Psychic Powers: Ni nguvu za kufanya miujiza. Wengi wanazo bila kujitambua. Je, wewe unazo?



Hey aamahani,Upo Dar ? If yes ,hiyo bookshop inapopatikana hivo vitabu ipo wapi kwa Dar ,maana bookshop nyingi hawana hivyo vitabu .
 
Me Nina uwezo wa kujua mtu kitu anachoitaji kuniambia kabla hajatamka je nimiongoni mwa psychic power wakuu ?
 
mimi huwa nikimkumbuka mtu namuona pia nikiwaza kitu kinatokea na mara nyingine naota mtu fulani ni mchawi asubuhi niliemuota anakua ananiogopa au kunionea aibu...pia kuna siku nikiwa form two niliwahi kumuona mtu kwenye pembe ya mlango Lakin jion kuna mtu nilimsalim mara mbili hakuikia sasa je kuna uwezekano nilimsalim ndie yeye niliemuona kwenye pembe?
 
hii power inaitwaje
 
Mkuuu huwa nafuatilia sna huu uzi wako lengo ni kujifunza zaid ila umekaa kimya sana mkuu bado tunauitaji wako kaka
Mkuu ifa96, ni kweli huwa napotea, leo naurejelea na kujibu baadhi ya hoja.
Paskali
 
Hii kitu(threat) inaleta hamasa flan hivi. hembu ngoja kwanza niwaze nijue mimi nina nguvu zipi na zimenisaidiaje.
Mkuu Sijazaliwa, ni muhimu sana kujitambua. Watu wana nguvu ambazo ni mali, wamekalia tuu.
Paskali
 
Asante mkuu hii kitu ipo vizur hebu nifuatilie kwa ukaribu mijadala ya wadau humu ntajifunza kitu
 
Precognition, premonition and precognitive dreams - Perception of events before they happen.
Dah! hii huwa inanitokea mara nyingi tu, hata leo imenitokea.Leo nilienda duka moja nikakuta muuza duka anafanya usafi wa bidhaa zake ,kwa nlivyomuangalia nikamwambia mbona unafanya hivyo? au unataka kuvunja hizo bidhaa ili utumie mwenyewe? Haikupita dakika moja bidhaa yake moja ilidondoka kutoka kwenye shelf mpaka chini bahati nzuri haikuvunjika.....Muuzaji aliniambia nina mdomo mbaya.

Marafiki zangu ambao wanalijua hili labda ndio sababu baadhi yao wamekuwa wakinifuata na kuniomba ushauri niwaambie wafanye biashara gani au wafanye nini kuboresha biashara zao....wachache waliyafanyia kazi mawazo yangu na walifanikiwa. Kitu cha ajabu kwangu nikuwa sikuwa serious sana wakati nawaambia nini cha kufanya lakini baaadae walikuja kunipa feedback kuwa niliyosema walifanyia kazi na matokeo yalikuwa chanya.


  • Telepathy - Transfer of thoughts or emotions.
Nahisi Huu uwezo wa kusafiri kimawazo na kihisia ninao, nakumbuka ulikuwa unanisaidia sana kipindi nipo shule especially kwenye somo la Hisabati nakumbuka nilikuwa nasolve maswali magumu yalionishinda mchana darasani, nikiwa usingizini na nikiamka asubuhi nilikuwa narudia kufanya na kupatia vizuri kabisa.....kwangu mimi ilikuwa nikiamka kesho yake nilikuwa na solve lile swali ambalo ni gumu kama nimeshawahi kulifanya(Kama nafanya marudio).

Tukio lingine nnalo kumbuka kuna siku nikiwa shule ghafla kama picha hivi ikanijia akilini mwangu kuwa kuna jambo limetokea nyumbani....niliporudi nyumbani nikakuta ni kweli lile tukio limetokea exactly kama nilivyowaza.

Kusema ukweli mara nyingine naona ni msaada kwangu especially kwenye maswala ya mahusiano coz mara nyingi nilipokuwa kwenye mahusiano ambayo hayakuwa healthy nilijua mapema sana kuwa siko na mtu sahihi. Nakumbuka one of my ex aliwahi kuniambia kuwa najua vitu vingi mpaka anaogopa, kuna wakati alihisi nimemuwekea watu wamchunguze lakini haikuwa ivo taarifa zote nilizipata naturally even I can't explain it. She thought I was a lie detector coz my intuition says it all.

Tukio jingine nnalo likumbuka la hivi karibuni ni ajali ya gari ambayo nilipata mwaka mpya usiku 2017, nakumbuka wiki mbili kabla ya ajali nilishikwa na huzuni sana nlikuwa sijui kwanini lakini I felt it. Nakumbuka siku moja nikiwa na chat na mpenzi wangu nlimwambia mwezi huu utakuwa mgumu sana kwangu, sikujua kwanini nilisema vile...haikupita wiki nikapata ajali mbaya sana lakini bahati zuri gari tu ndo iliumia, mimi nilikuwa salama. Baada ya ajali ile nakumbuka siku ya 3 nilijihisi mwenye furaha na amani....ile hali ya huzuni ilitoweka ghafla.

NB: Sijawahi kufanya meditation ya aina yeyote ile na haya ni baadhi tu ya matukio ambayo nayakumbuka​
 
Njoo Central nakusubiri
 
Nimeshindwa
 
Dah vipi maswali ya Necta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…