Prostate cancer

Echolima

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2007
Posts
3,824
Reaction score
2,079
Nina mzee wangu ambaye ana tatizo la kibofu cha mkojo ni mzee miaka kama 63 hivi,ninampango wa kumpeleka Hospital akafanyiwe matibabu sahihi,wakati najiandaa kifedha naomba sana Mnisaidie nijue mgonjwa wangu huyu anatakiwa asile vyakula gani na ale vyakula gani wakati nasubiri kumpeleka hospitali.
Pia naomba mwenye mawasiliano na daktari mtaalam wa ugonjwa huu anipe namba zake
Nawasilisha.
 
Matatizo ya kibofu cha mkojo sio lazima yawe kansa. Prostate cancer ni tofauti.
Unaweza kumuona dr asheesh wa agha khan akakupa ushauri. Ila kama umeshathibitishiwa na vipimo kuwa ni kansa, basi dr ngoma anakufaa. Ana clinic mwenge lakini pia unaweza kwenda ocean road cancer institute.
Pole sana.
 
Anatakiwa kula chakula chochote kile.hakuna kinachozuia kula kwenye tatizo alilonalo.Uko mkoa gani ili watu wajue namna ya kukuelekeza?
 
kama uko dar ni bora umpeleke ocean road.Kansa haitibiwi kwenye private clinic, labda huyo daktari awe ameiba dawa za serikali na kuzipeleka huko
 
Nenda Tumaini Hospital na Onana na Prof Yongolo. Siwezi kuandika number yake hapa ila ninaPM namber yake sasa hivi.
 
Mimi niko wilaya ya kahama shinyanga,nashukuru kwa maelezo hayo maana kuna mtu alishanishauri kuwa asitumie vyakula vyenye sukari na asile nyama kwa wingi.
Anatakiwa kula chakula chochote kile.hakuna kinachozuia kula kwenye tatizo alilonalo.Uko mkoa gani ili watu wajue namna ya kukuelekeza?
 
Ni kweli hajapimwa na kudhibitika kuwa ana Prostate cancer lakini mimi nimeita hivyo baada kuona ana matatizo ya kukojoa mara kwa mara na wakati mwingine anakojoa matonematone tu.Nashukuru kwa mawazo hayo inabidi kwanza akapimwe ili idhibitike ni Prostate cancer au ni matatizo mengine ya kukojoa.
 
Mimi niko wilaya ya kahama shinyanga,nashukuru kwa maelezo hayo maana kuna mtu alishanishauri kuwa asitumie vyakula vyenye sukari na asile nyama kwa wingi.
Je, imethibitishwa kwamba ana kansa ya prostate? kama bado haijathibitishwa, ni vizuri akapelekwa bugando ili afanyiwe vipimo.
Tatizo la bugando, ni kwamba kuna Urologist mmoja tu, anaitwa Dr.Igenge.na hii ni baada ya daktari bingwa mzoefu wa siku nyingi kustaafu.
Sasa hospitali hii inahudumia wagonjwa kutoka kanda ya ziwa na kanda ya magharibi.Kumpata daktari huyu lazima umuone kwenye PRIVATE APPOINTMENT hapo hapo bugando.kwa kuwa clinic ya kawaida imejaa wagonjwa kibao, na madaktari waliopo sio madaktari bingwa, watapiga siasa na kumcheleweshea ndugu yako matibabu.
 

Mkuu, umempa ushauri mzuri sana.
 
Mimi ninachotaka ni matibabu ya uhakika kwa mgonjwa wangu niko tayari kwenda popote ili mradi mgonjwa wangu apate matibabu ya Uhakika no matter where.
 
Ninatibu matatzo hayo kwa100%kama bado ana tatzo hilomzee wako naomba uwasiliane nami,ntakusaidia 0759217720
 
Mkuu pole sana.nenda MZA muone dr mpelumbe kwenye private clinic yake.Unashuka stand ya misheni njia ya kwenda airport untembea kama unaenda isamilo kwenye hiyo njia ya lami ya kupanda jengo la kwanza kushoto kulia kwake ni kanisa simu ya nesi wa pale ni.0762502686-huyo dr specialist wa urology njia za mkojo.
 
Prostate means-is a male reproduct glands that it produce the fluid that carries sperm during ejaculation,it sorrounds urethra and the tubu through which urine pass out of the body.Prostate anlargent means;gland grown/became bigger,this happens to all mens theyget older in 50 year etc.when the glands grown it can press on the urethra and couse urination and bladder problems.Prostate anlargement is often called benign hypertrophy IT IS NOT A CANCER and IT DOES NOT RAISE YOUR RISK FOR PROSTATE CANCER.understod it IHAVE A MEDICAL OF ALL URINE PROBLEMS UNTIL NOW MORE THAN 50 PEOLES WAS HEALED,ITHINK THAT FEW TIME WE SHALL ENJOY TOSEE YOUR PARENT IN GOOD HEALTH.0759217720
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…