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki aliandamwa sana kiasi cha kufikia hatua kukimbilia Afrika Kusini kwa matibabu yaliyookoa uhai wake.

8. Askofu Josephat Gwajima alipata utulivu baada ya kukubali kuhamia CCM lakini kabla ya hapo ilikuwa ni tabu.

Kwa hiyo, sisi maaskofu tumejenga utamaduni wa kuonya mamlaka kila zinapotenda mambo ambayo tunadhani hayana manufaa kwa jamii. Tunafanya hivyo kwa njia mbalimbali ikiwemo maonyo ya faragha, nyaraka, kutuma ujumbe maalum (delegation), nk.

Sisi tunaamini kuwa Mkataba wa Bandari umeingiwa na serikali ya Tanzania na wala sio na watu wa kabila au dini fulani. Kwa hiyo, sisi tumemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili Serikali isikilize maoni na kelele za wananchi wake tukiwemo sisi, wala hatujatoa shinikizo kwa Rais wa Kabila au Rais wa Dini.

Kama kuna makundi mengine yana hoja juu ya Mkataba wa Bandari hayajazuiwa kuwasilisha hoja zao. Katika kupinga mkataba sisi tulijikita katika kuchambua yaliyomo katika mkataba ambavyo. Tunatarajia kuwa makundi mengine nayo yatafanya hivyo badala ya kuangalia sura, nasaba, koo, kabila au dini.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 20 Agosti 2023, 07:45 Usiku
 
Nabii aende kumuombea Pengo ..
Aache project yake ya kulazimisha Phili Mpango awe Rais mwaka 2025...
Anafaaa sababu Dr. Mpango ana akili na ni msomi mzuri kabisa
 
Back
Top Bottom