PSSSF ni miongoni mwa taasisi ambazo Rais wa JMT inabidi alifanyie marekebisho,
-manajimenti ya juu haiwajali wastaafu,
-watendaji wa mikoani wanaweza kupeleka dokezo au mapendekezo ya malipo, lakini watendaji/ mhusika wa Makao Makuu Dodoma,asifanyie kazi dokezo hilo miezi mitatu.
-Kuna mzee wangu amestaafu July 2019 lakini baadhi ya michango yake ilipelekwa PSSSF .amekuwa anafuatilia michango PSSSF mkoa wa Ilala tangu December 2029 bila mafanikio.
-Lakini tarehe 27July 2021, PSSSF mkoa wa Ilala,walipeleka madai yake PSSSF Makao Makuu Dodoma, mpaka sasa hivi bado hayajafanyiwa kazi .
-Amekwenda PSSSF mkoa wa Ilala na kuuliza status ya madai yake mpaka soli za viatu zimechakaa,
-hivi karibuni amefuatilia Madai yake kupitia dirisha dogo la maulizo(Enquiry) - ujumbe unafika kwa walengwa, lakini hajapata mrejesho.
-Wastaafu wanasumbuliwa na wanapata taabu Sana( nenda,rudi).
-Watumishi wa PSSSF wanakauli mbaya kwa wazee,hasa wazee waliochoka,wanaambiwa,mzee ninakusaidia,( badala ya kuona wanafanya au wanatimiza Majukumu yao),na wastaafu ndiyo mabosi wao,bila wanachama hawana kazi.
Mapendekezo
(1). Waziri Mwenye dhamana na taasisi hii nyeti,atupie jicho na amshauri Mheshimiwa Rais ipasavyo.
(2).Kwa watumishi wenye kauli mbaya wajirekebishe au wapangiwe Majukumu mengine (Back Office).
(3). Ninadhani uongozi wa taasisi hii hawatoshi au wajitafakari.
(4). Wateja wanapouliza taarifa zao kupitia dirisha dogo la maulizo,wawe wanapata majibu au ufafanuzi, otherwise hakuna haja ya kuweka dirisha dog (window) hilo.
(5).Kama ni kweli Serikali kuu,inadaiwa michango ya watumishi wake au mikopo,basi Ni busara michango Yao iwasilishwe ili wastaafu wapate stahiki zao,(kwa maana miaka 5 ijayo watumishi wengi wa umma wanastaafu).