PSRS interview questions (written, pract & oral)

PSRS interview questions (written, pract & oral)

Kabisa mkuu, tangazo limeanisha saa Saba mchana then interview inafanyika saa nne asubuhi..natamani kujua je ni kwa kanda na kada zote wamefanya hivi ??
Naona kweny Typing upande huo wa Mbeya alikosea ilikua Asubuhi. Maana kwa Mwanza inaonyesha ni Saa 1 Asubuhi na Tumefanya nao pamoja Yaani Afisa Tawala na Trade officer Chumba kimoja M 15 SAUT
 
Hapo unaanza highest education qualification to the lowest qualification Ila usitaje primary school unaishia sekondari
Duh hii ndo naiskia leo,mm naanzanga chin kuja juu then narelate as to why nimeapply for a job
But hzo ni kwa private companies as for utumish sjajua inakuaje
 
Mrejesho:


Kwakweli ni kwamba mimi kwa mara ya kwanza nilifika utumishi kwaajili ya written interview. Niseme tu nilifika Dodoma saa saba usiku kutokana na mazingira ya kusafiri kuwa magumu.Mara baada ya kufika sijuwa na sehemu ya kufikia,hivyo ilinilazimu nikeshe barabarani sehemu ambapo watu wapo muda wote.Asubuhi nilinunua maji nikanawa uso na kuchukua toyo mpaka UDOM.

Nilipofika nilihamaki uwingi wa watu! Nikasema Mungu hiki ni nini? Nikajisemea nimekuja kufanya nn huku? Nikiwa ninaonekana mshamba na upweke nisiye na hata rafiki wa kujadili naye chochote nikiwa nimesimama pembeni ya lecture theatre 1 kule college of business and education.


Baada ya muda walifika wasimamizi wakaanza kagua vyeti,nikafoleni nikaingia nikiwa na unyonge,ushamba,uchovu na usingizi mkubwa huku nikiwaza kuwa I am just trying.

Kweli paper ikaletwa,tukaelekezwa then tukafanya.Kiukweli ilikuwa NGUMUUUUUUUU! Ila inafanyika kwa wale wasomi na wafuatiliaji wazuri wa sera ya serikali katika utoaji wa mikopo kwa elimu ya juu.Ufanyaji wangu ulikuwa ni wa kujikongoja,huku nikihakikisha kila swali nagusa.


Nilijibu short and clear. Huku nikiwa nimekata tamaa. Ila kuna wanaume na wanawake haswaa waliomba hadi karatasi ya pili.Nilitoka na kuwahi stand nikapata chochote na kuanza safari ya kurudi kijijini kwetu nikiwa sina matumaini Yoyote.

Matokeo:

Leo nimeshikwa butwaa et nipo SELECTED FOR ORAL! Sikutegemea kabisa.Msimamo wangu ni kuwa nitarudi tena Dodoma kuwasikiliza maboss wakandaji live,nitakwenda KUJARIBU hiyo Oral.Sijawahi simama kwaajili ya Oral ila niwakute hukohuko hao wakandaji.Nikikosa basi,nitashukuru Mungu kwa kila kitu.


Kila lakher kwa woteeee mnaopigania huko,Mungu awafungulie njia.
Vp mkuu ulipita oral?
 
Recently utumishi hawatoi vitu nje ya ulichosoma darasani iwe written au Oral
 
Samahanii wakuu naomba aliyewahii kufanyaa interview utumishi kada ya diploma ya civil engineering anipee muongozo wa maswalii unakuaje???,,
 
Ukiulizwa ivyo inategemea na wewe uko vip? Nina maana hapo Kuna option kibao na wala hwanaga shida ya kujua unatokea ukoo gani na umezaliwa wapi

Kuna option hapa kama ulikuwa ni mfanyakazi huko nyuma na job kati ya equivalent zake ilikuwa experienced candidates is highly preferred!! Hapa unagusia elimu kidogo mfano itapiga position ya mwisho kwa level ya elimu yako for instance am a degree holder in ........utajuta kada yako na utaongea na udambwi kibao katika ufanyi kazi wako kama una experience utaelezea achievement katika carrier katika ufanisi wako umetatua ishu ....Nina maana ukisema una degree tayar washajua ulisoma msingi ukaenda sekondari labda ukaenda advance na chuo kabisa yaani imebeba kila kitu juu kwa juu kumbuka!! Pala washapitia documents zako za muhimu wanajua mpaka trh ya kuzaliwa so sio lazima ujieleze sana wanajua base katika carrier yako ulete ushawishi kidogo hawana shida na unatokea wapi sijui umezaliwa wapi.

Kingine we ni fresh graduate directly from the University hauna experience [emoji23][emoji23][emoji24]wala nn je point za carrier utazipata wapi? Yeap ushajitambulisha fresh mpaka wakujua una degree sehemu lakini kumbuka degree yako iko na mambo kibao ulipitita labda field Kuna project kama mmi tulifanya project mwaka wa pili kwenda wa tatu ,hata kama ukifanya volunteer ,hata research kama inarelate na kazi unaweza kumgusi kuonyesha uko fresh sehemu fulani ..gonga kingereza kilichoenda mbele japo unaweza kusita ila usirudie maneno jipangilie flow mwanzo mwisho .


Usipoteze mda unaweza kupewa dk 3 ukileta zile saijui I was born in ,am the third child in my family [emoji26][emoji26][emoji26]utaumia watakustopisha wakutoe nje.

Actually
 
H
Mmh haya mambo ya usaili hayanaga ata formula kikubwa ni kumuomba Mungu tu,wapo wanaojibu maswali kwa confidence na pengne kwa usahihi na wanakosa,only God
umesema point kubwa pale unaweza fanya vzuri ukaona umejibu fresh na kazi usipate mungu ndo mtoaji nasema hvyo kwa ushahidi wangu mm mwenyewe
 
  • 1.Mention components of research design

    2. Analysis of data in research is done in stages. Explain
  • Research proposal components

  • 1.What is the Criteria of good research?
    2.Define Ethnography research, Cross sectional research, Empirical research, Qualitative & Quantitative research.
    3.How research can be used to solve the problem?
    4.Difference between Research methods and research methodology
    5.Research design

  • Kama hiyo kazi ilihitaji degree programme zaidi ya moja Focus sana na Research.
    Sampling & its advantages, components of research proposal, Basics Types of Research, Research design, Approaches of data collection, (are few to mention) pitia na madesa ya class (muhimu sana haya).

  • Kama unajiandaa kufanya written interview utumishi jitahidi uwe na spidi ya kuandika maana wanaangalia sana ideas jibu maswali yote.

  • hakikisha kwa swali lolote litakalotokea una link na job description yako yaani kwa mfano wametaka uwaelezee background yako ya elimu Basi kwenye kuelezea uzoefu wako kwenye kada husika taja zile job description zote ulifanyaje ulipokuwa Field.hakikisha unazitaja ofisi au site ulizokuwepo

  • make sure unakariri zile job's duties and responsibilitie za vacancy husika kama zilihainishwa kweny tangazo zikariri mtu wangu utakuja nishukuru maana hazina kutunga

  • kikubwa wadau tujiandae bila kusahau express your self ilo la kwanza, kingine duties & responsibilities muhimu usikariri bali zielewe tu coz itakusaidia ikitokea umezisahau so utatunga kingereza chako mwisho utapata pointi ya kuandika, but kikubwa usisahau kusoma maswali yale ya class mfano wewe mtu wa akaunti basi pitia pitia vile vitu vidogo dogo mfano elements of balance sheets, principles of accounting n.k nina amini kila mtu ana uwezo wa kupata kazi utumishi tujiandae vzur ila tukumbuke na kuomba mungu muhimu sana
Yaan hapa.nimesikia mpka main yamecheza mzee
Hiyo nondomya research mzee mmmh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji419]Nimesoma uzi wote kwakwel nimepatwa na kitete alooo!!

Hapa nimetuma maombi kwa nafasi ya COMMUNITY DEVELOPMENT OFFICER GRADE II
Ninawaza kurudi kwenye notes, sina alooooo

[emoji837][emoji837][emoji837]DANGER
MWENYE maswali ya kada hiyo hapo aniambie
Hata hints zake wakuu

Ili mkeka ukitoka kama nitakuwepo nijue naset nuclear upande upi

Nawasilisha

MKANDAJI AKANDWE[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji419]Nimesoma uzi wote kwakwel nimepatwa na kitete alooo!!

Hapa nimetuma maombi kwa nafasi ya COMMUNITY DEVELOPMENT OFFICER GRADE II
Ninawaza kurudi kwenye notes, sina alooooo

[emoji837][emoji837][emoji837]DANGER
MWENYE maswali ya kada hiyo hapo aniambie
Hata hints zake wakuu

Ili mkeka ukitoka kama nitakuwepo nijue naset nuclear upande upi

Nawasilisha

MKANDAJI AKANDWE[emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Huwa inachukua muda gani hadi majina ya Usahili kutoka?
 
Back
Top Bottom