Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
asante kwa kuandika Jamiiforumsni kutokuheshimu utawala wa sheria ni wazo la kimuhemuko zaidi
Alizaliwa Mtwara. Yeye ni zawadi ya watanzania kutoka MtwaraKwani huyu alikuwa ni rais wa mtwara?
Wananchi wote ni specialRais mstaafu ni mtu special sana kwa taifa
Sawa kaka mkubwaWananchi wote ni special
Kila jambo lina wakati wake. Mbona Nyerere alipokufa hakukuwa na Jamiiforums ila sasa wakati wa kifo cha mzee Mkapa ipo?Mbona nyerere alivofariki mkapa hakuwaachia wafungwa wa Butiama.
Sent from my TECNO CX Air using JamiiForums mobile app
Acha mihemko we! Mkapa hakuwa rais wa Kanda, na Wala Magu sio rais wa kanda! Aliamua kusamehu, Tena hapo ni siku ya Uhuru, 9 Dec, anaweza kutoa msamaha kwa wafungwa nchi nzima wenye vigezo!Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Ndugu zangu watanzania;
Rais Magufuli angeweza kutoa msamaha kwa wafungwa wachache tu (MTWARA PEKEE) ili kuweza kuenzi matendo mema, hekima pamoja na busara za mzee Benjamin William Mkapa.
View attachment 1520786
Kwa kawaida Mh. Rais hutoa msamaha kwa wafungwa wakati wa maadhimisho ya sherehe za kitaifa kama uhuru, muungano, nyerere day, karume day, n.k Kwangu mimi binafsi ninaona siku ya leo ya terehe July 29, 2020 ni siku ya kitaifa ya mzee Mkapa.
Nimeamua kuandika hivi kwa maana kwamba ninatambua kuwa suala hili halipo kisheria, kikatiba wala kitaratibu huko serikalini, lakini watanzania waishio mtwara wanahitaji kupatiwa mkono wa shukrani. Mkoa ule wa Mtwara, Wilaya ya Masasi pamoja na kijiji cha Lupaso wametutolea mzalendo wa kweli, jasiri na shujaa wa taifa letu kwa kipindi chote cha miaka 82 aliyopata kuishi hapa duniani.
Licha ya kwamba alikuwa ni Rais wa Tanzania kwa miaka 10 ya uongozi wake, lakini pia mkoa wa Mtwara umetupa mtu aliyejali pia ushirikiano, uhusiano mwema pamoja na utengamano wa nchi yetu na mataifa ya jirani pamoja na ndugu zetu wengine wa bara zima hili la Afrika. Mkapa alikuwa ni mwana halisi wa afrika (A TRUE SON OF AFRICA)
View attachment 1520788
Alikuwa amejitolea katika ushirikiano wa kikanda pamoja na ule wa Kusini mwa jangwa la sahara (South-South Cooperation), ikiwa ni pamoja na kupatanisha katika mizozo ya kivita pamoja na ile ya kisiasa katika nchi mbali mbali za Kiafrika, ambapo alifanikiwa kuja na suluhisho za Kiafrika kwa shida za Kiafrika (African solutions to African problems).
Alikuwa sehemu ya Jopo la Jumuiya ya Waafrika waliojulikana (AU Panel of Eminent African Personalities) ambao waliingilia kati mzozo wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2008 nchini Kenya ambao ulisababisha kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo ilileta amani na utulivu nchini humo.
Kulingana na uimara wake katika medani ya siasa za kimataifa na diplomasia na kama mzee wa mwenye busara iliyotukuka katika taifa, Mkutano wa Wakuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) ulimteua kuwezesha Mazungumzo ya amani ya nchini Burundi ambayo yalileta pamoja serikali na makundi mbali mbali ya upinzani katika Jamhuri ya Burundi kati ya mwaka wa 2016 na 2018, na kufanya juhudu za makusudi juu ya namna bora ya kupata njia ya kutoka kwenye mzozo ule wa kisiasa.
PUMZIKA KWA AMANI MZEE MKAPA. VITA UMEIPIGANA NA MWENDO UMEUMALIZA BABA YETU. MUNGU AKUPE PEPO ILIYO NJEMA MZALENDO MWENZANGU.
View attachment 1520770
OUR MOTTO: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Msaada Please: Ninaomba kuonana na ndugu Athumani Kihamia
Ni wapi nimeandika kuwa Mkapa alikuwa ni Rais wa kanda?Acha mihemko we! Mkapa hakuwa rais wa Kanda,
Magu ndio nani tena huyu?Magu sio rais wa kanda!
Hiyo haiwezi kuwa faida kwa wana Mtwara ,ingekua kama angetangaza kufanya kitu kinachogusa jamii moja kwa moja kama kuwajengea kitu kitakachoongeza ajira kwa vijana ,labda ndio ungeita kwamba ni faida za wana Mtwara ,sasa kumwachia mfungwa aliye kutwa anabaka hii inamsaidiaje mwana Mtwara?Zawadi kwa watu wa Mtwara
Ninatambua fika suala hiliAliamua kusamehu, Tena hapo ni siku ya Uhuru, 9 Dec,
Anaweza pia kutoa msamaha kwa wafungwa wa magereza ya Mtwara kwa wenye vigezo kama sehemu ya zawadi ya mkono wa shukranianaweza kutoa msamaha kwa wafungwa nchi nzima wenye vigezo!
Du, kwa Nini Mtwara tu!?Anaweza pia kutoa msamaha kwa wafungwa wa magereza ya Mtwara kwa wenye vigezo kama sehemu ya zawadi ya mkono wa shukrani
Kwanini Mkapa alizikwa Mtwara na sio Kigoma wakati yote ni Tanzania?Du, kwa Nini Mtwara tu!?
Kama thread hii inakukera ondoka. Kwani ni lazima uisome?
Hiyo tu inawatosha Mtwara! Angeweza zikwa Far, Kushoto, au Dom!Kwanini Mkapa alizikwa Mtwara na sio Kigoma wakati yote ni Tanzania?
Kwanini azikwe far wakati sio kwao?Angeweza zikwa Far, Kushoto, au Dom!
Thanks for commenting on JF@Nisiisome???---Ningejuaje kama haina mantiki bila kuisoma??!!---- dogo, ukiweka andiko lolote ndani ya Jf tayari hilo linakuwa ni mali ya wana jf wote na ni hiyari ya member mwenyewe atoe maoni au asitoe juu ya hilo andiko.