PSSSF hizi Pesa za pole kwa wafiwa zinaendaga wapi?

PSSSF hizi Pesa za pole kwa wafiwa zinaendaga wapi?

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
62,101
Reaction score
38,487
Mkurugenzi
Polen na KAZI Bwana Yesu asifiwe na asllam alyekum

KUNA MSIBA umetutokea. Marehemu n member WENU

Wakati WA MSIBA akatokea NDUGU MMOJA na kusema Pssf wanatoa pole kwa marehemu mkirudi dar mwende kuulizia

Mzee akafika ofisini kwenu. Wana siku kama 43 tu. Akaambiwa zile pesa zote zimerudishwa ati alitakiwa kulalamikia kuziomba ndani ya mwezi mmoja.

Swali langu: tunajiuliza hivi natoka mkoani kuzika, nimefika naelekea ofisini kwenu mnasema hela imerudishwa imerudishwa.

Nani anazichukua hizi pesa za pole? Inasikitisha sana.

Angalieni huo utaratibu ni kutafunia dhambii ambazo haziwezi kusamehewa.

Mungu awabariki.
 
YAAANI MTU MWENYEWE KAFA NA 78 JAMANI MNAENDA KULAMBA PESA ZA POLE HII N LAANA SANA SANAA MUNGU ATAWAADHIBU KWA HILI
 
Huu n umafia unahisi sh ngapi zinapigwa kwa wanaopotiliza mwezi MMOJA na unajua ZINAENDAGA WAPI so bad
Hii n laanaa
Mwezi mmoja ni muda mfupi sana, hata 40 ya marehemu ( kwa wale wanaoamini) haijatimia. Wangeweka japo siku 60 (yaani zisizidi 60).
 
Mkurugenzi
Polen na KAZI Bwana Yesu asifiwe na asllam alyekum

KUNA MSIBA umetutokea. Marehemu n member WENU

Wakati WA MSIBA akatokea NDUGU MMOJA na kusema Pssf wanatoa pole kwa marehemu mkirudi dar mwende kuulizia

Mzee akafika ofisini kwenu. Wana siku kama 43 tu. Akaambiwa zile pesa zote zimerudishwa ati alitakiwa kulalamikia kuziomba ndani ya mwezi mmoja.

Swali langu: tunajiuliza hivi natoka mkoani kuzika, nimefika naelekea ofisini kwenu mnasema hela imerudishwa imerudishwa.

Nani anazichukua hizi pesa za pole? Inasikitisha sana.

Angalieni huo utaratibu ni kutafunia dhambii ambazo haziwezi kusamehewa.

Mungu awabariki.
Mafao ya Kifo yanatolewa kwa wategemezi wa Mwanachama aliyefariki dunia akiwa katika ajira kwa mujibu wa Ibara ya 36 ya Sheria 2 ya Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ya Mwaka 2018.

Masharti ya Ulipaji wa Mafao ya Kifo: -​

  • Awe Mwanachama Mfuko wa PSSSF.
  • Awe amefariki kabla hajatimiza umri wa kustaafu kwa hiari.

Utaratibu wa Malipo ya Mafao ya Kifo: -​

  • Iwapo Mwanachama aliyefariki hakuchangia miezi 180, wategemezi watalipwa mkupuo maalum (special lumpsum),
  • Mjane/mgane atalipwa asilimia arobaini 40%. Kama wapo zaidi ya mmoja, mafao yatagawanywa kwa usawa kulingana na idadi yao.
  • Watoto watalipwa asilimia sitini (60%). Kama hakuna watoto mjane/mgane atalipwa asilimia mia moja (100%). Iwapo wote hawapo, wazazi watalipwa asilimia mia moja (100%).
  • Ikiwa kuna mtoto/watoto wanaosoma nusu (50%) ya malipo yatalipwa kama mafao ya elimu na nusu itagawanywa kwa wategemezi.
  • Ikiwa kuna mtoto mwenye zaidi ya miaka 21 mwenye ulemavu wa mwili au akili atalipwa penesheni kwa maisha yake yote.
 
Back
Top Bottom