Mkandawile: huyu mtu yuko wapi sasa hivi?
Aliwahi kupata hela nyingi hadi akanunua daladla ambazo baadhi ya siku alikuwa yeye mwenyewe anafanya kazi kama kondakta, anakusanya hela akiwa amevaa suti na tai. Suti pia ndiyo lilikuwa vazi lake rasmi muda wote wa miaka minne alipokuwa anasoma UDSM, alikuwa anavaa suti kila siku hakuwahi kuvaa mavazi tofauti na suti
Huyu mimi nilimkuta akiwa Form Six mwaka 1990, na alikuwa nakaa Bweni la Azimio au Maendeleo, kama sikosei. Ni mtu mtaratbu mpole na mwenye hekima sana.
Kipindi alipokuwa yupo Pugu, yeye ndiyo alikuwa ni mwalimu msaidizi kwa wanafunzi wenzake wote wa FVII waliokuwa wanasoma somo la Chemistry (PCB na PCM). Yeye ndiye alikuwa anawafundisha pia wanafunzi wenzake wa FVI somo la Chemistry, ukiondoa mwalimu wa somo hilo
Kuna kipindi niliwahi kusikia alianzisha hadi shule huko maeneno ya Chanika. Huyu mtu yuko wapi siku hizi?