Proving the Bible (1): Carbon 14 Dating

Proving the Bible (1): Carbon 14 Dating

I think its not childish yo can just observe the demographic trends of the human species can answer it all
from year 2021 to 2022 there was an increase in no of people by 0.88% which is about 70,206,291 people in just one year now multiply that no by just 1000 years you get over 70 billion people and that is just for human species only which is not much efficient in reproduction rate.... assume those species that undergo asexual reproduction, the number might be unimaginable yet very real..
No no, we are not talking about the number of animals, we are talking about the number of animal kinds.

We can trap two people in a box and open it after a thousand years to find they've multiplied to a million people, that wouldn't be shocking because afterall they are still humans. But if we traped two humans and came to open the box after 6000 years and find a million humans, a million donkeys, a million rats and a million monkeys, now that would be shocking.

The thing with the ark story is that, they want us to believe that 6000 years ago only less than 7000 species entered the ark but they've now magically evolved into the millions of species we observe today in just that short span of time.
 
Mkuu nakumbushia hii...it's been weeks
Ok so where did all the "races" come from?

Kwanza there's only one race, the human race. This race business imeletwa thanks to the evolution hoax. We can all produce fertile children and the DNA differences between the different groups are actually insignificant.

Some scientists have us believe that since we look different then it must have taken thousands of years to produce the differences. This assumes that the differences between the groups are caused by "unique traits" in our genes which others lack.

But this isn't the case.

For example we have different skin colours which is simply caused by the amount of melanin. We all have the same genes for producing melanin, but we differ in the "potential" to produce melanin, caused by the variations in those genes that we all have.

The more the melanin, the darker the skin, and vice versa. Which is also affected by sunlight. The more time spent in the sun, more melanin produced.

Melanin is what causes different eye colors as well. More melanin, brown eyes. Little melanin, blue eyes.

Melanin is also what causes different hair colors. More melanin, black and brown hair. Less melanin, blonds and all. Red hair is a mutation in the genes producing melanin.

Another example, Asian eyes. What makes them different is that they have more fat around them. But we all have fat in our eyes. There's no unique gene for their eyes.

So all the information for the various differences were present in the eight people in the ark.

Since after some years their children eventually separated to different places isolating the gene pool, gene shuffling in the isolated gene pool caused the differences we see today, t
(the differences became more prominent with successive generations.)

Environmental adaptation also caused some characteristics to be more prominent in some areas.

For example dark skin blocks vitamin D absorption that's needed for calcium absorption for strong bones. So in areas with little sunlight, dark skinned individuals did not survive well. They developed diseases like rickets causing slow growth and bone fractures.

Certain groups lost the ability to have children of certain skin tones because they their groups lost the "potentials".

If we were to go back to the first groups before they separated, we might find a very different looking types of people! Mzungu skin with African hair, with Chinese eyes!

images (20).jpeg


Mwanzo 9:19 BHN

Hao ndio watoto watatu wa Noa, na kutokana nao watu walienea duniani kote.
 
How did all the species come from the 7000 animals?

So as we know according to Genesis, God created animals and plants in different kinds. Species (a man made concept whose definition is still being debated) are variations in a particular kind.

Kinds is a broader category, it may contain multiple species. For example horses, zebras and donkeys are different species of the equid kind.

Kinds are actually the boundaries within which animals can reproduce. A zebra can produce with a donkey (zonkey), a dolphin with a whale (wholphin), a tiger with a lion (liger), though some have lost the ability to produce with certain species of their kind (i.e reproductive isolation, caused by among other factors, geographical isolation).

(Check Baraminology: study attempting to classify fossils and living organisms according to their baramins i.e kinds).

So God instructed to keep seven pairs (i.e 14 animals) of the each clean kind, one pair of each unclean kind and seven pairs of every kind of bird.

The bible says every animal who breathed with nostrils died in the flood.

Noah did not have to bring insects because they could survive, they breath through their skin. He could've taken the delicate ones like butterflies and moths.

He also didn't take in marine animals, they could survive.

Now, there are fewer than 1.8 million recorded species. 98% of those are plants, fish species and non animals like bacteria, leaving out 34,000 land dependent animal species.

When estimating kinds in the ark, whenever data is insufficient, animals are split in different kinds rather than lumped together in one, thus keeping up with the worst case scenario.

It's likely also that Noah took young animals and smaller versions in the different kinds because they'd have taken less space, eat less, less waste, easier to manage, more resilient, and they'd have more time to reproduce after the flood.

So the researchers have estimated 1,400 animal kinds in the ark (and have prospects of decreasing the number with further research), accounting to less than 7000 land animals, from whose gene pool (genetic potential) produced the different variations of the kinds with different color, size, behavior etc.

For example these different species of the Ensantina salamanders in the Pacific Coast are separated by valleys, they look different but when they meet they interbreed, showing they are of the same kind.

images (16).jpeg


Brown bears and polar bears are classified as different species but when they happen to meet, they produce healthy offspring.

images (18).jpeg


African leopards and South American jaguars as well.

images (17).jpeg


Kuna Hawa Eastern na Western meadowlarks classified as different species. They are very similar but they rarely mate in the wild, but in the lab they do! They don't mate because they prefer different habitats and have different mating songs. But clearly they're of the same kind!

images (21).jpeg



Many "species" still hybridize to date, especially when brought to captivity, showing they're of the same kind.

To get the current number of species of land dwelling vertebrates from the original kinds in the ark, we need to only double the number, a practical process based on observable science.

Artificially bred animals (mostly dogs, cattle, hamsters) illustrate well the concept of genetic potential. It's an observable process of an exaggerated rate of variation (for example most dog breeds have been created in only the last 200years!)

images (19).jpeg
 
images (22).jpeg


About plants, the bible shows that 9months after the flood started, which is 4 months (128 days) after the ark rested on the mountain, a dove came back with a leaf, meaning plants had already started growing.

Remember the world (including mountains) didn't flood at once, it would have taken many weeks for all areas to flood.

Many seeds can still germinate even after being soaked in salt water for 140 days, an experiment done by the father of the hoax himself, Darwin!

Many plants could've survived on/as floating debris, which could be regrown after the water dried up, or experienced "asexual budding" i.e offspring plant growing from a piece of the parent plant.

Seeds could float with the floating animals carcasses too and later germinate (another experiment by Darwin).

Plus the ones they planted after they came out. The bible says he planted vineyards.

Are you satisfied with the answers?

If you've "more" questions not relating to these three, please don't ask!!!!
 
(usomaji wa dakika 14)

Tufanye hesabu!

Kabla hatujaanza, kuna maandiko haya matatu.

1 Wathesalonike 5:21

Pimeni kila kitu: Zingatieni kilicho chema.

Yohana 8:44

Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo. Siku zote alikuwa kinyume na ukweli. Hakuna ukweli ndani yake. Yuko kama uongo anaousema. Ndiyo, ibilisi ni mwongo. Na ni baba wa uongo.

Wakolosai 2:8

Angalieni mtu ye yote asiwateke kwa falsafa duni na potofu ambazo hutegemea mapokeo ya kibinadamu na mafundisho ya kidunia, na wala si Kristo mwenyewe.

Jambo kuu lililonifanya nitilie shaka biblia hapo zamani ni habari za historia. Tunajua historia ya Biblia inarudi nyuma takriban miaka 6000.

Lakini kadri muda ulivyoenda, wanahistoria na wanasayansi wa ki kidunia wanaoanza chunguzi zao kwa nadharia za kupinga biblia na Muumbaji walizidi kuja na "gunduzi" zao zenye kuelezea hali tofauti kabisa.

Imagine kusoma "mifupa ya miaka 200,000", "mabaki ya miaka 50,000,000", "miamba ya miaka 400,000,000,000",

Karibu kila kitabu na kila chombo cha Habari kinaripoti namba hizo!

Sasa Biblia inayoonyesha binadamu wa kwanza alikuwepo miaka 6000 tu iliyopita si inaonekana kituko!

View attachment 2646106

Wakristo walioshindwa kukana imani yao ilibidi waanze kuisoma biblia upya wajaribu kupatanisha hizo gunduzi na kweli zilizoandikwa kwenye biblia,

ndomana kuna wakristo wanaamini nadharia ya mageuzi, wanaona simulizi la Adam na Hawa ni fumbo na sio tukio halisi, wanaamini zile siku za uumbaji sio siku halisi bali ni mfano wa mamilioni ya miaka.

Lakini UKWELI ni kuwa njia zinazotumika kupima umri wa wa vitu vya zamani (Radiometric dating), vikiwemo mabaki ya viumbe hai, mawe na miamba, zote zinathibitisha dunia hii ni changa ya miaka elfu kadhaa tu, wala sio zee ya mabilioni ya miaka! Wala hakuna mabaki yenye umri mkubwa kiasi hicho!

Tuanze somo la jinsi ya kupima umri wa historia; tutaanza na Radiocarbon.

Kwanza kila kitu kimetengezwa na atomi (atoms), kama matofali yanavyotengeneza nyumba.

Kama ambavyo matofali yanatengenezwa na maji, mchanga na saruji, Atomi nazo zinatengenzwa na protons, neutrons na electrons.

Protons na neutrons zinakaa kwenye kiini. Electrons zinazunguka kiini.

View attachment 2646061

Idadi protons kwenye kiini ndo kinatokeza umbo tofauti (elements) lenye sifa za kipekee tofauti na maumbo mengine, Mfano sodium in protons 11, Oxygen ina 8, Nitrogen ina 7 n.k.

Idadi ya protons kwa kila element Huwa haibadiliki, na kwa kawaida idadi ya protons na neurons ni sawa kwa kila atomi.

Lakini kuna elements nyingine ambapo unakuta atomi zake tofauti zina idadi tofauti ya neutrons, lakini idadi ya protons ni ileile (Isotopes).

Mfano Carbon yenye protons 6 inaweza ikawa na neutrons 6, 7 au 8 (yaani Carbon 12, Carbon 13 na Carbon 14 respectively).

View attachment 2646065

Baadhi ya hizi isotopes huwa hazijatulia, zinajikuta zinatoa mionzi hadi zinabadilika kuwa element nyingine (radioactive decay).

Mfano Carbon-12 na Carbon-13 zimetulia. Lakini Carbon-14 haijatulia, itaanza kutoa mionzi mwishowe neutron moja inabadilika inakuwa proton, hivyo na umbo (element) linabadilika inakuwa Nitrogen-14.

Kuhesabu umri kutumia Carbon-14

Carbon-14 hupatikana duniani kutoka kwenye jua. Miale ya jua inakuja spidi na neutrons zake, inapiga anga letu lililojaa Nitrogen, Nitrogen ikiungana na hizo neutrons inatengeneza Carbon-14.

Carbon-14 na Carbon-12 zinaungana na Oxygen kutengeneza Carbon Dioxide inayotumiwa na mimea. Kwahiyo vyakula tunavyokula na hewa tunayopumua vina Carbon-14 na Carbon-12.

Viumbe hai vyote kwenye miili yao kuna uwiano wa C-14 na C-12 sawa na uwiano uliopo kwenye hewa (ambao kwa sasa ni C-14 moja kwa C-12 trillion moja).

View attachment 2646070

Kiumbe hai kikifa, kinaacha kupokea C-14 (kupitia chakula na hewa).

Na kwakuwa C-14 haijatulia (inageuka kuwa N-14), kadri muda unavyoenda itaendelea kupungua kwenye mwili.

Kwakuwa C-12 haibadiliki, na ndani ya mwili wa kiumbe kuna uwiano unaojulikana wa C-12 na C-14, tunaweza kujua kiasi cha C-14 kilichopotea kwenye mwili kwa kuhesabu kiasi cha C-12 kilichopo.

Wanatumia kifaa hicho kwenye picha kinaitwa Accelerator Mass Spectrometer (AMS) kinachopima uwiano wa Carbon hizi mbili.

View attachment 2646073

Sasa ili kupima umri, kwanza tujue hii C-14 inabadilika kwa kiwango/spidi gani.

Wanatumia half-life, yaani muda ambao inachukua kwa nusu ya idadi atomi iliyo kwenye Sampuli kupotea.

(Note: Kila umbo (element) ina half-life yake ambayo ni constant, na haitegemei idadi ya atomi kwenye sampuli ya kuanzia).

Half life ya C-14 ni miaka 5730.

Yaani nikichukua kopo nifungie humo idadi fulani ya C-14 pekeyake, baada ya miaka 5730 nitakuta nusu ya C-14 imebadilika imekuwa N-14. Baada ya miaka mingine 5730 nusu iliyobaki itabaki nusu yake tena (1 -> 1/2 -> 1/4 -> 1>8...n.k).

View attachment 2646079

Kwahiyo tayari tunakua tunajua:

- idadi ya C-12 iliyopo kwenye sampuli ya mwili uliokufa ambayo haibadiliki

- ratio ya C-12 na C-14 kwenye kiumbe hai, ambayo ni C-14 moja kwa C-12 trillion moja

- half life ya C-14, ambayo inafanya ratio ya C-12 na C-14 izidi kupungua, hivyo kadri ratio ilivyo ndogo ndo kadri muda mrefu ulivyopita baada ya kiumbe kufa.

Hivyo tunaweza kupima ni kiasi gani cha C-14 kilikuwepo kabla kiumbe hakijafa, hivyo kujua pia kilikuwa hai wakati gani uliopita.

Dhana moja muhimu

Kuna dhana moja (assumption) inayotumiwa kwenye haya mahesabu, ambayo ni kuwa uwiano wa C-14 na C-12 kwenye dunia ulikuwa sawa miaka yote.

Kama hii ni kweli, mahesabu yote ya umri kupitia kifaa cha AMS kilichotajwa huko juu, yanakuwa sahihi hadi takriban miaka 80,000 tu kwakuwa vyombo wanavyotumia watafiti kupima C-14 havina uwezo wa kutambua uwepo kiwango kidogo cha C-14 kilichobaki baada ya miaka hiyo.

Pia, kama dhana hiyo ya uwiano wa C-12 na C-14 sio kweli, basi mahesabu yote ya umri yanakuwa yamekosewa.

Ni jambo gani linaloweza kufanya uwiano wa C-14 na C-12 ubadilike?

Kama uwiano wa wa utengenezaji wa C-14 kwenye anga haulingani na kutolewa kwake (removal) hasa kupitia kupotea (decay), ratio ya C-12 na C-14 haiwezi kuwa sawa, hivyo kufanya ishindikane kutambua kiwango cha C-14 kilichokuwepo wakati kiumbe kimekufa.

Aliyegundua hii njia ya kupima umri kutumia C-14 (Dr. Willard Libby) ali assume uwiano huu wa utengenezaji na utolewaji wa C-14 kuwa sawa, na alitoa dhana hiyo kutoka kwenye dhana ya mageuzi, inayodhania kuwa dunia ina mabilioni ya miaka.

Dhana kwenye ulimwengu wa sayansi ni muhimu. Kama dhana ya kuanzia imekosewa, basi mahesabu yote yanayofuata hata kama ni sahihi bado yanatoa hitimisho lisilo sahihi.

Kwenye kazi zake huyo Dr. Libby alitambua kuwa uwiano wa utengenezaji na utolewaji wa C-14 sio sawa. Na hilo ilimsumbua kwasababu kama kweli dunia ina mabilioni ya miaka, umeshapita muda mrefu hivyo kunapasw kuwa na uwiano.

Mwenyewe alipiga mahesabu akaona kuwa kama dunia ilianza bila C-14 yoyote kwenye anga, ilipaswa kuchukua miaka 30,000 tu ili kutokee uwiano sawa Kati ya utengenezaji na utolewaji wa C-14.

Dr. Libby aliamua kupuuza tatizo hili kwenye mahesabu yake akasema itakuwa kuna kosa flani kwenye majaribio (experiments) lakini lazima uwiano uwe sawa.

Lakini ni KWELI kuwa uwiano wa C-14 na C-12 hauko constant kwasababu kuna C-14 nyingi zaidi zinazotengenezwa kuliko zinazopotea, wala sio kosa la experiment.

Inajulikana kuwa kiwango mahususi cha utengenezwaji wa C-14 (Specific Production Rate (SPR)) ni atomi 18.8 za C-14 kwa kila gramu moja ya Carbon kwa dakika moja.

Na kiwango mahususi cha utolewaji wa C-14 (The Specific Decay Rate (SDR)) ni kinajulikana, ni atomi 16.1 za C-14 kwa kila gramu moja ya Carbon kwa dakika moja.

Hii inamaanisha nini?

Inamaanisha kuwa, kama inachukua miaka 30,000 tu ili kufikia uwiano sawa wa utengenezaji na utolewaji na C-14 na bado hakuna uwiano, basi inawezekana dunia haina umri mkubwa kama wanamageuzi wanavyodhani.

Shamba la sumaku la Dunia (Earth's Magnetic Field)

Dunia imezungukwa na shamba la sumaku linalolinda dunia na mionzi hatari kutoka angani. Shamba hili linazidi kuishiwa nguvu.

View attachment 2646127

Kadri shamba hili linavyozidi kuwa na nguvu, ndivyo kiwango cha miale ya jua inayoingia duniani inapungua. Hivyo zamani wakati lilikuwa na nguvu zaidi, kulikuwa na kiwango kidogo cha utengenezwaji wa C-14 kuliko sasa.

Wachora historia ya shamba la sumaku la Dunia wanakubaliana na nadharia ya mwanafizikia anayetetea uumbaji Thomas Barnes kuwa nguvu ya shamba la sumaku la Dunia yetu imekuwa ikipungua nguvu miaka yote, hivyo haliwezi kuwa na zaidi ya miaka 10,000.

Leo hii, nguvu ya shamba la sumaku la Dunia imepungua kwa asilimia 10 toka mwaka 1845 ambapo mtaalam wa hisabati
Carl Friedrich Gauss alianza kulifwatilia.

Kama kiwango cha utengenezwaji wa C-14 ulikuwa mdogo hapo zamani, basi mahesabu yetu ya sasa yatadhani kuwa kuna kiwango kingi cha C-14 kimepotea kuliko kiwango halisi kilichopotea, hivyo kutoa umri mkubwa zaidi wa sampuli kuliko umri halisi.

Gharika la Noah

Gharika la Noah lingekuwa na matokeo gani kwenye kiwango cha Carbon?

View attachment 2646128

Gharika lingezika kiwango kikubwa sana cha wanyama na mimea hivyo kutengeneza nishati za ardhini kama mafuta na makaa ya mawe.

Kiwango cha nishati hizo zinazotokana na mabaki ya viumbe hai kilichopo leo, kinaashiria kulikuwa na idadi kubwa sana ya mimea kabla ya gharika.

Yaani kabla ya gharika, kulikuwa na kiasi cha Carbon ndani ya mimea na viumbe hai mara 500 zaidi ya ilivyo leo. Kimahesabu, hali hiyo ilipunguza zaidi kiwango cha C-14 na kupunguza zaidi uwiano wa C-12 na C-14.

Kikundi cha watafiti kilichoitwa Radioisotopes and the Age of The Earth (RATE) kilitumwa na mashirika yanayotetea sayansi ya uumbaji mwaka 1997 kufanya utafiti uliodumu miaka nane na kugharimu zaidi ya dollar milioni mbili.

Kilitumwa kutafuta data zinazopuuzwa au kufichwa na wanasayansi wanamageuzi na mahesabu yao.

Walifuatilia nadharia na taratibu zinazotumika kupima mawe, miamba na mabaki ya viumbe.

View attachment 2646110

Waligundua mengi ikiwemo:

1) Kuna C-14 kwenye mabaki ya viumbe ambayo kiumri hayakupaswa kuwa na C-14.

Kwamfano kuna njia wanamageuzi wanatumia kupima umri wa mabaki ya viumbe kwa kupima umri wa miamba ambamo mabaki hayo yamepatikana.

Mfano kuna sampuli ya mabaki ya mbao yalichukuliwa kwenye safu tofauti za miamba iliyopimwa na kukutwa na umri kati ya miaka 40,000,000 na 250,000,000, kwahiyo wanahitimisha kuwa na hizo mbao zina umri huo.

Lakini hata kwa kutumia njia yao ya C-14, walikuta sampuli hizo zina kiasi cha C-14 ambacho kinatoa umri wa mabaki hayo kuwa ni kati ya miaka 30,000 na 45,000 tu.

Watafiti wa RATE walipitia majarida ya wanazuoni waliotafiti kutumia C-14 na kukuta sampuli kibao (zaidi ya 40) za aina hiyo, yani sampuli za viumbe hai wanaodaiwa kuishi mamilioni ya miaka iliyopita lakini wana kiwango cha C-14 kingi badala ya kutokuwa nayo kabisa.

Watafiti wa RATE pia walichukua sampuli 10 za makaa ya mawe kutoka kwenye safu kadhaa za makaa ya mawe ambazo wanamageuzi walizipima na kudai ni za zamani sana (kuanzia miaka 65,000,000 hadi miaka 540,000,000). Walichukua tahadhari zote kuhakikisha haziwi contaminated.

Sampuli zote hizo zilikutwa na viwango vya kupimika vizuri kabisa vya C-14.

Ni jambo la kushangaza kwakuwa half-life ya Carbon ni fupi (miaka 5730) kwahiyo hakupaswi kuwa na kiwango cha kupimika cha C-14 baada ya miaka 100,000.

Kwa kutumia hesabu zao hizo hizo za C-14, sampuli zote kutoka safu zote za makaa ya mawe kuanzia ya miaka milioni 65 hadi miaka milioni 540, zote zilikutwa na takribani miaka 50,000 tu.

Ukitumia mahesabu ya halisi zaidi ukizingatia uwiano wa C-12 na C-14 kabla ya gharika la Noah, umri unapatikana kuwa ni miaka 5,000 tu.

Matokeo haya yanaonyesha umri wa safu zote za miamba ya chokaa haizidi miaka 100,000 (kwasababu ya uwepo wa C-14), na inaweza kuwa ndogo zaidi.

2) Ugunduzi mwingine wa kikundi cha RATE ni kiwango cha C-14 kinachopatika kwenye Almasi (Diamond).

View attachment 2646102

Wanasayansi wa kidunia kupitia njia nyingine za kupima umri (ambazo tutaona baadae pia nazo zinadhihirisha umri mdogo wa Dunia), walisema Almasi zina miaka mamilioni hadi mabilioni.

Watafiti wa RATE walichukua sampuli 12 za Almasi na zote zilikutwa na C-14 ingawa kwa kiasi kidogo kuliko sampuli za viumbe.

Hili limethiitishwa na watafiti wengine pia tofauti n RATE, kuwa Almasi zina C-14.

Huu ni uthibitisho tosha kuwa Makaa ya mawe na Almasi havina umri wa mabilioni ya miaka kama wanamageuzi wanavyodai.

Wazo la kuwa "wakati wa sasa ndio funguo ya kujua wakati uliopita" linawaletea shida wanaoamini kuwa dunia ni ya mabilioni ya miaka.

Namna mbadala ya kusoma data za C-14 tofauti na wanamageuzi wanavyodai ni kuwa: kulitokea gharika dunia nzima ambayo ndo imetengeneza safu za miamba na mabaki ya viumbe hai ambao sampuli zao zote bado zina C-14.

View attachment 2646113


View attachment 2646130

(Nimekuwa nikikusanya uthibitisho wa gharika. Very interesting. Uthibitisho ulio wazi kabisa kila mahali lakini ndo hivyo wanatafuta kila namna kutafuta interpretation ya ajabu ya data mradi wakwepe kutaja gharika la Noah. Wengine wanakubali kulikuwa na gharika Dunia nzima lakini sio ya kwenye biblia [emoji23])

Wakristo wasiogope Carbon 14, Carbon 14 iko upande wetu kutetea Dunia changa kabisa ya miaka elfu kadhaa tu iliyopita.

2 Petro 3:8

Lakini wapendwa msisahau neno hili, kwamba kwa Bwana, siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja.

Methali 3:5,6

Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atanyoosha mapito yako.


Makala kwa hisani ya Answers in Genesis.

Next time: Kuhusu njia wanazotumia kupima miamba kuwa mabilioni ya miaka (radioisotope dating na isochron dating) ambazo kiuhalisia TUMEPIGWA pia, na ukweli ni kinyume kabisa.
Uzi
 
Back
Top Bottom