Psychological crisis -Mgogoro wa kisaikolojia katika Maisha ya binadamu ni chanzo kikubwa cha msongo wa mawazo

DR HAYA LAND

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2017
Posts
32,386
Reaction score
83,431
Psychological crisis

Mgogoro wa kisaikolojia ni chanzo cha stress katika maisha .

Inaanza hivi.

Katika utafutaji -wengi tumejikuta tunasafiri , kutoka eneo moja mpaka eneo lingine.

Ila wengi tukifika katika baadhi ya maeneo bado tunakuwa na ile hali ya kuendelea kutamani ulipotoka .

Yaani hii inakuwa hivi UPO Arusha kikazi au kimaisha ila bado unaendelea kupawaza nyumbani kwenu Bukoba .

Kila wakati ukiona disappointment katika maisha yako Una -wish Kama ungekuwa nyumbani kwenu muda huo labda hayo yasingekupata .

Na kila ukiwaza kufanya uwekezaji katika mkoa mpya bado unasita sita ukifikiria kuwa unabidi kuwekeza Nyumbani kwenu aliyakuwa hata nyumbani kwenu haupo.


Na mwisho mwisho wa game unajikuta hakuna chochote umefanya .


Hivyo ukiwa upo sehemu unakaa au unategemea kutumia nusu ya maisha yako fikiria kukamatilia fursa katika hilo eneo wala usiilemaze akili yako kuwa nyumbani ni bora kuliko ulipo .


Hizi nchi zetu mfano Tanzania ukifatilia maeneo mengi yapo the same utofauti uliopo ni majengo , recreation place Ila kimaisha ni the same .


hivyo ni muhimu kuchagua sehemu bora ya Ku-settle kimaisha na kuendelea na uwekezaji .


Ukiangalia wazee wengi ambao hawana Nyumba ,Shamba wala ardhi mjini , ujue walianza hivyo kuwa hawawezi kununua ardhi mjini na walipiga hesabu kuwa wakizeeka watarudi nyumbani

Na mwisho wame-lose both games home and away

Maisha ukiyapangilia unaweza kuishi dsms Kama upo bukoba na ukaishi bukoba Kama upo DSM .

Mgogoro wa kisaikolojia ni mbaya unaweza kukufanya ukaamini mke wa jirani ni mzuri kuliko mke wako na jirani yako akaamini hivyo hivyo at the end utakuwa ume-chase nothing.

Kufanya maamuzi ukiwa na nguvu na uwezo ni jambo jema ukitoka sehemu sahau habari za huko. For a while and focus with ur life .
 
Kufanya maamuzi ukiwa na nguvu na uwezo ni jambo jema ukitoka sehemu sahau habari za huko. For a while and focus with ur life .💪🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Hata wazungu walitoka bara moja hadi bara jingine huku wameacha familia zao na waliwekeza mbali na nchi zao.

Nyumbani kupo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…