Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 180
- Thread starter
-
- #61
Hahahahaha!
Nakumbuka kipindi kile mchezo wa tausi wa kina mjuba na siti ulikuwa unapendwa kishenzi bongo na tulikuwa tunaangalia kila jumapili usiku pale mbele na dining hall karibu na bweni la ujamaa.
Jamaa alikera kichizi!
MImi nilimuacha mkandawire dada pale miaka ya mwanzo ya tisini, alikuwa anajitahidi aisee!!
I wish tungekuwa na alumni ya Pugu kwenye yahoo groups na vilevile tungefanya bash moja la karne hasa katika kipindi cha kumuenzi nyerere
Hivi yule ticha nyoka yuko wapi?
Sikusoma pugu najua ni boys skul, ila nilisoma tution za Mkandawile alipokuwa anafundisha mtendeni primary school na mchikichini, alinipatia elimu nzuri sana kwenye organic chemistry. Ila Siku hizi ana shule yake binafsi ipo mitaa ya Pugu. Inaitwa jina lake Mkandawile high school. Mambo yake siku hizi yapo swafiii.
Mkuu P53 Respect! Hapo kwenye bold nimecheka sana mzee......lile lijamaa lilikuwa noma sana!
Ha!ha!ha!haaaaa.....Mama Pendo + Pendo mwenyewe we acha tu....ile miandaazi yake ilikuwa poa kweli si tulikuwa tunampiga bao kweli.....ila kale ka Pendo.....mzee kalikuwa kametulia........! mzee unawakumbuka wale chokoraa...watoto wama ex Pugu boys.....hawana baba now? ...wakuu yeyote aliyegonga demu pale, si tulikuta vitoto vingi sana vya ma ex Pugu boys so please rudini mkacheki kuna damu zenu pale!
Mzee nilikuwa next to your class....EGM na mzee Msungu, Shire na yule teacher Mhaya wa Hesabu! Mkuu utakuwa ulikuwa na kina Mwatebele, Matobogolo Masalu etc sio?
Nakubaliana na wazo lako Mkuu na kama kuna nia kweli basi nitafanya juu chini kuwatafuta ex pugu students wote ninaowafahamu.
Huyo Mkandawile dada sikumkuta.Labda wana undugu na huyu Mkandawile mwingine au ni majina tu?
Daaah enzi za tausi ilikuwa tausi kweli.......ilikuwa kale ka intro ka tausi kakianza tu....utasikia machizi wanakimbia mabwenini kulekea pale nje bwaloni ha!ha!ha!..Tausi ndege wangu, ndege wangu wa fahari.......acha tu!.....Sitasahau pale mahali aiseee!
Kudadadeki!! yaani nyie mliona mpaka michezo ya tiviiii!!!!!!!!!!! nimemaind, sie tukiwa na akina nzowi tuliiishia kupokea wageni wa wizarani na mbio za mwenge tu!!! hakukuwa hata hivyo tivii...
Damn!!!! you lived in another world and not pugu
DOCEBIT VOS OMNIA!!!
MTM.....Usitake tucheke ndugu yetu...ha!ha!ha!ha!aaaaa!.......Hako kaTV kaliwekwa pale nje ya bwalo...just for Tausi na habari...then Juma wasi wasi...kang'oa kapeleka nyumbani kwake...tokea hapo no TV nafikiri mpaka leo mkuu!
Aisee nimecheka mpaka basi, yaani jamaa kaona mnafaidi siyo?? hivi Juma wasiwasi yuko wapi?
Naskia Charwe walimchapa makofi huko Kilosa... alizidi kuwaibia Tambaza na wattoto wa mjini wakija tuition kule pugu, jamaa alikuwa kama anakula ganja aisee jinsi alivyokuwa mpuzi
Mzee nilikuwa next to your class....EGM na mzee Msungu, Shire na yule teacher Mhaya wa Hesabu! Mkuu utakuwa ulikuwa na kina Mwatebele, Matobogolo Masalu etc sio?
Yule ticha Mhaya aliitwa Rwezaula!
Yes you got it bombii nyumbii! Kale kajamaa kalinipaga 27% kwenye test ya kwanza kabisa ya Mathematics........kalikuwa na mkwara sana kale kajamaa! bt really hesabu zilikuwa zinapanda....ila alikuwa mchoyo kumwaga utirio wote!
Duh... Aisee hizo tulikuwa tunaita namba za viatu!!
Ha!ha!ha!ha!haaaaaa! Kumbe MC nawe ni walewale wa DOCEBIT VOS OMNIA heeee!
Mkuu Mwal. Msungu alishatangulia mbele za haki.......! Kamanda Mabagala aka Mabags aliendaga UDSM......sijui yupo wapi now! Ila huyu jamaa alikuwa noma.....bed check, akikuta mmelala wawili anauliza cheti cha ndoa kipo wapi....h!ha!ha!haaaaa! Aliwatukimbisa hadi Pond ya kule Mapinduzi.......!tukala forest, noma sana yule jamaaa!
Yeah, mimi nilikuwa pale form 5/6 1994 - 1996, Mabagala alikuwa mwalimu wangu wa bweni, Azimio.
RIP Msungu (Majiman and Umememan)
Hii thread inanikumbusha mbali sana, Siku ya kwanza nilipofika tu ilikuwa siku ya Ubwabwa aka Uchele, kwa kuwa ilikuwa ndio tumefungua wanafunzi tulikuwa wachache kwa hiyo siku hiyo share ikamtosha kila mtu, mimi nikala kidogo kisha mwingine nikaumwaga, aaaa Madenti wa siku nyingi hapo wakanishangaa na kusema unamwaga uchele Pugu, wewe hauko serious na Utaukumbuka. Tehe tehe tehe ....... niliukumbuka wiki iliyofuata
Yeah, mimi nilikuwa pale form 5/6 1994 - 1996, Mabagala alikuwa mwalimu wangu wa bweni, Azimio.
RIP Msungu (Majiman and Umememan)
Hii thread inanikumbusha mbali sana, Siku ya kwanza nilipofika tu ilikuwa siku ya Ubwabwa aka Uchele, kwa kuwa ilikuwa ndio tumefungua wanafunzi tulikuwa wachache kwa hiyo siku hiyo share ikamtosha kila mtu, mimi nikala kidogo kisha mwingine nikaumwaga, aaaa Madenti wa siku nyingi hapo wakanishangaa na kusema unamwaga uchele Pugu, wewe hauko serious na Utaukumbuka. Tehe tehe tehe ....... niliukumbuka wiki iliyofuata