Mkuu
Bruno Guimares , kwanza hongera kwa swali lako, najua japo ni swali la kawaida sana lakini the motive behind ni swali la kizalendo kwa Mtanzania mzalendo kujiuliza what will happen if anything happens, hivyo wewe na wengine kudhania kuwa kila kinachofanywa na rais wa JMT, wahusika wote ni watu wa PSU!. Its not!.
Rais wa JMT anaweza kuhudumiwa na mtu yoyote wa profession yoyote ya jambo husika, kazi ya PSU ni kuhakikisha tuu kuwa usalama upo na sio lazima wao PSU ndio wafanye kila kitu!.
Rais ambaye PSU wao wanafanya kila kitu ni rais wa Marekani, akisafiri nchi yoyote anatumia ndege maalum ya rais inaitwa Airforce One. Japo hiyo Airforce One ambayo ni ndege maalum ya Jumbo Jet , inaelezwa kuwa iko moja, lakini kila ikiruka inakuwa accompanied na Jumbo Jet nyingine mbili ambazo ni advance party, moja inabeba supplies, zikiwomo gari na vifaa vyote atakavyo tumia rais wa Marekani akiwa popote, na ya pili inabeba personal wa kufanya kila kitu, kuanzia wapishi, madereva hadi wafanyakazi wa kila kitu.
Siku Ile Obama kaja, walikuja na kila kitu chao, hadi magari, akalala Kilimanjaro Kempimski, hoteli nzima ilikodiwa, na kule presidential suite wali vacate staff wote wakaingia watu wao mpaka mpishi na msafisha choo!. Walitumia supplies zao hadi maji ya kunywa ni maji yao!.
Sisi rais wetu akisafiri nje anatumia ndege za mashirika ya ndege hivyo anaendeshwa na yeyote, hata ile Royal Tour alieendesha ile hot air balloon ni dereva wa baloon. Akisafiri kwa ATC anaendeshwa na Pilot wa ATC, akipanda chopa ni pilot wa chopa, hivyo akipanda boti ni pilot wa hiyo boti and not necessarily watu wa PSU!. Sio kila kitu ni PSU kuna vitu vingine PSU wetu hawawezi kuzuia mfano hili tukio nililo lizungumza hapa kuhusu usalama wa rais wetu, kwani PSU wetu waliweza?.
US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali?
Humo nilisema
Mbona hao PSU walishindwa kuzuia na mwisho wa siku...
Tuliishia kulia!.
P