PSRS | Utumishi Wa Umma/Sekretarieti ya ajira angalieni hii

PSRS | Utumishi Wa Umma/Sekretarieti ya ajira angalieni hii

Niache Nteseke

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2020
Posts
2,162
Reaction score
2,616
Salaam kwenu wakuu.

Natumai muwazima wa afya kabisa. Well, suala lilionifanya mpaka kuanzisha topic hii ni kuhusiana na restrictions tunazokutana kwenye Ajira Portal.

Mmekuwa mkisisitiza sana kea waombaji wa nafasi za kazi kuhuisha (update) taarifa zao, hata wengine wamekuwa wakishindwa kufanya maombi ingawaje wametimiza vigezo vyote.

Mimi binafsi nimetimiza vigezo vyote katika kada yangu (DRIVER), lakini bado mmeninyima haki yangu ya kimsingi ya kuweza ku-apply kwenye nafasi mlizozitoa hivi punde.

Kunako Category ya PROFESSIONAL QUALIFICATIONS mmeweka kipengele cha kujaza Country, Institution Name, Course Name, Year From - To na sehemu ya MZIGOJUU (upload) kwa ajili ya kuweka leseni ya udereva.

Sasa basi, hapo kwenye Year From - To mmeweka miaka kwa nambari kabisa, yaani mtu hawezi kuandika mwaka kama anavyoandika Institution Name, mmeanza na mwaka 1978 - 2021.

Hivi tufikirie kwa haraka haraka tu Wakuu wa Utumishi, hivi kuna mtu anaweza kuwa na leseni ya mwaka 1978 wakuu...?

Hiyo sehemu sio ya kusema kuwa mtu alisoma mwaka huo HAPANA hiyo miaka ni muda wa kudumu kea leseni husika. Sasa hebu chukulia mtu ame-renew leseni yake mwaka huu na sasa hivi wanatoa miaka mkutano ina maana itaisha zaidi ya huo mwaka mliouweka hapo (2021), sasa hamuoni kuwa hili ni tatizo wakuu...?

Mi nadhani mngeanza japo kuweka mwaka 2015 au 2017 mpaka 2030 for future use. Ila mnapoanza mwaka 1978 - 2021 sidhani kama hii position mmetumia uweledi wenu vya kutosha wakuu.

Natumai mpo humu na mtalifanyia kazi suala hili, ili wenye sofa na vigezo kwenye kada husika waweza kupata nafasi ya kuweza ku-apply.

Niwatakie kila la heri kwenye majukumu ya kulijenga Taifa Letu. Shukran.

NAWASILISHA.


IMG_20211026_201847_882.jpg
 
Aisee malalamiko yamekuwa mengi kwa Ajira Portal ina mapungufu kadhaa ambayo yasipofanyiwa kazi haitaleta tija katika nyanja ya Ajira mkuu.
Wewe wasema hivo Ila sisi tuliopata ajira tunaona sawa mfumo uko vizuri tu wako very fair.kwenye oral interview omba bahati ya haiba yako kupendwa na mmoja wa panel member..pia maswali ya kuorodhesha orodhesha point nyingi tumia lugha ya English tu usitumie kiswahili hata kama wakikutaka ufanye hivo
 
Wewe wasema hivo Ila sisi tuliopata ajira tunaona sawa mfumo uko vizuri tu wako very fair.kwenye oral interview omba bahati ya haiba yako kupendwa na mmoja wa panel member..pia maswali ya kuorodhesha orodhesha point nyingi tumia lugha ya English tu usitumie kiswahili hata kama wakikutaka ufanye hivo

Aisee, mimi sipo huko kiongozi nilichokileta hapa ni huo mfumo wa Ajira Portal walivyouweka wala sijazungumzia interview japo nimekuelewa vizuri ila umetoka nje ya mada mkuu...!
 
Back
Top Bottom