ukifika ukiishi ukajionea na kupanda ndio utaelewa vizuri. binafsi naona public transports za nrb na dar zina utamaduni tofauti kabisaaaa.
matatu vs daladala, kuanzia aina za gari, nauli kupanda na kushuka kutegemea na muda (peak off peak) pimped brandings(zinaweza kuwa ukuta wa matangazo, utakuta zimechorwa wasanii, watu mashuhuri, celebrities etc na zimeandikwa jumbe na quotes ndani nje), musics aka hewa, mataa taa mengi kama gari za kusindikiza harusi au father christmass, seat belts for safety ingawa hazifungwi muda wote n.k, kuingia kwa kupanga mstari kwenye main stages aka vituo, aina za gari nyingi isuzu hizi ama zamani bongo tuliita chai maharage (hii inatokan na isuzu kuwa na assembling plant nrb na inawezekana inakua nafuu), lugha za makonda aka makanga. na umiliki wake ziko katika saccos aka sacco mfano wamasaa sacco, OngataLine sacco(hii ni classic kwa maana gari zake huwa ziko pimped mbaya) jamaa hadi wana tuzo za sacco ipi gari zake ziko Porsche....kuna zingine hadi ni first class... na kila sacco ina routes zake huu kiukweli ni utaratibu mzuri
haya tukirudi bongo gari zetu na zenyewe zina yake, kwanza ni comfortable hasa ukikuta hizi coaster zetu zikiwa bado mpya(sidhani na sijawahi ona matatu ya coaster nrb), hazipambwi pambwi unnecessarily. Nrb ukinunua gari kawaida tu kavu kavu ukaiweka barabarani hujaiwekea muziki au hewa wenyewe wanavoita n kuipimp basi biashara yako itakua hati hati. ni utamaduni tu. za bongo pia routes zimeandikwa mbele ila za nrb zinatumia namba.
Public train hizi za kupeleka watu Jijini dar ipo hata nrbi pia ipo. boda boda aka nduzi pia zipo ,bajaj ziko chache sanaaaa almost to nothing sio kama bongo.
boti /meli/ mitumbwi nrb hakuna bahari/ziwa/mito.
kifupi public transports ni utamduni wa nchi na nchi na watu. ni sawa kuanza kudadavua Beijing subway na London metro na New York subway