PSU kuna manahodha wa meli/boti?

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,479
Reaction score
3,788
Rais Samia Suluhi Hassan leo alitumia usafiri wa boti kutoka Zanzibar kuja Dar Es Salaam.

Je, huko kwenye Idara ya Ulinzi wa Rais kuna ambao ni manahodha wa boti au meli? Ambapo ikitokea Rais anatumia usafiri wa maji basi waweze kumuendesha?

Maana safari za namna hizi za Rais kutumia usafiri wa maji huwa ni mara chache sana.

Na je, ikitokea watu wa namna hiyo hawapo huko idarani? Rais anaweza kuendeshwa na nahodha yoyote yule?
 
Kila idara imekamilika ndugu yangu hata ukitaka bodaboda wapo tu, Usalama wa Rais ndio Jambo la kwanza kwa idara yoyote Ile ya ulinzi na usalama duniani kwote, Hata hivyo sisi watanzania maombi yetu Ni makubwa Sana kwa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani, maana palipo na ulinzi wa mwenyezi mungu shetani hawezi kujipenyeza,

lakini pasipo na Mwenyezi mungu unaweza kuta hata walinzi wana pigwa na upofu wa kutotambua hatari, lakini mh Rais wetu yupo salama kwa maombi yetu watanzania pamoja na walinzi wa mh Rais wetu mpendwa nao wanalindwa na kuongozwa na Mwenyezi Mungu aliye mtoa njia na maarifa
 
Kwaiyo na wale abiria wengine walisachiwa au na wenye usalama?
 
Kwani marais wanapotumia usafiri wa ndege za abiria huwa hao PSU, ndio wanakuwa ma PILOT?!!
 
Inawezekana wasiwe kikosi maalum , lakini wakawa Tiss , angalia sana madereva wa mabasi ya mwendokasi , 90% wametoka kitengo tena kwa geresha ya Jw
 
Wapo mzee. Kuna hadi wa treni.

Sema ulivosema ilitokea hawapo sijajua kiusalama nadhani hataruhusiwa.
Hataruhusiwa Kama Royal tour unajua kwann hakupanda baloon
 
Na akipanda ndege anarushwa na nani?
 
Mkuu Bruno Guimares , kwanza hongera kwa swali lako, najua japo ni swali la kawaida sana lakini the motive behind ni swali la kizalendo kwa Mtanzania mzalendo kujiuliza what will happen if anything happens?!, hivyo wewe na wengine kudhania kuwa kila kinachofanywa na rais wa JMT, wahusika wote ni lazima wawe ni watu wa PSU!. Its not!.

Rais wa JMT anaweza kuhudumiwa na mtu yoyote wa profession yoyote ya jambo husika, kazi ya PSU ni kuhakikisha tuu kuwa usalama upo na sio lazima wao PSU ndio wafanye kila kitu!.

Rais ambaye PSU wao wanafanya kila kitu ni rais wa Marekani, akisafiri nchi yoyote anatumia ndege maalum ya rais inaitwa Airforce One. Japo hiyo Airforce One ambayo ni ndege maalum ya Jumbo Jet , inaelezwa kuwa iko moja, lakini kila ikiruka inakuwa accompanied na Jumbo Jet nyingine mbili ambazo ni advance party, moja inabeba supplies, zikiwomo gari na vifaa vyote atakavyo tumia rais wa Marekani akiwa popote, na ya pili inabeba personal wa kufanya kila kitu, kuanzia wapishi, madereva hadi wafanyakazi wa kila kitu.

Siku Ile Obama kaja, walikuja na kila kitu chao, hadi magari, akalala Kilimanjaro Kempimski, hoteli nzima ilikodiwa, na kule presidential suite wali vacate staff wote wakaingia watu wao mpaka mpishi na msafisha choo!. Walitumia supplies zao hadi maji ya kunywa ni maji yao!.

Sisi rais wetu akisafiri nje anatumia ndege za mashirika ya ndege hivyo anaendeshwa na yeyote, hata ile Royal Tour alieendesha ile hot air balloon ni dereva wa baloon. Akisafiri kwa ATC anaendeshwa na Pilot wa ATC, akipanda chopa ni pilot wa chopa, hivyo akipanda boti ni pilot wa hiyo boti and not necessarily watu wa PSU!. Sio kila kitu ni PSU kuna vitu vingine PSU wetu hawawezi kuzuia mfano hili tukio nililo lizungumza hapa kuhusu usalama wa rais wetu, kwani PSU wetu waliweza?. US/EU Walimtoa Saadam, Ghadafi na Mugabe? Je, wanapanga kumtoa Rais Magufuli madarakani? Watanzania wazalendo tutakubali?
Humo nilisema
Mbona hao PSU wetu walishindwa kuzuia na mwisho wa siku...
Si tuliishia kulia?!.

P
 

Ulinzi Mkali ni wakiduku wa N Korea. Inasemekana wana kitengo maalumu cha kulinda na kutunza haja ndg na kubwa. Hii ilisababishwa na Mosad kudukua hivyo vitu kwa Yesse Arafat na wakagundua ana Cancer itakayo muua baada ya miaka kadhaa.
 
Ulinzi Mkali ni wakiduku wa N Korea. Inasemekana wana kitengo maalumu cha kulinda na kutunza haja ndg na kubwa. Hii ilisababishwa na Mosad kudukua hivyo vitu kwa Yesse Arafat na wakagundua ana Cancer itakayo muua baada ya miaka kadhaa.
Duh...!.
P
 
Ulinzi Mkali ni wakiduku wa N Korea. Inasemekana wana kitengo maalumu cha kulinda na kutunza haja ndg na kubwa. Hii ilisababishwa na Mosad kudukua hivyo vitu kwa Yesse Arafat na wakagundua ana Cancer itakayo muua baada ya miaka kadhaa.
Story za huko kwenye vijiwe vyenu vya kahawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…