Next Level
JF-Expert Member
- Nov 17, 2008
- 3,153
- 180
- Thread starter
-
- #81
Vipi wakuu mnakumbuka yale maandamano tulifanya mwaka 1999 baada ya kifo cha Mwal.JK hai ukumbi wa Karimjee? mnakumbuka madikodiko tuliyokutana nayo pale Karimjee? ha!ha!ha sio mchezo!
Any plan for tomorrow......siku special ya ex Mwal. wa Pugu boys wakuu!
Mnawakumbuka TAASISI??
Mabagala alikuwa na kiduka karibu na Nyumba za walimu, siku moja watu wakaamua wamkasirishe kwa makusudi, bahati mbaya walifanya hivyo kwa kutumia kijana wa form one (sorry for him) ambaye alikuwa ni mgeni.
Walimpatia Sh 100, wakamwelekeza kiduka cha mabagala kilipo wakati huo mabagala mwenyewe alikuwa dukani, wakamwambia "We dogo nenda kwenye lile duka katununulie Mabagala tatu, mwambie muuzaji na chenji irudi.
Dogo kama alivyoelekezwa. "Shikamooo... Naomba Mabagala tatu na chenji irudi"
Jamaa alifunga duka, fikiria mwenyewe nini kilitokea.......
S0147 PUGU SECONDARY SCHOOL <H3>DIV-I = 19 DIV-II = 34 DIV-III = 56 DIV-IV = 182 FLD = 96
Ha!ha!ha!ha! LG......True! true kabisa......kumbe na weye ni ex Pugu Boy? Safi mkubwa.....!
Mkuu hapo kny bold ....that challenge is there to live mkuu......mpaka leo hii ukienda pale Pugu, vijana bado wana matatizo ya maji, chakula na sasa uchakavu wa majengo.......sijui kwa nini serikali haifanyii kitu ile shule aisee!
Oh No! Nilisikia juu ya Msungu mkali wa Jiografia (aliyegoma kufuga kuku wakati analetewa ale mayai ya bure) - sijui kama alikujaongoka baadaye na kuoa. Kumbe na Mphizikia Mugyabuso kaishia? Really sorry japo hakuwahi kunifundisha, alikomalia PCM (streams B,C,D) tu. Na Swai mwenye sauti nyembamba na mpole pia? Du! Ama kweli thread hii imenikumbusha mbali sana. Thanks!Unawakumbuka walimu wafuatao?Mabagara,Wajimira,Nzoi,Msungu(marehemu),Secondmaster Swai(marehemu),Headmaster Mtera,Mama Mukuru,Mzee Mukuru,Makono(marehemu),Teti,Mkwiche,Grace Chuma,Mamiro,Mama Mtera,Mbulanya,Godfrey Wasiwasi,Kaunda(mwalimu wa michezo 1984-1988),Mzava,Chamuriro,Mugyabuso(marehemu),Bakari Mbonde(Ex-Rufiji Mp)n.k Orodha yao ni wengi sana,waliotangulia mbele ya haki Mungu awaweke mahari panapostaili, aaaammmmmmiiiiiiiiiinnnn.
Ha!ha!ha!ha!ha!aaa...have got some of their pictures.....! Jamaa walikuwa wanajitolea kweli kuwasindikiza to mwisho wa Lami jioni wanapoondoka kupitia ''Bagdad''....ha!ha!ha!ha!haaa.......vile vibinti vilikuwa vipozeo vy fungus boys....sijui siku hizi bado wapo wale?
Mkuu mbona kipindi hicho hii shule ilikuwa imeshafanyiwa ukarabati wa nguvu na DANIDA na ilikuwa inaonekana ni bomba?? Wewe ulizia miaka ya nyuma ktk ya miaka ya 1980 hv jinsi ilivyokuwa imechoka.
Kila asubuhi mkondo mmoja lazima kuchota maji ya kupikia kila mwanafunzi ndoo sita kutoka Pondi,na jioni darasa lingine nalo huchukua nafasi.Kweli tunahaki ya kupata maisha tuliyonayo,Pugu wee acha tuuuuu.
Leo nimekumbuka sana Pugu seki na zile safari za kwenda Jangwani kwa Machagga na Tambaza kwa mama shija!!! wako wapi mama shija, machaga na yule mwalimu wa biology mwanamke wa pugu alifundisha PCB na charwe?
Leo nimekumbuka sana Pugu seki na zile safari za kwenda Jangwani kwa Machagga na Tambaza kwa mama shija!!! wako wapi mama shija, machaga na yule mwalimu wa biology mwanamke wa pugu alifundisha PCB na charwe?