Prostate cancer

Prostate cancer

Echolima

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2007
Posts
3,824
Reaction score
2,079
Nina kaka yangu ambaye ana umri wa miaka 54 na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kushindwa kukojoa anawezeza kutoka usiku hata mara nne kukojoa.
Tatizo hapa kwetu kuna tatizo hilo limekuwa likiwapata wengi sana na wengine wanawekewa Mpira ya kuwasaidia kukojoa lakini daima wamekuwa hawaponi nimeshuhudia kwa macho yangu wazee sita wanafariki kutokana na tatizo hili kiasi ambacho linanisababisha nifikiri na kujiuliza Je?? kuna tiba kamili ya Ugonjwa huu????kama tiba sahii ya ugonjwa ipo naomba kujua naweza kumpeleka mgonjwa wangu wapi????? naomba msaada wenu.
 
inawezekana kinachowaua hao wazee moja kwa moja sio cancer bali ni UTI. UTI sio ugonjwa unaowapata wanaume kirahisi lakini huwapata zaidi wenye matatizo kama ya prostate cancer na hasa zaidi wale ambao huwekewa mipira ya kukojolea. wadudu hao hupanda juu na kushambulia figo. nashauri mkienda hospitali muongee na daktari wenu kuhusu hili swala ikiwezekana mpate dawa kwa ajili ya kujikinga na maambukizi (prophylaxis)
 
Nina kaka yangu ambaye ana umri wa miaka 54 na amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kushindwa kukojoa anawezeza kutoka usiku hata mara nne kukojoa.
Tatizo hapa kwetu kuna tatizo hilo limekuwa likiwapata wengi sana na wengine wanawekewa Mpira ya kuwasaidia kukojoa lakini daima wamekuwa hawaponi nimeshuhudia kwa macho yangu wazee sita wanafariki kutokana na tatizo hili kiasi ambacho linanisababisha nifikiri na kujiuliza Je?? kuna tiba kamili ya Ugonjwa huu????kama tiba sahii ya ugonjwa ipo naomba kujua naweza kumpeleka mgonjwa wangu wapi????? naomba msaada wenu.

Mkuu Echolima, kwanza naomba nikusahihishe: Sio kila tatizo la mzee kushindwa kukojoa ni prostate cancer. Kwa wanaume umri unavyozidi kusogea pia na ile tezi ya kiume yaani Prostate gland nayo inakuwa na inapokuwa kubwa huziba mkojo kupita na hivyo kulazimu kuwekewa mpira wa mkojo wakati madaktari wakiendelea na uchunguzi wa kuweza kujua kama ni kukua tu kea tesi hiyo yaani prostate hyperplasia ambayo sio kansa ama kuna dalili ya kansa ambapo ni lazima nyama za prostate kutolewa na kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kina, Histopathology. Sasa kusema wazee wengi wanakufa inawezekana pia wanafanyiwa upasuaji wa kuondoa tezi hizo wakiwa ni wathoofu ama wana matatizo ya kifua kwani hata dawa ya usingizi kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji ni hatari pia. Inashauriwa kabisa kila mwanaume anapofikisha umri wa miaka 45 na kuendelea lazima angalau amar oja kila mwaka kufanyiwa uchunguzi wa tezi hii ya kiume, prostate ili kuweza kubaini dalili za kansa mapema, hii inatakiwa ifanyike hospitali kwa dakatati kumpima na pia kuchukua kipimo cha damu kuangalia kichocheo kiitwacho Prostate Specific Antigen, PSA. Nikushauri kumpeleka kaka yako hospitali aweze kuchunguzwa kuna wataalamu wa magonjwa haya idara ya Urology, sijajua uko mkoa gani ili niweze kukuelekeza wapi unaweza kwenda, kwa kanda ya ziwa Bugando Hospitali, Kaskazini KCMC, Mashariki kanda za juu kuna Muhimbili, na juu kusini kuna Mbeya rufaa, hata Peramiho pia. waelimishe na wengine wanapofikia miaka 45 ni vyema kwenda kuchunguzwa sote tukumbuke kwamba saratani muda mabao inaleta dalili basi inakuwa imeshasambaa na ni vigumu kuidhibiti kwa upasuaji na dawa. Pia na kina dada tukumbuke kujichunguza matiti yetu walau mara moja kwa mwezi na uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi mara moja kwa mwaka.
 
Last edited by a moderator:
Wakuu nawashukuru sana sana kwa ushauri wenu mzuri ambao hata mimi nimeona ni kweli wazee wengi wanaowekewa mpira ya kuwasaidia kukojoa wanakufa kwa UTI maana wanakaa na mipira hiyo zaidi ya mwezi mmoja na wengine hata miwili hivyo kusababisha magonjwa mengine kuwavamia.
Pia nakushukuru sana MEASKRON kwa maelekezo yako ya kina mimi niko wilaya ya KAHAMA nategemea kumpeleka mgonjwa wangu pale Bugandoili aweze kupata vipimo sahihi lakini bado nina shaka kama kuna tiba ya uhakika maana nimeshuhudia wazee wengi hapa KAHAMA wamekuwa wakifa pamoja na kwenda Hospitalini na kutibiwa matibabu,Lakini nakubaliana na wewe yawezekana kama ulivyosema yawezekana kabisa kuwa wanachelewa kwenda Hospitalini kupata uchunguzi wa awali sasa wanapokwenda Hospitali wakiwa wanahali mbaya sasa ndiyo matatizo yanakuwa makubwa.Nashauri hata mimi Wanaume wote kuanzia miaka 46 wawe wamnapima hali zao za afya.
 
Hiyo kitu hapa kwetu ndio issue kubwa lakini nje ya nchi uchunguzi ni siku tatu au nne na operation ikibidi ndani ya same week kwahiyo katika kipindi cha wiki mbili uko fit labda maumivu kidogo kwa ajili ya kupona kidonda cha operation,nina mtu namfahamu alipata hayo matatizo akaenda Muhimbili apointment ya kumuona doctor ilikuwa ni baada ya miezi 6,ikabidi tumchangie pesa akaenda S.Africa,ndani ya wiki mbili kila kitu kilishafanyika na akarudi wiki ya tatu,mpaka sasa ni zaidi ya miaka 10 tokea amefanyiwa hiyo operation and he is doing fine.
 
Back
Top Bottom