BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Wakizungumza na Waandishi wa Habari, juu ya utambulisho na maandalizi ya Mkutano huo ambao kwa Tanzania unaenda kuwa wa kwanza kuandaliwa na Chama cha Maafisa Mahusiano Tanzania (PRST).
Katibu Mkuu wa PRST, Ndege Makura alibainisha kuwa mkutano huo unaofahamika kwa jina la ‘APA Tanzania 2022’ utafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa JNCC na katika Ukumbi wa Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency utakuwa na fursa mbalimbali kwa Tanzania, kwani itapokea wageni zaidi ya 400 kutoka Duniani kote.
"Hadi sasa washiriki waliothibitisha kushiriki ni 300 kutoka mataifa zaidi ya 23, lakini hadi kufika mwezi Mei, tunatarajia idadi hiyo ikaongezeka hadi kufikia 400 ya Washiriki, pamoja na nchi wanazotoka.
"Tutatumia fursa hii, kuitangaza na kuiuza Tanzania katika fursa zake zote ikiwemo kupitia Utalii," alisema Ndege.
Katika tukio la mikutano hii, tutakuwa na sehemu tatu;
Mkutano wa Kitaaluma kwa Wanafunzi wa Vyuo vya Uandishi wa Habari, Wanafunzi wanaosomea Mahusiano kwa Umma na wengineo.
Lakini pia kutakuwa na mikutano ya ndani ambayo wadau watajadili mambo mbalimbali na mawasilisho na kuja na majawabu na pia kutakuwa na tukio la Usiku wa Tanzania (Tanzania Night).
Ni mkutano wa kwanza ambao unafanyika Tanzania kuwakutanisha Wanataaluma wote Duniani Nchini Tanzania, mkutano huu ni kufuatia Kampeni ya Afrika kuleta mageuzi ya kimaendeleo katika kuisema Bara la Afrika kwa mazuri na mema mengine mengi ambayo tunaamini haijasemewa.
Pia huu mkutano mbali ya kuisemea Afrika, lakini unalenga zaidi kuitangaza Tanzania katika kuuza taswira ya nchi yetu kwenye nchi zingine mbalimbali ambao watakuja kwenye mkutano huu.
Aidha, alifafanua kuwa mikutano hiyo pia ni kuifanya Afrika kuwa washindani wa dunia, ambapo Mahusiano kwa Umma ni kichocheo cha ushindani. Aidha, tutaenda kufanya ziara ya utalii ikiwemo kwenda vivutio vya Zanzibar.
Na kuongeza kuwa, wanaendelea kufanya mazungumzo ili kuona wanashirikiana na wasimamizi wa Royal Tours katika kuwafikia wageni wengi kupitia mkutano huo.
"Mbali na mkutano wa Kitaaluma, Usiku wa Tanzania utakuwa maalum kuonyesha vivutio vyetu vyote vya Kitalii na masuala yote ya kuinadi Tanzania na tutashirikiana na wadau wote.
"Kwa upande wake Makamu wa Rais wa PRST, Mary Kafyome amesema wanatarajia katika mkutano huo, wanategemea Maafisa Habari na Taasisi zao kupata fursa ya kuweza kunadi maeneo yao.
"Taasisi na Idara mbalimbali za Serikali kama TFS, TAWA,TANAPA, TTB na wengineo, watapata fursa ya kunadi fursa walizonazo.
"Mkutano huu ni mwanzo na ni wa kwanza kwa sasa hivyo tunaamini wadau wakiwemo wanahabari na vyombo vya habari tutaendelea kushirikiana," alisema Mary Kafyome.
Ambapo aliwaomba Maafisa Mahusiano wa Tanzania kushiriki kwa mapana yao mkutano huo ilikuweza kuijifunza mambo mbalimbali ya namna ya kuinadi nchi.
Amesema kuwa Tanzania wamepata nafasi hiyo kutokana na vigezo mbalimbali ikiwemo masuala ya kisiasa lakini pia ukuaji wa masuala ya kitaaluma ya Mahusiano kwa Umma.
Naye, Kaimu Mwenyekiti wa PRST, Jossey Mwakasyuka alisema nafasi hiyo imepatikana kwa Tanzania, kutokana na kuwa na vigezo vingi kuliko nchi zingine.
Tanzania tunakuwa wa kwanza kufanya mkutano huu hapa Tanzania, kwa mara ya mwisho ulifanyika 2019. Hivyo kwa mwaka huu 2022, fursa hii tumepata sisi tuendelee kujitokeza kwa wingi kushiriki.
Mikutano hiyo ni muendelezo wa mikutano ulioanzishwa mwaka, 2015 kwa ajili ya kuisemea Afrika, ilikuwa ni kampeni ilioanzishwa na APA na vyama vingine vya kitaaluma.
PRST imeanzishwa mwaka 2017 na kuanza kazi mwaka 2018, huku ikiwa na wanachama mbalimbali.