Salamu zenu wana JF.
Leo naomba tuzungumzie Public Transport kati ya majiji haya mawili yaani Dar es salaam na Nairobi.
Nawaomba tulete habari zenye references, hususani picha na link zile za kuaminika.
Mimi nitajitahidi kuleta taarifa kutoka dar es salaam maan ndio naishi mda mwingi.
View attachment 435896
Sasa nitaanza kwa aina ya usafiri uliopo dar es salaam
1. Train
2. Usafiri wa majini-Kivuko(Pantoni)
3. Bajaji
4. Pikipiki (Boda boda)
5. Taxi
6. Daladala
7. BRT - Dar Rapid Transit
8. Usafiri wa Boats kwenda kwenye visiwa vya Dar es Salaam
Nitaanza kuelezea usafiri baada ya usafiri.
Nawaomba na nyie wenzetu (Watani zetu) Toka huko Nairobi mtuletee usafiri wenu.
Hii ni kwa faida ya wale wanaosafiri.
Kejerei, Vijembe na kutoa povu lako unaruhusiwa.
Karibu
Hana cha kuonesha ndio maana anaharibu Uzi. Mpuuze na endelea kutujuza.Wewe lengo lako ni kuharibu. Ok
Wewe endelea tu lakini sio poa
Ni ushamba huo.
Bila shaka wewe ni kitengo cha UVCCM huo usafiri umeshatumia ukaona raha yake?
hiyo treni ungebahatika kuiona leo namna ilivyo, nadhani ungepata kigugumizi kupost hiyo picha
Wewe lengo lako ni kuharibu. Ok
Wewe endelea tu lakini sio poa
Ni ushamba huo.
I doubt that, umewahi panda basi wakati wa rush hour?Nairobi hawana BRT lakini mfumo wao wa public transport umekaa vizuri sana. Kwanza kama sikosei mabasi yote yanasimamiwa na kampuni au shirika, pili kuna nidhamu kwa abiria, hakuna kusimama na vilevile hakuna kugombania kuingia kwenye basi, abiria wanapanga mstari kistaarabu bila shuruti. Kwa kifupi niliupenda ule utaratibu.
Licha ya kwamba Dar es Salaam tumeleta BRT, kwa mwendo tunaoenda nao na kama huduma itaendelea kua ya kiwango hicho, mradi hautakua na tija na mwisho utakufa kabisa.
Wewe ni mtz au mkenya, ??Acheni kuua albino.
Annael MOTOCHINI game over mlicho weka hapa kinaeleweka, tatizo humu kuna mamluki wengi sana, kuna watu wapo kwenye payroll fulani. Nini kingumu kuelewa mpaka unashindwa kukaa kwenye mada? Nilitegemea wenzetu wangeweza kuelezea Nairobi wana safari vipi kila siku ili wasio juwa waweze kujifunza, lakini ni vijembe mwanzo mwisho (talking about building bridges.. huh).
Japo sina picha, kwa upande wengu mimi mabasi ya matatu ya Nairobi yana nishinda vitu viwili, muziki mkubwa, na speed. Unaweza kupanda matatu unapigiwa BASS mpaka ukasikia kama kichwa kinataka kupasuka. Sijuwi kina mama wajawazito wanawezaje kutumia usafiri na watoto wao tumboni. Speed ni swala lingine hatari, wakenya wanalijuwa vizuri.