Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
S.hikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Ndugu zangu watanzania;
Rais Magufuli angeweza kutoa msamaha kwa wafungwa wachache tu (MTWARA PEKEE) ili kuweza kuenzi matendo mema, hekima pamoja na busara za mzee Benjamin William Mkapa.
Kwa kawaida Mh. Rais hutoa msamaha kwa wafungwa wakati wa maadhimisho ya sherehe za kitaifa kama uhuru, muungano, nyerere day, karume day, n.k Kwangu mimi binafsi ninaona siku ya leo ya terehe July 29, 2020 ni siku ya kitaifa ya mzee Mkapa kama mtu aliyekuwa mkuu wa nchi kwa muda wa miaka 10 mfululizo.
Simaanishi kwamba kila anapokufa mwanasiasa msamaha unapaswa kutolewa, hapana, bali mtu aliyekuwa kiongozi mkuu wa nchi sio mtu wa kufanana na mlalahoi kama Infantry Soldier.
Nimeamua kuandika hivi kwa maana kwamba ninatambua kuwa suala hili halipo kisheria, kikatiba wala kitaratibu huko serikalini, lakini watanzania waishio mtwara wanahitaji kupatiwa mkono wa shukrani. Mkoa ule wa Mtwara, Wilaya ya Masasi pamoja na kijiji cha Lupaso wametutolea mzalendo wa kweli, jasiri na shujaa wa taifa letu kwa kipindi chote cha miaka 82 aliyopata kuishi hapa duniani.
Licha ya kwamba alikuwa ni Rais wa Tanzania kwa miaka 10 ya uongozi wake, lakini pia mkoa wa Mtwara umetupa mtu aliyejali pia ushirikiano, uhusiano mwema pamoja na utengamano wa nchi yetu na mataifa ya jirani pamoja na ndugu zetu wengine wa bara zima hili la Afrika. Mkapa alikuwa ni mwana halisi wa afrika (A TRUE SON OF AFRICA)
Alikuwa amejitolea katika ushirikiano wa kikanda pamoja na ule wa Kusini mwa jangwa la sahara (South-South Cooperation), ikiwa ni pamoja na kupatanisha katika mizozo ya kivita pamoja na ile ya kisiasa katika nchi mbali mbali za Kiafrika, ambapo alifanikiwa kuja na suluhisho za Kiafrika kwa shida za Kiafrika (African solutions to African problems).
Alikuwa sehemu ya Jopo la Jumuiya ya Waafrika waliojulikana (AU Panel of Eminent African Personalities) ambao waliingilia kati mzozo wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 nchini Kenya ambao ulisababisha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ilileta amani na utulivu nchini humo.
Kulingana na uimara wake katika medani ya siasa za kimataifa na diplomasia na kama mzee wa mwenye busara iliyotukuka katika taifa, Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) ulimteua kuwezesha Mazungumzo ya amani ya nchini Burundi ambayo yalileta pamoja serikali na makundi mbali mbali ya upinzani katika Jamhuri ya Burundi kati ya mwaka wa 2016 na 2018, na kufanya juhudu za makusudi juu ya namna bora ya kupata njia ya kutoka kwenye mzozo ule wa kisiasa.
PUMZIKA KWA AMANI MZEE MKAPA. VITA UMEIPIGANA NA MWENDO UMEUMALIZA BABA YETU. MUNGU AKUPE PEPO ILIYO NJEMA MZALENDO MWENZANGU.
OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO***