PSG watinga hatua ya nusu fainali FIFA Club World Cup 2025

PSG watinga hatua ya nusu fainali FIFA Club World Cup 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia la Klabu la FIFA (#FIFACWC) mwaka 2025 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani katika mchezo wa robo fainali uliopigwa mjini Atlanta, Marekani.

Mchezo huo wa kuvutia ulijaa kasi, ufundi na ushindani mkubwa kutoka kwa matajiri hao wa Ufaransa dhidi ya mabingwa wa Bundesliga, lakini hatimaye PSG waliibuka kidedea na kuweka historia ya kufika hatua ya nne bora katika mfumo mpya wa mashindano haya.

Kwa sasa, PSG wanasubiri kujua watakutana na nani kati ya Real Madrid ya Hispania au Borussia Dortmund ya Ujerumani, ambao wanatarajiwa kuvaana usiku huu katika mchezo mwingine wa robo fainali utakaotoa mpinzani wa mwisho kwenye nusu fainali.
1751739957318.png

Mashabiki wa soka duniani kote wanasubiri kwa hamu kuona iwapo kutakuwa na vita ya miamba wa La Liga dhidi ya PSG au kama Dortmund wataandika ukurasa mpya kwa kuingia nusu fainali na kuchuana na wakali hao wa Ligue 1.

Nusu fainali nyingine tayari inajumuisha pambano la moto kati ya Chelsea ya England dhidi ya Fluminense ya Brazil, ambalo pia linasubiriwa kwa shauku kubwa. Kombe la Dunia la Klabu linaendelea kuwapa mashabiki burudani ya hali ya juu, huku kila dakika ikisukwa na historia.
 
Tena wametinga wakiwa na red card mbili
 
Simba wameingia robo fainali au wanamsubiri Real Madrid
 
Dogo Jamal Musiala kaumia vibaya sana, yaani mguu umegeuka, hapo naona miezi sita Yuko wodini.
 
Back
Top Bottom