PSRS naombeni msaada wa ufafanuzi kwenye hili tafadhali

Mtoto wa Jadu

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2018
Posts
470
Reaction score
1,138
Kwanza hongereni kwa kufanya kazi yenu vizuri sana! Kwa kweli kwa kipindi hiki, kwa style hiyo ya interview imeondoa kubebanabebana!!

1. Kwa uzoefu wangu ni kwamba, huwezi kupata cheti cha NIDA bila kuwa na cheti cha kuzaliwa. Sasa mimi nikiwa nina cheti cha NIDA alafu cha kuzaliwa sina, iwaje nizuiliwe kufanya usahili?! Maana cheti cha kuzaliwa, si kipo ndani ya NIDA?

2. Kwenye usahili, mtu asiyekuwa na Transcript hakuruhusiwa kufanya usahili, licha ya kuwa na certified original certificates. Kuna ulazima gani wa Transcript na certificate kwa pamoja kwenye usahili? Na kwenye tangazo la kuitwa kwenye usahili, Transcript haikuorodheshwa kama document ya kuambatanisha!

Mwenye uelewa wa hayo naomba kueleweshwa!!
 

Attachments

  • IMG_20261018_202714.jpg
    107.2 KB · Views: 8
Mkuu ishu ya transcript ilinikuta usaili wa dec 2024, yani tulikuwa watu 45, na watu 44 walipata kazi katika kituo chetu, na mimi sikupata sababu nilitolewa kisa hicho cheti cha matokeo.
 
Sasa wewe umesema huwezi kupata cheti cha NIDA bila kuwa na cheti kuzaliwa. Sasa kama unacho na unajua wanakihitaji zingatia. Japo masuala ya vyeti vya makaratasi ni kero kwa zama hizi za teknolojia watu kuzurula na makaratasi ni aibu tu.

Suala la pili, transcript bila shaka ilikuwa post ya academia ambayo ni lazima wajiridhishe GPA kabla hujaingia. Cheti hakioneshi GPA mpaka transcript. Kama haikuwa academia post, basi una haki ya kukata rufaa kam unaweza
 
Njia za kupunguza watu izi wala sioni tatizo. Ni sawa na mnao kuja mmevaa ndala na jeans au t shirt kwenye interview
 
Mkuu ishu ya transcript ilinikuta usaili wa dec 2024, yani tulikuwa watu 45, na watu 44 walipata kazi katika kituo chetu, na mimi sikupata sababu nilitolewa kisa hicho cheti cha matokeo.

Pole sana aisee!

Kwahiyo kuna interview uliwahi kuhudhuria bila transcript, na ukaruhusiwa kufanya?

Au hili swala la transcript linategemea na mkaguzi wa interview siku hiyo?
 

Sikujua, kumbe kuna utaratibu wa kukata rufaa enhee!?

Lakini hata ukikata, watakupa kweli aptitude test yako na ufanye peke yako siku nyingine?

Kwenye issue ya transcript, hakika kwenye tangazo la kuitwa kwenye usahili hawaorodhesha kama ni doc inayohitajika.... Au mimi ndio nakosea? Unaweza angalia hilo tangazo hapo juu!!
 
wanachoweza kukusaidia ni kukupiga pini mazima 😃
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…