Prosper Mnjari adaiwa kupotea baada ya kuchukuliwa Agosti 2 na watu waliojitambulisha TANESCO

Anaitwa Prosper Theonas Mnjari, anatafutwa alichukuliwa nyumbani kwake Chamazi Mbagala tarehe 2/8/2024 saa 5 asubuhi na watu waliojitambulisha Tanesco, toka walivyo mchukua simu ilizimwa haipatikani na hajaonekana, niwaombeni ukimuona au kuwa na Taarifa zozote kumuhusu tafadhali wasiliana na namba 0757677676/ 0719523522/ 0713990003/0766944200

Pia soma > Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”

---
Kijana PROSPER THEONAS MNJARI Mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mbagala,Chamazi

Ni dereva wa bodaboda kwa application ya "FARASI " anapaki kituo cha Tandika, anaishi na mke na watoto wa wawili.

(Wakati anachuliwa mtoto wake mdogo wa kike alilia sana) watekaji wakawa wanambembeleza (usijali Baba atarudi)

Ametekwa kwa kufuatwa na kuchukuliwa akiwa nyumbani kwake Chamazi alipopanga na watu waliojitambulisha kuwa ni askari pamoja na Watumishi wa TANESCO.

Walio omba namba ya LUKU akawapa,risiti ya kununua umeme mara ya mwisho akawapa,mwisho walimuomba waende naye ofisi ya Jirani ya Tanesco,kwamba nyumba ina deni kubwa sana.

Aliwataarifu nyumba si ya kwake anaomba awaunganishe na Mwenyenyumba,wakamwambia asijali ni jambo la dakika 5 tu.

Siku ya tarehe 2 August 2024 majira ya saa 5 : 00 asubuhi.

Walipofanikiwa kumchukua na kuondoka naye muda huohuo simu zake zote zilizima na hazijawahi kupatikana hewani hadi leo.

Ndugu zake wamemtafuta vituo vyote vya Polisi na Hospitali katika vyumba vya kuhifadhia maiti hawajafanikiwa kumuona ndugu yao

Wamefungua jalada la uchunguzi kituo cha polisi Mbagala na kupewa RB namba MBR/RB/6306/2024.

Kama ukimuona mahali popote tafadhali wasiliana na ndugu zake kwa kutumia simu namba 0757677676 au 0719523522 au 0713990003 au 0766944200
Ni hatari Sana.

Kwa vyovyote vile Watu wa kawaida wanaamini kwamba hao waliofanya hivyo ni "Watu wasiojulikana."

Jeshi la Polisi na Tiss lina kazi kubwa sana ya kufanya ili kujisafisha kutokana na uchafu huu mbaya kabisa.
 
Hivi inakuwaje mtu anakufuata nyumbani kwako, halafu kirahisi unakubali tu kuondoka nao kwenda kusikojulikana!!
 
Hili nalo ni tatizo lingine.

Hivi unawezaje kumwamini kirahisi mtu ambaye hujawahi kufahamiana naye kabla????
Elimu ya Usalama binafsi ni muhimu sana kutolewa kwa jamii kwa sasa.

Watu wanatakiwa wapewe elimu kuhusu masuala haya ya Usalama, e.g. abduction technics na namna ya mtu kuweza kuzi-detect pamoja na mbinu za kujihami
 
Kuwe na utaratibu kama.polisi akimchukuwa mtu, mjumbe ni lazima ajulishwe na sababu za kumchukuwa.
 
SHIDA NI CCM ITAWALE MILELE NA WAZANZIBARI WAENDELEE KUITAWALA TANGANYIKA NA KUIBA RASILIMALI ZOTE HADI WAWE KAMA DUBAI.

tume ya haki jinai ilitumia Kodi za WATANGANYIKA bure kabisa.

mama anaupiga mwingi.
Kwa ujinga huu unaposema Bora mshughulikiwe tuu
 
Kuna sheria inabidi kuundwa kuhusu umiliki wa silaha kama mfano wa umiliki simu.ili kupunguza haya ya kuchukuana bila sababu.
masau anakwambia wanajiteka
 
Kuwe na utaratibu kama.polisi akimchukuwa mtu, mjumbe ni lazima ajulishwe na sababu za kumchukuwa.
Mbona Sheria zilizopo zinataka iwe hivyo.
Sema tatizo ni Polisi wetu hawataki kutii Sheria, badala yake wao ndio wamekuwa vinara wa kuvunja Sheria za nchi na kujihusisha na vitendo vya Uhalifu.
That's why watu wengi sana wanaamini kwamba Watu ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo viovu vya utekaji Watu ni hao Askari Polisi
 
Mjiulize tu,huyo jamaa ni bodaboda hajishugulishi na siasa
 wala siyo mwanaharakati
kwanini atekwe...
je jamaa alikuwa ana shuguli nyingine ya ziada
je labda alikuwa anatembea na mke wa mtu
Je jamaa alikuwa mdhulumati

Hayo ndiyo maswali ya kuuliza

Ova
Huyo Jamaa nilikuwa naye short course y'a IT pale Don Bosco Temeke Mikoroshini 2018/2019 kipindi hicho alikuwa anakuja na pikipiki pia alikuwa ni Free lancer wa mitandao y'a simu.
Hajakaa kiboya ni mjanja flan WA mjini.
Nahisi yawezekana karusha mzigo WA watu
 
Uneona kazi sasa
Sahv kuna style imeingia
Watu wakidhulumiana,kutembea na mke wa mtu watu wanakuja wanakuteka wanaenda kumalizana na wewe

Ova
 
Nadhani ifike kipindi waruhusu watu wamiliki silaha tu kama Marekani ili hata mtu akija kwako ajipange kabisa, kuna uwezekano mkubwa jamaa alishindwa kuresist sababu walikuwa na silaha nzito, serikali inatakiwa hili iliangalie
 
Anaitwa Prosper Theonas Mnjari, anatafutwa alichukuliwa nyumbani kwake Chamazi Mbagala tarehe 2/8/2024 saa 5 asubuhi na watu waliojitambulisha Tanesco, toka walivyo mchukua simu ilizimwa haipatikani na hajaonekana, niwaombeni ukimuona au kuwa na Taarifa zozote kumuhusu tafadhali wasiliana na namba 0757677676/ 0719523522/ 0713990003/0766944200

Pia soma > Special Thread: Taarifa za Watu waliopotea au kuchukuliwa na “Watu Wasiojulikana”

---
Kijana PROSPER THEONAS MNJARI Mkazi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mbagala,Chamazi

Ni dereva wa bodaboda kwa application ya "FARASI " anapaki kituo cha Tandika, anaishi na mke na watoto wa wawili.

(Wakati anachuliwa mtoto wake mdogo wa kike alilia sana) watekaji wakawa wanambembeleza (usijali Baba atarudi)

Ametekwa kwa kufuatwa na kuchukuliwa akiwa nyumbani kwake Chamazi alipopanga na watu waliojitambulisha kuwa ni askari pamoja na Watumishi wa TANESCO.

Walio omba namba ya LUKU akawapa,risiti ya kununua umeme mara ya mwisho akawapa,mwisho walimuomba waende naye ofisi ya Jirani ya Tanesco,kwamba nyumba ina deni kubwa sana.

Aliwataarifu nyumba si ya kwake anaomba awaunganishe na Mwenyenyumba,wakamwambia asijali ni jambo la dakika 5 tu.

Siku ya tarehe 2 August 2024 majira ya saa 5 : 00 asubuhi.

Walipofanikiwa kumchukua na kuondoka naye muda huohuo simu zake zote zilizima na hazijawahi kupatikana hewani hadi leo.

Ndugu zake wamemtafuta vituo vyote vya Polisi na Hospitali katika vyumba vya kuhifadhia maiti hawajafanikiwa kumuona ndugu yao

Wamefungua jalada la uchunguzi kituo cha polisi Mbagala na kupewa RB namba MBR/RB/6306/2024.

Kama ukimuona mahali popote tafadhali wasiliana na ndugu zake kwa kutumia simu namba 0757677676 au 0719523522 au 0713990003 au 0766944200
SASA TANESCO WAMEPEWA LINI MAMLAKA YA KUKAMATA? HAPA LINATENGENEZWA ZENGWE ILI IONEKANE WANAOTEKWA WANATENGENEZA MATUKIO.
 
Polisisiem wameamua kubadili mbinu ya kujifanya tanesco ili wasijulikane.Mbinu za kishamba sana
 
Mjiulize tu,huyo jamaa ni bodaboda hajishugulishi na siasa
 wala siyo mwanaharakati
kwanini atekwe...
je jamaa alikuwa ana shuguli nyingine ya ziada
je labda alikuwa anatembea na mke wa mtu
Je jamaa alikuwa mdhulumati

Hayo ndiyo maswali ya kuuliza

Ova
Kama ni boda hiyo ya mke wa mtu inaweza ikahusu.
 
Back
Top Bottom